Makapuku Forum

...naam, hujaniita ili nimeitika ili tuongee. Bado dakika 55 kukamilisha siku 365 za mwaka 2024. Tunakaribia kuuaga 2024.
Binafsi na kama wadau wa jukwaa hili, mwaka 2024 umekuwa ni mwaka mzuri na wenye changamoto za kibinadamu na mazingira. Tumepoteza wapendwa wetu lakini pai kuna mambo mengi mazuri yametokea upande wetu, kila kitu ni kushukuru.

Nikutakia mwisho mwema wa 2024 na kukunuia 2025 njema kwako na kwa kila uliye karibu na wewe.
Obe safarini Mtwara
 
Heri ya mwaka mpya watu wa Mungu.
Atoto Shunie Makiwendo Tresor Mandala mbalizi1 Poker Obe makaveli10 , Midekoo na wengine mje hapa tujadiliane ugumu wa januari
Asante kwa salamu za kheri mdau wa maana.
Ugumu wa Januari huwa haujadiliki maana kwanza kuna mambo ya shule kwa tunaowalea, hivi hii tabia ya kufungua shule mapema imeanzishwa mwaka gani, eti siku hizi kuna watoto wanatangulia mapema shuleni kisa wako madarasa ya mitihani, kwanini!!?

Toka hapo kwenye madarasa ya mitihani kufungua shule tarehe 6 jan, haki iko wapi. Unabagua wanafunzi, walimu wakuu wanapokea simu huku wanatooth pick mdomoni na hivyo wanashindwa kabisa kusikiliza kero tunazokutana nazo wazazi tukienda kulipa kwa control number, network ikiwa chini number haitoki, tarehe za mshahara zirudishwe nyuma au tulipwe wiki kwa wiki, teller anakuangalia kwa ushawishi ili uchomoe afuishirini kwenye ada, mwalimu anakasirika ukimwambia kuwa kuna makato ya shingiafutatu umeshindwa kukamilisha muamala

Tuachane na hayo sasa, unatoka kwenye kibanda cha mpesa, bodaboda anapita kavaa tshirt yenye picha ya Tundu Lissu unajiuliza kwani ubaya uko wapi kuhakikisha kuwa wakuu wa mikoa na marpc wawe wanapigiwa kura na kuchaguliwa na wananchi wa maeneo husika.

Wakati nawaza haya nagundua kabisa ni miaka kumi imepita leo tangu nipate kitambulisho cha NIDA na muda wake umekwisha. Wapi napaswa kurenew hiki kitambulisho ili nisiachwe na foleni ya wanaosubiri bima ya afya kwa kila mmojqa.

Bado unataka niendelee na masuala ya Januari mdau au niache nisikumalizie bando!

heri ya mwaka 2025 wadau wema wa jukwaa hili. Ndugu yenu nipo na mjue nini, hapa ni sehemu nzuri kuwepo sababu wewe upo
 
Asante binamu na kwako pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…