Valentine's Njema kwako wewe mdau wa jukwaa hili adhimu, naam mpo kama mimi ambao mazingira yanakulazimu kukaa mbali kidogo na kushindwa kujumuika na wote tunaowathamini.
Ndugu yenu nimekuwa na wakati mzuri sana, kuna mambo ya moyo na kuna mambo ya nafsi. Moyo una mwisho na unasahaulika lakini nafsi inaishi na haichakai. Leo mimi nimefanya mambo ya nafsi na nimefurahia.
Endelea kusambaza upendo na kuishi kwa kufuata nafsi inakuambia nini