Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo September 6, 2023.
Screenshot_20230906_063718_Opera%20Mini.jpg
 
Serikali ya India chini ya Waziri Mkuu Narendra Modi imebadilisha jina la India na kuipa Nchi hiyo jina la ‘Bharat’ katika kadi za mialiko ya chakula cha jioni zilizotumwa kwa Wageni watakaohudhuria mkutano wa kilele cha G20 wiki hii na kuongeza uvumi kwamba jina la Nchi hiyo litabadilishwa rasmi hivi karibuni.

Rais wa India, Droupadi Murmu alijitambulisha kama "Rais wa Bharat" badala ya "Rais wa India" katika kadi hizo zilizotumwa kwa Wageni wanaohudhuria mkutano wa G20.

India ni Mwenyeji wa mkutano unaofanyika kila mwaka wa G20 likiwa ni kongamano baina ya Serikali zinazojumuisha Nchi 19 pamoja na Umoja wa Ulaya Jijini New Delhi, Viongozi wengi duniani akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron watahudhuria.

Taifa hilo lenye zaidi ya Watu bilioni 1.4 linajulikana rasmi kwa majina mawili, India pamoja na Bharat lakini jina la India ndio linatumika zaidi ndani na nje ya Nchi hiyo. ‘Hindustan’ ni neno lingine linalotumika kuitambua Nchi hiyo na mara nyingi hutumiwa katika fasihi na aina nyingins za tamaduni maarufu nchini humo.

Mapema hii leo Vyomvo vingi vya Habari nchini India viliripoti kwamba Serikali inaweza kupeleka azimio la kubadilishwa kwa jina la nchi hiyo kutoka“India” na kuitwa “Bharat” wakati wa kikao cha Bunge maalum mwezi huu.
Screenshot_20230906_070539_Instagram.jpg
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano September 06, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi September 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3213 kwa lita, dizeli Tsh. 3259 na mafuta ya taa 2943.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi September 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi August 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Itakumbukwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano August 02, 2023 saa 6:01, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ilikuwa ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.
Screenshot_20230906_070727_Instagram.jpg
 
Uhaba wa mafuta ya petroli na dizeli kwenye vituo vya kuuzia mafuta katika Mji wa Babati Mkoani Manyara leo umepelekea foleni kubwa kwa Madereva bodaboda na magari madogo kutoka na nishati hiyo kupatikana kwenye kituo kimoja pekee katika Mji wa Babati.

Wakiongea na @ayotv_ baadhi ya Madereva wameomba Serikali kuangalia kwa jicho la kipekee suala la mafuta kwani wanahisi Wafanyabiashara hufanya hujuma kusubiri mabadiliko ya bei elekezi itakayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA)

Kwa upande wake Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Fue Chedieli amesema uhaba huo wa mafuta umetokana na urasimu wa Wasambazaji wakubwa kutowauzia Kwa wakati Wafanyabiashara wa mafuta na kusababisha adha kwa Wananchi huku akisema vituo vingine vinatarajia kushusha mafuta jioni leo hali itakayopunguza adha ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa Wananchi.
Screenshot_20230906_070829_Instagram.jpg
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imesema itaanzisha huduma ya upandikizaji ini ifikapo mwaka 2025 ikiwa ni mwendelezo wa azma ya Serikali kuhakikisha kwamba huduma za ubingwa bobezi zinapatikana nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya awali ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya ini yaliyofanyika Hospitali hapo katika kuelekea kwenye kongamano la Wataalamu wa Magonjwa ya Ini Barani Afrika (COLDA) linalotarajiwa kufanyika September 7 hadi 9 Jijini Dar es Salaam.

Prof. Janabi amesema katika kuelekea hatua ya upandikizaji ini mafunzo mbalimbali ya Wataalamu yanaendelea kutolewa kupitia Kituo cha kutoa mafunzo, uchunguzi na matibabu ya kibobezi ya Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na ini katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika kilichopo MNH kilichoanzishwa mwaka 2012 kwa ushirikiano na ufadhili wa Taasisi ya Munich Foundation ya Ujerumani, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili hivyo kuifanya Hospitali kuwa miongoni mwa vituo vichache vyenye hadhi ya namna hii Barani Afrika.

Vituo vingine vipo Rabat Morocco, Johannesburg Afrika ya Kusini na Cairo Misri.
Screenshot_20230906_071256_Instagram.jpg
 
‘Kivumbi leo’ hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kutangaza bei mpya za mafuta Septemba ambazo zimepaa huku maumivu zaidi yakiwa katika bei ya dizeli.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa jana Jumanne Septemba 5, 2023 saa 4 usiku na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk James Mwainyakule imeonesha kuwa kuanzia leo Jumatano Septemba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam Petroli itauzwa Sh3,213 na dizeli itauzwa kwa Sh3,259.

Bei hizo zinamaanisha kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam petroli imeongezeka kwa Sh14 kutoka Sh3,199 Agosti huku dizeli ikiongezeka zaidi kwa Sh324.

Hata hivyo kwa upande wa mikoa mingine yenye bandari zinazoshusha mafuta nchini pia bei ya mafuta imepaa; Mtwara kwa mwezi huu lita moja ya petrol itauzwa Sh3,285 ikiongezeka kutoka Sh3,271 na upande wa dizeli itauzwa Sh3,332 kutoka Sh3,008 mwezi uliopita.

Aidha, bei ya mafuta pia imepaa kwa mkoa wa Tanga ambapo kwa sasa lita moja ya petroli itauzwa Sh3,259 kutoka Sh3,245 Agosti huku dizeli nayo ikiongezeka zaidi kutoka Sh2,981 Agosti hadi Sh3,305.

Wakati hali ikiwa hivo katika mikoa mitatu yenye bandari, pia bei itang’ata zaidi mkoani Kagera katika eneo la Kyerwa (Ruberwa) ambapo petroli itauzwa Sh3,450 kwa lita na dizeli itauzwa Sh3,497 kwa lita.
Screenshot_20230906_071437_Instagram.jpg
 
Maderava bajaji, bodaboda na watu wenye magari binafsi wakiwa wameunga foleni huku wakiwa wamebeba geleni za kuwekea mafuta katika moja ya kituo cha mafuta kilichopo katikati ya mji wa Moshi, mkoani Kilimanjaro karibu na Stendi Kuu ya Mabasi Moshi kutokana na uhaba uliopo.
Screenshot_20230906_071546_Instagram.jpg
 
Balozi wa China nchini Niger, Jiang Feng, amesema nchi yake inakusudia kuchukua ‘jukumu la usuluhishi’ katika mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Mwanadiplomasia huyo ameyasema hayo katika mahojiano Jumatatu Septemba 4, 2023 kwenye televisheni ya taifa ya Niger, mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ali Mahaman Lamine Zeine, aliyeteuliwa na wanajeshi kushika wadhifa huo.

"Serikali ya China inakusudia kuchukua jukumu la kuwa mpatanishi ili kutafuta suluhisho la kisiasa la mzozo huu wa Niger," amesema balozi huyo katika mahojiano hayo.

"China inafuata misingi na kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, tunahimiza nchi za Afrika, kutatua matatizo yao kwa njia amani kupitia meza za mazungumzo,” amesema balozi huyo.

Duru za kisiasa zinabainisha kuwa China ni mshirika mkuu wa kiuchumi wa Niger, hasa katika sekta ya nishati.

Nchi hizo mbili zinajenga bomba la mafuta la kilomita 2,000 ambalo ni refu zaidi barani Afrika, linalokusudiwa kusafirisha mafuta ghafi kutoka mashamba ya Agadem (kusini-mashariki mwa Niger) hadi bandari ya Sèmè nchini Benin.

Visima vya mafuta vya Agadem vinatumiwa na kampuni ya mafuta ya China National Petroleum Corporation (CNPC), ambayo pia imejenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Zinder, kusini mwa Niger, chenye uwezo wa kubeba mapipa 20,000 kwa siku na kwamba kampuni hiyo ya China ina asilimia kubwa ya hisa katika kiwanda hicho.

Makampuni ya China pia yanafanya kazi ya ujenzi kwenye bwawa la Kandadji liliko Mto Niger, mradi wa pharaonic wenye thamani ya faranga za CFA bilioni 740 (sawa na euro bilioni 1.1), ulioko magharibi mwa nchi, ambao unapaswa kuzalisha GWh 629 kila mwaka ili kuwezesha Niger kujikomboa kutoka kwa utegemezi wake wa nishati kwa nchi jirani ya Nigeria.

Kufuatia mapinduzi hayo, Nigeria ililazimika kusitisha usambazaji wake wa umeme nchini Niger, kutokana na vikwazo vilivyoamuliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas).
Screenshot_20230906_071648_Instagram.jpg
 
Idadi ya Watanzania waliofariki katika ajali ya moto iliyotokea Alhamisi wiki iliyopita nchini Afrika Kusini, imeongezeka hadi kufikia 6 huku zoezi la kutambua miili likiendelea.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam, Balozi wa Tanzania nchini humo, Meja Jenerali mstaafu, Gaudence Milanzi, amesema idadi ya vifo imeongezeka kutoka 74 hadi 77.

“Suala la utambuzi linaendelea na limetokana na ushirikiano kati ya ubalozi na maafisa wa Serikali ya Afrika Kusini, mpaka sasa tumetambua miili sita za Watanzania,” amesema Milanzi.

Kuhusu taratibu za kusafirisha miili ya Watanzania hao kwa ajili ya maziko nchini, Balozi Milanzi amesema kuwa bado hawajaanza taratibu hizo, isipokuwa wameanza kufanya taratibu za kujua ndugu wa waliofariki.
Screenshot_20230906_071749_Instagram.jpg
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema nchi imeandika historia mpya kwa kuwakabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania wahamiaji wasiohamishika 3,319 ambao wameishi nchini kwa zaidi ya miaka 50 wakiwa na asili ya mataifa jirani ya Burundi, Comoro, Msumbiji na Rwanda.

Rais Dk Mwinyi amesema hayo leo tarehe 5 Septemba 2023 katika hafla ya kukabidhi vyeti vya uraia wa Tanzania kundi la Wahamiaji wasiohamishika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, Rais Dk Mwinyi amefurahishwa kutekelezwa ahadi yake aliyoitoa baada ya kuingia madarakani mwaka 2020 kwa kumalizika zoezi hilo na kuwafanya watambulike kuwa Raia wa Tanzania badala ya wahamiaji wasiohamishika.

Vilevile, Rais Dk Mwinyi ametoa wito kwa Idara ya Uhamiaji nchini kuziimarisha sheria zilizopo hususani sheria ya uraia wa Tanzania kwa kuwa sheria hii haijafanyiwa mapitio kwa kipindi kirefu kwa madhumuni ya kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowahusu wananchi na wageni wanaofika nchini.
Screenshot_20230906_071927_Instagram.jpg
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imepanga kuanzisha huduma ya kupandikiza ini kuanzia 2025.

Huduma hiyo inatajwa kuwa mwendelezo wa azma ya Serikali kuhakikisha huduma za ubingwa bobezi zinapatikana nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Mohamed Janabi amebainisha hayo wakati akifungua mafunzo ya awali ya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya ini, kuelekea kwenye Kongamano la Wataalamu wa Magonjwa ya Ini Bara la Afrika (Colda), linalotarajiwa kufanyika Septemba 7-9 jijini Dar es Salaam.

Amesema mafunzo mbalimbali ya wataalamu yanaendelea kutolewa kupitia kituo cha kutoa mafunzo, uchunguzi na matibabu ya kibobezi ya magonjwa ya mfumo wa chakula na ini, katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika kilichopo MNH.

Amesema kuwa kongamano la wataalamu wa magonjwa ya ini barani Afrika, ni moja ya maandalizi katika kusaidia huduma za upandikizaji ini kuanza kufanyika nchini.

"Kongamano litatoa fursa ya wataalamu kujifunza, kujadili na kupanga mwendelezo wa mafunzo ya mara kwa mara ya ndani na nje ya nchi ambayo yatawajengea uwezo wataalamu kuanzisha huduma ya upandikizaji ini nchini.

“Hii safari ni ndefu na nzito lakini tunaamini kwa msaada wa Serikali na wadau mbalimbali, tutafanikiwa kwani hadi sasa kituo kina uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa waliofanyiwa huduma hiyo nje ya nchi, pale wanaporejea nyumbani tofauti na awali ambapo walilazimika kurudi nje ya nchi," amesema.
Screenshot_20230906_072040_Instagram.jpg
 
Inaelezwa kuwa mpenzi wa Mason Greenwood Harriet Robson alikuwa sehemu ya walioangalia mazoezi ya Getafe leo (Timu mpya ya mpenzi wake)

Muda mfupi baada ya mazoezi ameshare picha kwenye insta story yake akionyesha kumsapoti mpenzi wake kwenye maisha yake mapya ndani ya Getafe .

Harriet ndiye aliyemletea shida leo yameisha maisha yanaendelea
Screenshot_20230906_072210_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom