Makapuku Forum

Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kwa kufanikiwa kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 baada ya kutoa suluhu na Algeria katika mchezo uliochezwa Uwanja wa 19 Mei 1956.

“Hongereni vijana wetu wa Taifa Stars kwa kufuzu michuano ya kuwania kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (2023 Africa Cup of Nations). Mmeandika historia kwani hii ni mara yetu ya 3 kufuzu tangu kuanzishwa kwa mashindano haya. Nawatakia kila la kheri.” aliandika Rais Samia.

Hii inakuwa mara ya tatu kwa Stars kufuzu kucheza fainali hizo, ikianza 1980, 2019 na sasa 2023.

Screenshot_20230908_092446_Instagram.jpg
 
Ni matumaini mapya. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya majaribio ya tiba ya virusi vya Ukimwi (VVU) kutarajiwa kuanza nchini Denmark kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Tiba hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu inatarajiwa kuanza baada ya matokeo ya majaribio ya awali ya maabara, yaliyofanywa na timu mbili za wanasayansi wa Australia kwa ushirikiano na wenzao kutoka Denmark kuonyesha matumaini ya kupata dawa.

Matumaini haya yanakuja ikiwa imepita miaka 40 tangu Ukimwi uingie Tanzania, huku takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zikionyesha karibu watu milioni 40 wanaishi na VVU duniani.

Mwakani pamoja na Denmark, majaribio ya dawa hiyo pia yataanza huko Melbourne, Australia. Utafiti wa Australia umehakikisha kuwa, dawa ya Oncologic venetoclax ina uwezo wa kuchunguza seli katika mwili wa binadamu ambazo zinaathiriwa na virusi, suala ambalo lilikuwa gumu kwa tafiti zote zilizofanywa kwa miaka 40 iliyopita.

Kutokana na uwezo wa dawa hiyo, vidonge vyenye jina la kibiashara la Venclexta vilitengenezwa awali ili kupambana na saratani ya damu.

Ilithibitishwa nchini Marekani mwaka 2016 na tangu wakati huo kwa mujibu wa madaktari, tayari imesaidia maelfu ya wagonjwa wa saratani.

Uchunguzi na hatimaye utumiaji wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo unawezesha kuzuia kuongezeka kwa virusi vya Ukimwi, hali inayozuia uharibifu wa kinga ya mwathiriwa mara moja.

Mwathirika anapotumia dawa za kufubaza makali kwa kufuata masharti ya dozi, virusi hupunguza kasi ya kuzaliana, lakini anapoacha huzaliana kwa wingi na kupunguza kinga za mwili, hivyo hupata magonjwa nyemelezi.

Screenshot_20230908_092710_Instagram.jpg
 
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametoa siku 90 kwa vituo vya kulelea watoto na wazee visivyo na usajili vikamilishe kwa mujibu wa sheria na watakaoshindwa wachukuliwe hatua.

Wakati Dk Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati akitoa maelekezo hayo, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa naye ametoa siku 90 kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa), kubadilika kifikra kwa kujiendesha kama sekta binafsi na kuondoa malalamiko.

Mawazri hao walitoa maagizo hayo jana jijini hapa kwa nyakati tofauti, ambapo Dk Biteko alizungumza alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa maofisa ustawi wa jamii nchini, huku Bashungwa akitoa maelekezo hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa wakala hao.

Dk Biteko ambaye alikuwa akimwamwakilisha Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango. Pia, alitoa maagizo tisa kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima ili kuboresha sekta ya ustawi wa jamii.

Miongoni mwa maagizo hayo ni kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia sera, sheria na miongozo, wamiliki wa makao ya watoto wanaogeuza vitega uchumi kuacha mara moja, waendelee kusuruhisha migogoro, kuwatambua na kuwapatia huduma watoto walio katika mazingira hatarishi.

Mengine ni maofisa ustawi wa jamii kuendelea kutoa elimu ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia, ulinzi na usalama wa watoto kwenye mikusanyiko, kuimarisha kampeni zihusuzo masuala ya ukatili, viongozi wa dini na wazee wa mila kukemea matendo maovu na mwisho wazazi na walezi kuzingatia wajibu wao.

“Waziri mwenye dhamana shirikiana na vyombo vya sheria ili kuwabaini wamiliki hao na kuwachukulia hatua za kisheria, natoa rai kwa watu na taasisi zote zinazotoa huduma za ustawi wa jamii katika vituo visivyosajiliwa kuvisajili haraka na mwisho ni siku 90 kuanzia leo,” alisema Dk Biteko.

Naibu waziri mkuu huyo alisema mmomonyoko wa maadili unasababisha madhara mengi katika jamii ikiwemo ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, migogoro ndani ya familia na ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

Screenshot_20230908_092854_Instagram.jpg
 
Wachezaji watano wa Kiafrika wanawania kutwaa tuzo ya Ballon d'Or, mojawapo ya tuzo zenye heshima kubwa katika ulimwengu wa soka.

BBC imewataja wanasoka hao kuwa ni pamoja na Asisat Oshoala, mshambuliaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria na klabu ya FC Barcelona ya Uhispania, ambaye kimsingi, ndiye mwanamke pekee kutoka barani Afrika aliyeteuliwa katika kipengele cha wanawake.

Wengine ni Victor Osimhen wa Nigeria, Mohamed Salah wa Misri, Andre Onana wa Cameroon na Yassine Bounou wa Morocco, ambao kwa pamoja wametajwa kwenye orodha ya wachezaji walioteuliwa 2023, baada ya kuwavutia mashabiki na wadadisi wa soka msimu uliopita.

Tuzo ya Ballon d'Or ni tuzo ya kila mwaka na washindi wa mwaka huu watatangazwa kwenye sherehe huko Paris, Ufaransa Oktoba 30. Mpaka sasa, Rais wa Liberia, George Weah, ndiye anabaki kuwa mwafrika pekee aliyewahishinda tuzo hiyo ya Ballon d'Or, akiwa anaichezea AC Milan mwaka 1995.

Screenshot_20230908_093022_Instagram.jpg
 
Wagombea wakuu wa upinzani katika nafasi ya urais wa Nigeria kupitia wanasheria wao wamesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama uliothibitisha ushindi wa Rais Bola Tinubu katika uchaguzi wa urais wa mwezi Februari ambao ulikuwa na utata.

Wagombea Atiku Abubakar wa chama cha People's Democratic Party na Peter Obi wa Labour Party's, ambao walishika nafasi ya pili na ya tatu kwenye uchaguzi huo, waliwasilisha mahakamani kesi ya kutaka uchaguzi ufutwe kwa madai ya wizi wa kura na mawakala kushindwa kuchapisha matokeo ya uchaguzi kupitia mtandao.

Lakini Mahakama ya rufaa ya Nigeria hapo jana ilitupilia mbali maombi yao katika hukumu ambayo iliyosomwa kwa zaidi ya saa 11.

Wakili wa Obi, Livy Uzoukwu, aliwaambia wanahabari kuwa timu yake itaipitia hukumu kikamilifu na kukata rufaa katika Mahakama ya Juu.

Rufaa katika Mahakama ya Juu nchini humo, rufaa inapaswa kuwasilishwa ndani ya 14 siku kutoka tarehe ya uamuzi wa mahakama na kwamba Mahakama hiyo ya juu, ina siku 60 za kusikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi wake.

Screenshot_20230908_093116_Instagram.jpg
 
Ikulu ya Kremlin imesema Rais Vladimir Putin, hana mpango wa kushiriki mkutano wa kilele wa mataifa 20 yaliyostawi kiviwanda na yanayoinukia kiuchumi (G20), hata kwa njia ya video.

DW imemripoti msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, akiwaambia waandishi wa habari kwamba shughuli zote katika mkutano huo, zitaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Lavrov, ambaye kimsingi, ndiye kiongozi wa ujumbe wa Russia mjini New Delhi.

Pia waziri huyo, ndiye aliyeiwakilisha Russia katika mkutano wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Brics, uliofanyika mwezi Agosti, mjini Johannesburg; ambapo kulikuwa na sintofahamu iwapo Afrika Kusini ingelazimika kumkamata Putin kutokana na ukweli kwamba, Afrika Kusini ni mwananchama wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Kwa upande mwingine, mkutano huo wa G20, unajiri huku kukiwa na uhusiano mbaya kati ya Moscow na nchi za Magharibi, uliosababishwa a mzozo unaoendela kati yake na Ukraine, ambao ulisababisha mvutano mkubwa katika mkutano kama huo mwaka jana, mjini Bali, nchini Indonesia.

Kwa mujibu wa DW, pia Rais wa China Xi Jingping, hatohudhuria mkutano huo wa G20 nchini India, Rais huyo anafanya hivyo huku kukiwa na vuguvugu la mvutano wa mpaka kati yake, Marekani na India.
Screenshot_20230908_093248_Instagram.jpg
 
Ni kawaida binadamu kujaribu vitu hata vile ambavyo wengine hudhani haviwezekani, hasa wakitaka jambo lao lifanikiwe. Duniani kote inafahamika kuwa sehemu anayoishi Rais, Malkia au Mfalme huwa na ulinzi mkali ambao si rahisi kuingia bila sababu za msingi.

Wakati watu wengine wakiwa na hofu ya kusogea katika lango la ikulu bila sababu ya msingi kutokana na ulinzi mkali, fahamu kuwa yupo mwanaume mmoja aliyewahi kuingia Kasri la Kifalme la Uingereza (Buckingham Palace), yalipokuwa makazi hayati Malkia wa Uingereza Elizabeth II, na kuzama hadi chumbani alikolala Malkia.

Screenshot_20230908_093409_Instagram.jpg
 
Services Offered:
  • Visa Consultation: We provide guidance on visa requirements, eligibility criteria, and application procedures for various countries.
  • Application Assistance: We help applicants complete visa application forms accurately and gather required documents.
  • Documentation Review: We review the applicant's documents to ensure they meet the embassy or consulate's requirements.
  • Appointment Scheduling: We assist in scheduling visa interviews or appointments with relevant authorities.
  • Visa Processing: We submit visa applications on behalf of clients and track their progress.
  • Expedited Services: We also offer expedited visa processing for urgent travel needs.
  • Visa Types: We handle various types of visas, including tourist, business, student, work, and immigrant visas.

Expertise:
  • We are typically well-versed in the specific requirements of different countries and visa categories.
  • We keep up-to-date with changes in visa regulations and application procedures.

When considering using a visa agency, it's essential you reach out to Bryte Sky Links, for your specific travel needs.
enlarge_bryteskylinks.jpg
 
Back
Top Bottom