Makapuku Forum

Makapuku Forum

Robert Lucas Mkazi wa Mtaa wa Ipogoro E Kata ya Ruaha Mkoani Iringa amekutwa amejinyonga chumbani na waya ya umeme kwa kujitundika katika paa la nyumba huku akiacha ujumbe uliosema ameamua kufanya hivyo kwasababu ya hila tu na asilaumiwe Mtu yoyote.

Pracilia Medard ni Mke wa Robert ambapo ameiambia @AyoTV_ kuwa yeye na Mumewe hawakuwa na ugomvi wowote na alikuwa haoneshi kama alikuwa Mtu mwenye huzuni bali alikuwa anaona Mume wake yuko sawa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema marehemu aliacha ujumbe unaosomeka “Mimi Robert Lucas nimezaliwa tarehe 29 /9/ 1975 nimeamua kufanya hivi kwasababu ya hila naomba Mke wangu msimsumbue wala Watoto wangu ninaoishi nao na kabla ya mazishi yangu naomba Mdogo wangu Rematus Lucas afike ndio nizikwe “

Mwenyekiti wa Ipogolo E amesema Robert alikuwa na Mtoto ambaye alikuwa anafaya mitihani ya darasa la 7 na Mtot huyo amechukuliwa na Mwalimu wake ili amliwaze huku akisubiri mazishi ya Baba yake.View attachment 2752269
Maisha haya, pole yake😟😟😟
 
CAF CONFEDERETION CUP
.
[emoji1241] SINGIDA FG Vs FUTURE FC [emoji1093]
[emoji354] 16:00
[emoji2522] Azam Complex
.
Singida wanatakiwa leo kupata matokeo mazuri nyumbani ili kupunguza presha mechi ya ugenini ambayo itakuwa ngumu zaidi kwao tofauti na ya mwanzo.
Screenshot_20230917_145631_Instagram.jpg
 
[emoji599] KOCHA wa Manchester United, Erik Ten Hag anadaiwa kumpa machaguo mawili supastaa wa kikosi hicho, Jadon Sancho ama kuomba msamaha hadharani au akubali kuendelea kusugua benchi.
.
Licha ya mabosi wa timu hiyo kuingilia kati, lakini Ten Hag amekataa kusamehe na kwa sababu hiyo, ripoti zinadai huenda akakubali kukaa nje hadi Januari, mwakani ambapo atajiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo au kusajiliwa moja kwa moja.
Screenshot_20230917_145728_Instagram.jpg
 
Farhan Kihamu

Nikisema huyu ni Ball Dancer wa kutisha mnasema mpira ni matokeo sio kuchezea mpira, nikiwapa takwimu zake za Ligi Kuu mnasema anatamba kwenye mechi ndogo, nikija na takwimu za Kimataifa mnasema mpira sio takwimu, ila huyu ndie Mchezaji bora wa muda wote kuwahi kutokea kwenye ardhi hii.

Huyu ndie kipimo cha Mchezaji bora kwenye hii nchi, kuna baadhi pia walikuwa wanasema aondoke! Guys huyu ni Mchezaji mkubwa wa mechi kubwa, utofauti nadhani mnauona.
Screenshot_20230917_145917_Instagram.jpg
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa ngazi zote kuacha kukaa ofisini na kushuka chini kusikiliza na kutatua kero ambapo ameeleza kusikitishwa kuona kero za Wananchi wa Vijijini zinapelekwa Ikulu wakati kwenye maeneo yao kuna Viongozi.

Akiongea na Wananchi leo Sept 17,2023 kwenye mkutano wa hadhara Masasi Mjini Mkoani Mtwara, Rais Samia amesema “Nitoe wito kwa Uongozi mzima wa Mkoa na ngazi zote hadi Uongozi wa Vijiji na Mtaa kusikiliza na kutatua kero za Wananchi, Waziri wa TAMISEMI amelisema vizuri hapa nami naomba nimuunge mkono, mtakaposhuka jamani, nyinyi sio Watawala, hata Mimi sio Mtawala, Mimi ni Mtumishi wa Wananchi, Mawaziri wangu ni Watumishi wa Wananchi, tuliowashusha chini huku kutuwakilisha ni Watumishi wa Wananchi”

“Unapoacha kiti cha Utumishi ukakaa kiti cha Utawala ndio maana huwezi kushuka kwa Mwananchi kwenda kumsikiliza, niombe sana Viongozi wa CCM simamieni hilo, Serikali hii mmeiweka nyinyi sasa mkijifanya wadogo na kufanya Watendaji kuwa wakubwa mnakosea, wasimamieni Watendaji warudi wakasimamie Wananchi”

“Haipendezi kuna Wasimamizi wa shughuli za Wananchi ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata mpaka Vijiji lakini unapokea pale Ikulu kero ya Mwananchi wa Kijiji inakuja kule Ikulu, haipendezi, tuliowaweka kwenye ngazi hizo mna kazi gani!?, kaeni vizuri fanyeni kazi zenu vinginevyo hatutowavumilia kupokea tena kero za Wananchi kule Ikulu wakati huku kuna Viongozi wapo”
Screenshot_20230917_151517_Instagram.jpg
 
Kutokana na uhaba wa maji ambao umelikumba Jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, mamlaka zinazosambaza maji zimewaagiza wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake, kupunguza matumizi.

Kwa mujibu wa BBC, taasisi hizo za Rand Water na Johannesburg Water, siku ya Jumapili zilisema kuwa matumizi makubwa ya maji kwa wakazi yanasababisha mfumo kuelemewa na hii inatokana na uwepo wa kiasi kidogo cha hifadhi ya maji.

Hivyo basi, taasisi hizo zimewataka wakazi kuokoa maji kwa kupunguza muda wa kuoga hadi dakika mbili, matumizi ya maji chooni na uoshaji wa magari, uwe ni mwishoni mwa wiki tena kwa kutumia ndoo.

Kampuni hizo pia zimewataka wakazi kuacha kujaza maji mabwawa ya kuogelea, hadi uhaba wa maji utakapoisha, lakini pia wametakiwa kuacha kumwagilia bustani na nyasi kwa majisafi na kurekebisha au kutoa taarifa kuhusu uvujaji wa maji.

Johannesburg kwa sasa iko chini ya vikwazo vya kila mwaka vya maji, ambavyo mara nyingi hudumu wakati wa kiangazi cha Afrika Kusini kati ya Septemba na Machi.

Katika wiki za hivi karibuni, baadhi ya wakaazi wa jiji hilo na taasisi kama vile hospitali zimekosa maji, na kusababisha kutoridhika kwa umma.
Screenshot_20230918_134940_Instagram.jpg
 
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko juzi alitembelea Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Agosti 30, 2023 kuongoza wizara hiyo.

Mradi huo umekamilika kwa asilimia 91.72, huku ukitarajiwa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme nchini utakapokamilika na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea mradi huo, Dk Biteko alimpongeza mkandarasi kwa kasi yake ya kutekeleza mradi huo wa kimkakati pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa usimamizi wake wa mradi huo na kueleza kwamba muda siyo mrefu wananchi wataanza kupata umeme wa uhakika..

"Nimefurahi kwamba mradi umefikia asilimia 91.72 na mkandarasi analipwa kila anapotoa certificate (hati ya malipo) yake. Kwa hiyo katika malipo yote anayodai, ameshalipwa asilimia 85.5 ya fedha zote ambazo ameziandikia certificate," alisema Dk Biteko.

Alisema changamoto ya umeme inayotokana na vyanzo vya maji kupungua, inatarajiwa kumalizwa kutokana na kuwepo kwa mradi huo na kwamba muda siyo mrefu wananchi wataanza kupata umeme wa uhakika.

Mradi huo wenye thamani ya Sh6.6 trilioni, unatarajiwa kuzalisha megawati 2115 za umeme, ambao utasaidia kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme nchini ambalo linatokana na upungufu wa maji kwenye mabwawa yanayotumika kuzalisha umeme.

Desemba 22, 2023 Rais Samia alishiriki hatua ya kufunga njia ya uchepusha maji na kuanza ujazaji wa maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme.

Screenshot_20230918_135119_Instagram.jpg
 
Taasisi ya kimataifa ya Global Fund imeonyesha wasiwasi katika mpango wa kutokomeza magonjwa ya Ukimwi, kifua kikuu na malaria kunakochangiwa na mabadiliko ya tabianchi.

Katika ripoti yao mpya iliyotolewa leo Jumatatu Septemba 18, 2023, taasisi hiyo inasema mabadiliko ya tabianchi na migogoro duniani, vinakwamisha juhudi za kimataifa za kupambana na magonjwa hayo matatu.

Ripoti ya taasisi hiyo ambayo ni mfuko wa kimataifa wa kupambana na maradhi hayo, inaonesha kwamba japokuwa miradi ya kupambana na Ukimwi, malaria na kifua kikuu imerejea kote duniani baada ya kuathiriwa na janga la virusi vya Uviko, lakini hivi sasa inakabiliwa na vikwazo vinavyotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na migogoro.

DW imeripoti kuwa kiongozi wa taasisi hiyo, Peter Sands amesema majanga ya kimazingira mfano wa mafuriko, licha ya kwamba yanaongeza idadi ya wagonjwa, lakini pia yanasabisha kuwepo ugumu katka kuwafikia wagonjwa kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande mwingine, ripoti hiyo imesema ongezeko la joto pia limefanya ugonjwa kama malaria kusambaa hata kwenye maeneo ambayo hapo awali hayakuwa na matukio ya maradhi hayo.

Bosi huyo wa mfuko huo amesema, hali inayoendelea sasa inatishia malengo ya kutokomeza magonjwa hayo matatu ifikapo mwaka 2030.

Screenshot_20230918_135222_Instagram.jpg
 
Serikali nchini Congo Brazzaville imezikosoa na kupinga tetesi za kuwapo kwa mapinduzi ya kijeshi nchini humo kama ilivyoripotiwa na mitandao ya kijamii.

Taarifa za nchi hiyo kupinduliwa na wanajeshi zilisambaa katika mitandao ya kijamii wakati Rais wa muda mrefu wa nchi hiyo, Denis Sassou Nguesso akiwa nje ya nchi kikazi.

Ufafanuzi huo umetolewa Jumapili usiku Septemba 17, 2023 na Waziri wa Habari, Thierry Moungalla aliyewatoa hofu wananchi na kuziita taarifa hizo kuwa ni uzushi.

"MUHIMU - Taarifa za uongo zinazoeleza tukio zito #Brazzaville. Serikali inakanusha habari hizi.

Tunaomba utulivu uendelee na watu waendelee na shughuli zao za kila siku," ameandika Waziri huyo katika mtandao wake wa kijamii wa X.
Screenshot_20230918_135349_Instagram.jpg
 
ROBERTINHO HUYU HAPA ::
.
“Tumecheza vizuri, ingawa tulikuwa na baadhi ya makosa ambayo yaliwapa nafasi wapinzani wetu, nilisema kabla hii timu ni nzuri (Power Dynamos) lakini bado nafasi yetu ni kubwa tutarudi imara zaidi tutakapokuwa nyumbani,”
.
“Tutakwenda kufanyia kazi changamoto ambazo tumekutana nazo, Simba ni timu kubwa itatengeneza ushindi mkubwa tukiwa mbele ya mashabiki wetu.”
.
Kocha huyo raia wa Brazili anasaka rekodi ya kuivusha timu kuingia makundi, kama alivyofanya na Rayon Sports 2018 na Vipers msimu uliopita, lakini akitaka kuingia katika historia ya makocha walioivusha Simba makundi ya CAF katika miaka ya hivi karibuni baada ya marehemu James Siang’a wa Kenya, Patrick Aussems na Sven Vandenbroeck kutoka Ubelgiji, Mhispania Pablo Martin.
Screenshot_20230918_135542_Instagram.jpg
 
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi licha ya kuwapongeza wachezaji wake amesema walistahili ushindi mkubwa zaidi ya huo dhidi ya wapinzani wao.Gamondi alisema bado hawajamalizana na Al Merrikh na amewataka wachezaji kusahau haraka matokeo hayo na kuanza kufikiria mechi ijayo ya Ligi Kuu ikiialika Namungo keshokutwa Jumatano, kisha kurudia mchezo wa CAF.
.
“Tulikuwa na dakika 90 nzuri, nawapongeza sana wachezaji wangu, licha ya ugumu wa mchezo hasa kipindi cha kwanza, ila walirudi kipindi cha pili na akili kubwa ya kutafuta ushindi na tukafanikiwa, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini nadhani tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu kulingana na jinsi tulivyotengeneza nafasi za wazi,”
.
“Mechi hii ya kwanza imekwisha, sasa tunatakiwa kuhamisha akili kwenye mechi ya ligi na baada ya hapo tutamalizana na wapinzani wetu hao wa CAF, nataka nikwambie bado hatujashinda, ushindi mzuri unatakiwa kuwa mechi hii ya pili, hata wao wanaweza kutufunga kwetu kama hatutakuwa makini.”
.
Kocha huyo anaisaka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza tangu mwaka 1998 kuivusha Yanga kuingia makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pia kuandika historia nyingine ya kuing’oa timu ya Sudan kwenye mechi za CAF tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo mwaka 1969.
Screenshot_20230918_135734_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom