Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya lep January 18, 2024.
Screenshot_20240118_070114_Opera%20Mini.jpg
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji (Mo) ametajwa na Jarida la Forbes kuwa tajiri namba 12 barani Afrika na bilionea kijana zaidi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.

Kwa mujibu wa jarida hilo mashuhuri ambalo hufuatilia ukwasi wa watu, ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita Mo amepanda kiutajiri barani Afrika kutoka nafasi ya 15 hadi 12.

Mbali na kupanda kiutajiri ukwasi wa mfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd (METL), umepanda kutoka Dola za Marekani 1.5 bilioni (Sh3.77 trilioni) mwaka uliopita hadi Dola 1.8 bilioni (Sh4.52 trilioni) jambo linalomfanya kuwa tajiri namba moja ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kwa ujumla ukwasi wa mabilionea 20 wanaoongoza Afrika uliongezeka kwa Dola 900 milioni (Sh2.26 trilioni) na kufika Dola Sh82.4 bilioni (Sh207.23 trilioni) mwaka 2024.

Upimaji wa ukwasi wa watu uliofanywa na Forbes uliangalia gharama halisi kwenye masoko ya mitaji na viwango vya kubadilishia fedha vilivyopo sokoni hadi Januari 8, 2024.

Screenshot_20240123_141407_InstaPro%20.jpg
 
Raia wawili wa Nigeria wanaotuhumiwa kuua na kutoweka na kichwa cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta (JKUAT), Rita Waeni (20) huko Kasarani nchini Kenya, wamekamatwa huku uchunguzi ukionyesha kuwa waliishi nchini humo kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa tovuti ya Nation, watuhumiwa hao ni William Ovie Opia, ambaye muda wake wa kuishi nchini humo umeisha, na Johnbull Asbor, ambaye hakuwa na kibali chochote cha kuishi nchini humo wakati anakamatwa.

Taarifa zinasema Asbor aliwaambia wapelelezi kwamba alipoteza vibali vya kusafiria miaka miwili iliyopita.

Watuhumiwa hao walifuatiliwa na Idara ya Uchunguzi wa Jinai (CRIB) hadi kwenye ghorofa moja huko Ndenderu, Kaunti ya Kiambu na kukamatwa Jumapili.

Konstebo Wangila kutoka ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) huko Kasarani, aliiambia mahakama ya Makadara jana Jumatatu ya Januari 22, 2024 kwamba watuhumiwa hao walikuwa wakiishi karibu na eneo ambalo kichwa cha Rita Waeni kilipatikana.

Miongoni mwa vitu vilivyopatikana katika nyumba ambayo watuhumiwa walikuwa wakiishi ni pamoja na Kisu, kitambulisho cha taifa cha Mkenya (jina linahifadhiwa), simu sita, kompyuta mpakato tatu na laini za simu 10.
Screenshot_20240123_141611_InstaPro%20.jpg
 
Ndugu wa wafanyabiashara wawili wa mbao waliopotea mwaka jana, wameliangukia Jeshi la Polisi nchini, wakitaka liwasaidie kuwatafuta ndugu zao.

Wafanyabiashara hao wa mbao Juma Iddi (45) na Haruna Iddi (50) walitoweka mnamo Desemba 28, 2023 saa 10 jioni katika maeneo tofauti ya Mwenge na Mghanga, mjini Singida

Akizungumza na Mwananchi Digital, mmoja wa wanafamilia hao, Seif Juma amesema wao kama familia hawana tena cha kufanya zaidi ya kuvisikiliza vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuwatafuta bila mafanikio tangu mwaka jana.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa alisema wamefanya taratibu zote za kipolisi na kuwasilisha makao makuu.

Juhudi za kumtafuta Msemaji wa Jeshi Polisi, SACP David Misime kulizungumzia suala hilo zinaendelea japo kuanzia saa tatu asubuhi ya leo, simu yake haikuwa ikipatikana.
Screenshot_20240123_141746_InstaPro%20.jpg
 
Mamlaka na taasisi nne za Serikali zimeanza uchunguzi wa kimaabara wa maji katika mto Ngerengere kutokana na kudaiwa kuchanganyika na povu linaloelezwa ni la kemikali, ambayo ni malighafi ya kutengeneza sabuni.

Mamlaka na taasisi hizo ni Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Maabara ya Maji na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (Nemc) Kanda ya Rufiji.

Mhandishi wa Mazingira wa Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu, Abdallah Mshana amesema wataalamu wameshachukua vipimo vya awali ili kuona kama kuna viashiria vya mabadiliko ya maji katika mto Ngerengere.

Akizungumza na Mwananchi Digital jana Januari 22, 2024 Mshana amesema timu ya wataalamu hao ilifika maeneo ya Nane Nane na Tungi ambako kulionekana povu jeupe kutoka kwenye korongo linalopitisha maji wakati wa mvua, ambayo yanatiririka kuelekea mtoni.

Januari 21,2024 kulionekana video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha povu jeupe, jamii ikiaminishwa kuwa ni mawingu yameanguka kutoka angani.
Screenshot_20240123_142008_InstaPro%20.jpg
 
Taarifa mpya
Lizzyash Ashliegh, ambaye ni chanzo cha kusambaa video kwenye mitandao ya kijamii akieleza yeye na wenzake wanne walipewa ujauzito kwa mpigo na mwanamuziki wa Marekani, Zeddy Will, ameibuka kukanusha.

Kupitia mtandao wa Tiktok, Lizzyash amesema hana ujauzito, bali kilichotokea ni kwamba walikuwa wakiandaa video ya muziki.

Lizzyash akisema hayo, taarifa zake za awali kuhusu yeye na wenzake wanne kuandaliwa sherehe kabla ya mtoto kuzaliwa (Baby Shower) zimeendelea kuonekana kwenye tovuti mbalimbali, zikiwamo Daily Mail, India Today, New York Post, The Economic Times na Complex.

“Usiamini kila kitu unachokiona kwenye mtandao. Hii imesambaa sana! Makala za runinga za habari zinazochapisha uandishi wa habari feki, mimi si mjamzito, hii ilikuwa kwa ajili ya video ya muziki ambayo sikuwa na ruhusa ya kusema hivyo,” ameandika Lizzyash kwenye mtandao wa Instagram.

Taarifa za awali

Katika hali ya kushangaza, mwanamuziki nchini Marekani, Zeddy Will amewafanyia sherehe wanawake watano aliowapa ujauzito kwa mpigo.

Sherehe hiyo kabla ya mtoto kuzaliwa (Baby Shower) imegeuka gumzo kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakihoji ni njia gani ameitumia kuwafanya wanawake hao kuelewana na kukubali kushiriki sherehe hiyo ya pamoja.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Mail, tukio hilo lilionekana kwa mara ya kwanza kupita mtandao wa kijamii wa Tiktok ambako picha ya mjongeo (video) ilichapishwa na mmoja wa wanawake hao.

Lizzy Ashleigh, ndiye alichapisha video hiyo huku akiweka wazi juu ya sherehe hiyo iliyofanyika Januari 14, 2024.

Mwaliko wa sherehe hiyo ulikuwa umeambatanishwa na maneno yasemayo, "Welcome little Zeddy Wills 1-5."

Wanawake wengine waliopewa ujauzito na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 ni Bonnie B, Jylene Vila, Kay Marie, na Iyanla Kalifa Galletti. @lizzyashmusic

Screenshot_20240123_142104_InstaPro%20.jpg
 
View attachment 2880474
Hahahahahaha...kidume hiki .safi sanq
 
Back
Top Bottom