Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo February 6, 2024.
Screenshot_20240206_072109_Opera%20Mini.jpg
 
Kitambo kidogo upo kama haupo, na huu ndiyo uzuri wa hili Jukwaa kwa sababu muda wote kuna watu wema wanakuwepo kupafanya hapa ndani sehemu nzuri kuwepo.

Kwa wenzangu na mimi, vijana wenye mambo ya kizee, wanaovaa saa ilhali kuangalia muda wanatumia simu za tachi,. Wanaopenda muziki wa kisasa ila wananunua album za miaka ya 90 kurudi nyuma watakuwa wanamkumbuka mwanamuziki wa country Toby Keith.

Naam, jamaa alikuwa anajua na hakuwahi kuonekana kutojua hata pale alipogundulika na saratani, mionzi ikasaidia kwa miongo miwili lakini mwili ni mwili, huwezi kuishi leo kama ulivyoishi jana na kesho siyo ya kwako. Laiti tungejua. Toby Keith kafariki mapema kuamkia leo (inategemea uko wapi-Makapuku ni kama utawala wa uingereza, kuna sehemu ni saa tisa mchana muda huu) na kama shabiki wa muziki wake, nimeona nikujuze na nitapandisha nyimbo zake mbili nazozipenda huku ule ambao naushabikia unaosema Nilikuwa bora jana sio leo, umri umesongea na sasa gari inabidi linahitaji kusukumwa (maneno yangu hayo-tafsiri unavyoweza), na tena kama kawaida nikivuna korosho zangu, huwa siachi kwenda kwenye hii bar.

Sababu nyingine ya mimi ndugu yako kunywa bia tatu za kwanza kumkumbuka huyu jamaa kabla sijaungana na kundi la wababa wa nyumbani kuagiza shots za kuwapa sababu ya kuchelewa kurudi nyumbani
Furahia maisha, you are not the younger you....


View: https://www.youtube.com/watch?v=-Fulz4ytZ54
 
Back
Top Bottom