Makapuku Forum

Makapuku Forum

[emoji2788]: “Sikumpa presha, niliongea na Guede, nikamwambia unapaswa kufunga, nakusapoti, unajua wakati mwingine anakosa nafasi, nikamwambia tulia, magoli yatakuja.
.
“Kiukweli Guede ni straika mzuri, anafiti kabisa katika mfumo wetu wa uchezaji. Ni mzuri katika mipira ya juu, kimbinu ni mzuri pia, kwetu yeye (Guede) na Okrah usajili wao katika dirisha dogo ni mzuri sana.” - Kocha Miguel Gamondi.

Screenshot_20240223_075942_InstaPro%20.jpg
 
Mshambuliaji was West Ham Michail Antonio amewaombaradhi Liverpool kwa kauli yake aliyoitoa mwanzoni mwa msimu akisema msimu huu West Ham itamaliza ligi ikiwa juu ya Liverpool

“Mwanzoni mwa msimu nilitoa kauli kwamba msimu huu tutamaliza msimu juu ya Liverpool yale yalikuwa mawazo yangu binafsi lakini nitumie fursa hii kuwaomba radhi wachezaji na mashabiki wa Liverpool kwa kauli ile”

Kazi kwenu mashabiki wa Liverpool kuhusu kuipokea radhi ya Antonio lakini kwenye msimamo nukta muhimu ni kwamba West Ham ipo chini ya Manchester United
Screenshot_20240223_080109_InstaPro%20.jpg
 
Kiungo wa Real Madrid ya Hispania Toni Kroos amethibitisha kuwa atarudi kuitumikia timu yake ya Taifa ya Ujerumani kwenye mashindano ya EURO 2024 Mwaka huu na kishaa atatangaza Rasmi kustaafu timu ya Taifa..

Mwaka 2020 Alitagaza kustaafu kuitumikia timu ya Taifa Ila ameamua kufuta uamuzi wake wa awali na Atatürk Mzigoni

Alipoulizwa kuhusu uamuzi huu amesema ameshawishiwa na squad ya sasa ya timu hiyo na anaamini itafanya makubwa kwenye EURO
Screenshot_20240223_080204_InstaPro%20.jpg
 
Rashidi Hussein Mkayala Mkazi wa Mtaa wa Gemu Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji amejinyonga kwa kutumia kilemba chake cha kichwani muda mfupi baada ya kumuua Mke wake, Bernadeta Cosmas(33) kwa kumnyonga chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro ndani ya ndoa yao.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Buswalu Mulumbu Mkama ameiambia @ayotv_ kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokea siku za nyuma ambapo Mke wa marehemu alifika kwa Mwenyekiti na kutoa taarifa ya vitendo vya Mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza ambapo mara kadhaa kesi zao zilikuwa zikipelekwa kwake kwa ajili ya usuluhishi.

Mwenyekiti huyo amesema siku moja kabla tukio Mwanamke huyo alilala nyumbani kwake baada ya kukimbia nyumbani kwa Mume wake kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa Mume wake ambapo katika tukio hilo alidai kunusurika kuuawa baada ya kukabwa shingo na waya wa umeme na alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbia na kukimbilia kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo umeonesha kuwa Rashidi Hussein alimnyonga Mke wake kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kupitia dirishani ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.
Screenshot_20240223_080520_InstaPro%20.jpg
 
Ni picha ya nyumba iliyopo Mwanga Kusini, Kigoma ambamo Mwanaume aitwae Rashidi anadaiwa kumuua Mke wake Bernadetha kisha na yeye kujinyonga ndani ya nyumba hiyohiyo baada ya kutokea mgogoro kati yao.

Kama ulipitwa ni kwamba Rashidi ambaye ni Mkazi wa Mtaa wa Gemu Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji alijinyonga kwa kutumia kilemba chake muda mfupi baada ya kumuua Mke wake, Bernadeta Cosmas(33) kwa kumnyonga chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro ndani ya ndoa yao.

Mwenyekiti wa Mtaa huo, Buswalu Mulumbu Mkama ameiambia @ayotv_ kuwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliotokea siku za nyuma ambapo Mke wa marehemu alifika kwa Mwenyekiti na kutoa taarifa ya vitendo vya Mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza ambapo mara kadhaa kesi zao zilikuwa zikipelekwa kwake kwa ajili ya usuluhishi.

Mwenyekiti huyo amesema siku moja kabla tukio Mwanamke huyo alilala nyumbani kwake baada ya kukimbia nyumbani kwa Mume wake kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa Mume wake ambapo katika tukio hilo alidai kunusurika kuuawa baada ya kukabwa shingo na waya wa umeme na alipopata nafasi ya kuchomoka alikimbia na kukimbilia kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo umeonesha kuwa Rashidi Hussein alimnyonga Mke wake kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kupitia dirishani ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.
Screenshot_20240223_080618_InstaPro%20.jpg
 
Wengi waliofuatilia kurasa za Millard Ayo na kuisoma habari ya Mwanaume Mkazi wa Kata ya Mwanga Kusini, Kigoma kudaiwa kumuua Mke wake kwa kumnyonga kisha na yeye kujinyonga, wameonesha masikitiko yao kutokana na tukio hilo na wengine kutamani kufahamu zaidi chanzo cha migogoro na umri wa ndoa hiyo.

Kwa mujibu wa Mtu wa karibu wa Familia, ndoa ya wawili hao ( Rashidi Mkayala na Bernadetha Cosmas) ilifungwa September mwaka 2022, hivyo hadi sasa ina muda wa mwaka mmoja na miezi minne japokuwa uhusiano wao ulianza miaka mingi iliyopita hata kabla ya kufunga ndoa na walifanikiwa kupata Mtoto mmoja wa kiume ambaye ana zaidi ya miaka saba kwa sasa.

Kaka wa Marehemu Bernadetha ameiambia @AyoTV_ kwamba Dada yake alimpigia simu saa tatu asubuhi na kumuomba amfate nyumbani kwa Mwenyekiti wa Mtaa alikokimbilia na kupewa hifadhi toka jana yake baada ya kukimbia kipigo cha Mume wake.

“Aliniambia jana Rashidi amenipiga kidogo aniue, alichukua nyaya za cable za TV (av cable) na kwenda kuziuza lakini mimi akaniambia zimeungua, baadae akaanza kunipiga nikamtuma Mtoto akimbie kumuita Mwenyekiti ambaye alikuja kunichukua ndio nikalala kwake”

Kaka huyu wa Marehemu amesema alimchukua Bernadetha na kwenda nae kwa Rashidi kwa nia ya kusuluisha lakini Rashidi alionekana kuwa mkali akihoji Mke wake amelala wapi usiku wa jana ——> “Dada yangu alisema anataka talaka lakini Mwanaume akasema siwezi kuachana na wewe sababu umeshanipa kovu la maisha, nikamwambia Dada yangu oga twende Ustawi wa Jamii lakini Mume wake alitoka na kusimama mlangoni na kuniapia kwa jina la Marehemu Mama yake kwamba hatompiga tena, Dada akabaki akasema anajiandaa kisha anifate.......mimi nikaondoka”

“Ilipofika saa 10 nikampigia akapokea nikamwambia mbona hujatokea ? akasema anamalizia kuoga…. hiyo simu ndio ikawa ya mwanzo na mwisho, nilipompigia baadae hakupokea nikampigia Baba naye akasema hapokelewi, baadae tulivyokuja nyumbani kwao tukakuta pamefungwa ambapo Polisi walituruhusu tuvunje mlango na tulipovunja maiti ya kwanza nimekutana nayo mlangoni ni ya dada yangu, Mwanaume naye kajinyonga” ——— Kaka wa Berna. #MillardAyoUPDATES #RIP[emoji1545]
Screenshot_20240223_080750_InstaPro%20.jpg
 
Mahakama Kuu Nchini Kenya imeamuaw kuwa kuanzia sasa Wafungwa wote wanaotumikia kifungo gerezani pamoja na Mahabusu, wanayo haki ya kuhudhuria maziko ya Ndugu zao wa karibu wa Familia na kusisitiza kuwa hatua hiyo sio tu ni sehemu ya kulinda haki za Binadamu lakini itawasaidia Wahusika kuwa sawa kihisia.

Jaji wa Mahakama hiyo Lawrence Mugambi ametoa uamuzi huo huku akisema hata hivyo kama kutakuwa na mazingira ambayo yatafanya suala hilo kuwa gumu taratibu zitazingatiwa ili ruhusa itolewe kwa umakini “Mfano kama Mfungwa alihukumiwa kwa kosa la mauaji na Ndugu wa aliyeuawa wapo msibani hii itahatarisha usalama wa Mfungwa anapokwenda kuzika hivyo ni sawa kutotoa ruksa”

Uamuzi huu unakuja baada ya Mfungwa Moses Dola wa Gereza la Kiambu kuwasilisha ombi Mahakamani akilaani kitendo cha kuzuiwa kwenda kumzika Mama yake July 12,2021 akisema kitendo hicho kimemnyima haki yake ya kibinadamu.

Umeonaje
Screenshot_20240223_145953_InstaPro%20.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya, Miriam Mritabna mwenzake Revocatus Muyella maarufu kwa jina la Ray.

Hukumu hiyo inasomwa leo Ijumaa Februari 23, 2024 na Jaji Edwin Kakolaki aliyeisikiliza.

Washtakiwa hao, Miriam na Muyella wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji ya kukusudia la kumuua Aneth Elisaria Msuya (wifi wa Miriam) aliyekuwa mdogo wa Bilionea Msuya.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali nyumbani kwake Kibada Kigamboni, Dar es Salaam Mei 25, 2016.

Katika hukumu hiyo Jaji Kakolaki ameanza kwa kurejea shtaka linalowakabili kisha ushahidi wa upande wa mashtaka akifanya muhtasari wa ushahidi wa kila shahidi.

Kisha atarejea utetezi wa washtakiwa kabla ya kuchanganua namna gani upande wa mashtaka umeweza au umeshindwa kuthibitisha shtaka bila kuacha shaka kwa washtakiwa wote.

Screenshot_20240223_150234_InstaPro%20.jpg
 
Wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ikiendelea kusoma hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha, Erasto Msuya maarufu kama Bilionea Msuya; Miriam Mritabna na mwenzake.

Idadi ndogo ya ndugu wa pande zote wamejitokeza kusikikiza hukumu hiyo, tofauti na kesi nyingine, huwa wengi hadi kukosa nafasi ya kukaa.

Leo Ijumaa Februari 23, 2024 ndugu, jamaa na marafiki wa washtakiwa na wale wa upande wa walalamikaji wameweza kuingia wote katika ukumbi namba moja wa Mahakama hiyo na kukaa bila changamoto yoyote ikilinganishwa na kesi kama ya kina Halima Mdee, idadi ya watu ilikuwa kubwa na kushauriwa wengine wakae nje ya chumba cha Mahakama wasubirie uamuzi.

Washtakiwa hao, Miriam na Muyella wanakabiliwa na shtaka moja la mauaji ya kukusudia la mauaji ya Aneth Msuya (wifi wa Miriam) aliyekuwa mdogo wa Bilionea Msuya.

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali nyumbani kwake Kibada Kigamboni, Dar es Salaam Mei 25, 2016.

Screenshot_20240223_150344_InstaPro%20.jpg
 
Watumiaji wa Barabara ya Kilwa wamejikuta kwenye adha ya foleni kubwa ya magari kuanzia Mbagala leo Ijumaa asubuhi Februari 23, 2024 baada ya kutokea ajali iliyohusisha gari ndogo na lori eneo la Mtoni wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Screenshot_20240223_150520_InstaPro%20.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, bilionea Erasto Msuya.

Miriam pamoja na mshitakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wanadaiwa kumuua kwa kumchinja, Aneth Elisaria Msuya ambaye ni wifi yake Miriam.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, Miriam na mwenzake Muyella wanadaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia Mei 26, 2016 huko nyumbani kwa Aneth, Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Aneth alikuwa mdogo wa bilionea Msuya, aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwa kutumia bunduki ya kivita aina ya SMG eneo la Mijohoroni, Barabara Kuu ya Moshi-Arusha wilayani Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Agosti 7, 2013.

Hukumu hiyo inayotarajiwa kusomwa na Jaji Edwin Kakolaki aliyeisikiliza kesi hiyo, ndio itakayoamua hatima yao iwapo wana hatia au la.
Na kama wana hatia, adhabu ni kunyongwa hadi kufa na kama hawana, wanaweza kuachiwa huru.

Mpaka leo hukumu hiyo inapotolewa, washitakiwa wameishi mahabusu kwa takribani miaka minane wakisubiri kukamilika kwa usikilizwaji wa kesi, kwa kuwa shtaka la mauaji linalowakabili halina dhamana kwa mujibu wa sheria nchini.

Screenshot_20240223_150616_InstaPro%20.jpg
 
CAF CHAMPIONS LEAGUE
.
[emoji1081] ASEC MIMOSAS [emoji739] SIMBA SC [emoji1241]
[emoji354] 22:00
[emoji2522] Stade Felix Houphouet
.
Kama ilivyo kauli mbiu ya Simba “Nguvu Moja”, mashabiki wa soka leo usiku watakuwa kitu kimoja wakiombea Simba ishinde ugenini dhidi ya ASEC, lakini kesho jioni Galaxy akiwa nyumbani aambulie sare dhidi ya Wydad. Lakini matokeo yakiwa tofauti bado Simba italazimika kutumia nguvu kwenye mechi ya mwisho nyumbani huku ikisikilizia na matokeo mengine ili kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Kila la kheri Simba.
Screenshot_20240223_151014_InstaPro%20.jpg
 
Taarifa za uhakika ni kwamba Ihefu SC imehamia mkoani Singida hii ni baada ya kuuchagua uwanja wa CCM Liti kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu mzima.

Leo watendaji wote wa timu za ligi kuu wametumiwa taarifa rasmi ya kuwa michezo yote ya nyumbani ya Ihefu SC itachezwa CCM Liti, Singida, Taarifa ya Bodi imesema kuwa Ihefu SC itatumia uwanja wa CCM Liti Singida badala ya HIGHLAND ESTATE, Ubaruku, Mbeya.

Wakati huohuo, Singida Fountain Gate FC imeuchagua uwanja wa CCM Kirumba kama uwanja wao wa nyumbani mpaka mwishoni mwa msimu huu.

Screenshot_20240223_151121_InstaPro%20.jpg
 
Wapo wanaoutazama mchezo wa ASEC Mimosas vs Simba kama mchezo mwepesi kwa Simba kwa sababu ASEC Mimosas tayari imefuzu hatua ya mtoano [Robo Fainali], kwa hiyo hawana presha wala hawana cha kupoteza.

ASEC Mimosas imejengwa kama platform kwa wachezaji kuonesha uwezo wao na kuondoka kwenda mataifa ya Ulaya kama Ufaransa, Austria, Ubelgiji, na klabu kuingiza pesa kupitia mauzo ya wachezaji.

Kwa hiyo mechi za CAF kwa ASEC Mimosas ni soko kubwa la kuonesha vipaji vya wachezaji wao, kila mchezaji anaepata nafasi anataka kuonesha ubora wake ili kutengeneza thamani yake sokoni.

Dirisha la usajili lililopita wamemuuza Pacome, Kramo, Yao Kwasi, dirisha la usajili la msimu uliopita walimuuza Stephane Aziz Ki na wengine walienda Ulaya. ASEC Mimosas imeshajipambanua katika biashara ya kuuza wachezaji, licha ya kufuzu hatua ya Robo Fainali lakini wanatafuta uhakika wa kuuza wachezaji wao.
Screenshot_20240223_151247_InstaPro%20.jpg
 
ASEC MIMOSAS V/s SIMBA ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili, lakini ni muhimu zaidi kwa Simba kwa sababu bado haijafuzu hatua ya Robo Fainali, ASEC Mimosas yenyewe tayari imejihakikishia kucheza Robo Fainali.

Katika mchezo huu Simba inahitaji alama tatu au alama moja, endapo itapata alama tatu itafikisha alama nane na ikiwa itashinda mchezo wa mwisho nyumbani [Benjamin Mkapa Stadium] dhidi ya Jwaneng Galaxy itakuwa imefuzu Robo Fainali.

Ikitokea leo Simba ikapata alama moja itafikisha alama sita, kama itashinda mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy itafikisha alama tisa. Alama hizo zinaweza kufikiwa na Wydad kama itashinda mechi zake mbili dhidi ya Jwaneng Galaxy na ASEC Mimosas.

Kama Simba na Wydad zitalingana alama, Simba ina faida ya kushinda kwa idadi kubwa ya magoli katika mechi mbili ambazo timu hizo zilikutana. Simba ilipoteza 1-0 dhidi ya Wydad ugenini lakini ikashinda 2-0 nyumbani.

Kama Simba itapoteza leo dhidi ya ASEC Mimosas halafu Wydad ikashinda dhidi ya Jeaneng Galaxy, Simba itakuwa kwenye wakati mgumu sana wa kufuzu kwa sababu hata ikishinda mchezo wa mwisho itafikisha alama nane na Wydad ikishinda mchezo wa mwisho itafikisha alama tisa.

Kwa hiyo ili Simba iendelee kubaki na matumaini makubwa ya kwenda hatua ya Robo Fainali inapaswa kupata alama tatu au moja kwenye mchezo wa leo dhidi ya ASEC Mimosas.
Screenshot_20240223_151334_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom