Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nakusalimu sana Makiwendo popote utapomuona Atoto mwambie amfikishie Shunie salamu zangu nampenda sana.

Uhali gani moudgulf nimatumaini yangu umzima wa afya hofu ni kwa Mideko maana sikuiz yupo busy sana kama Lee

Mshua master Tresor Mandala vp weekend inasemaje au imepooza kama uji wa Carasco Putin

Siku zote mshamba_hachekwi sasa sielewi kwanini Depal na udugu wake cocastic wanamcheka mtumishi Saint Anne

Mzee mwenzangu Grahams msalimie sana Lovelovie mwambie niko mwanza hapa pspf nimetoka kupokea kiinua mgongo changu.
Boss wangu Mjep nakusabahi popote ulipo nashkuru kwa offer ya full tank ya mafuta.

Papa mobimba raraa reree ukifa hauozi mkuu. Wasalimie wale wana wote wa misifa camp Kelsea
😁
 
[emoji187] “Takwimu zinatuonyesha Kevin De Bruyne ni bora kuliko Zinedine Zidane. Macho yetu yanatuambia Zidane ni bora kwa mbali kuliko staa huyu wa Manchester City na timu ya taifa ya Ubelgiji. Takwimu zinatuonyesha Cristiano Ronaldo ni bora kuliko Diego Maradona na Ronaldo De Lima. Hali halisi inatuambia hao wawili ni bora kuliko Ronaldo. Hapa ndipo linapoibuka suala la Kibu.
.
Hana mabao mengi lakini kuna kitu ambacho Simba wanakiona kwa Kibu kuliko kwa wachezaji wengine. Ukiwaambia Simba nani aondoke kati ya Kibu au Freddy Michael watakwambia Freddy aondoke ingawa ni huyu huyu amefunga mabao mengi kuliko Kibu. Soka la namba linatuchanganya katika dunia ya kisasa. Unajaribu kushindana na hali halisi. Hapa ndipo Kibu anapohitaji pesa nyingi katika mkataba wake. Hapo ndipo Kibu anadengua.” — Edo Kumwembe.View attachment 2982548
Amenena vema ingawa siungani naye
 
Magazeti ya leo May 7, 2024.
Screenshot_20240507_073725_Opera%20Mini.jpg
Screenshot_20240507_073757_Opera%20Mini.jpg
 
Mabosi wa Simba wameshatuma mtu kwa beki wa kati wa ASEC Mimosas, Anthony Tra Bi Tra (25). Hesabu za vigogo hao wa Simba zinakuja baada ya kutokuwa na uhakika wa kubakia msimu ujao kwa beki wa kikosi hicho, Henock Inonga ambaye taarifa zinaeleza mwishoni mwa msimu huu anaweza kuondoka ili kutafuta changamoto mpya huku FAR Rabat ya Morocco ikimuhitaji.
.
Tra Bi Tra ameiongoza ASEC Mimosas kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku akionyesha nia ya dhati ya kutaka kuondoka kutafuta changamoto mpya baada ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 2021 akitokea FC Foix.
.
Tayari mabosi hao wameanza kujipanga mapema baada ya kuona ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni ngumu kuuchukua kwani watani zao Yanga wako kwenye nafasi nzuri ya kuuchukua kwa mara ya tatu mfululizo jambo ambalo hawataki litokea msimu ujao.

Simba mpaka sasa ina asilimia kubwa ya kumpata beki mzawa wa Coastal Union, Lameck Lawi mwenye uwezo wa kucheza nafasi tatu tofauti kuanzia beki wa kati, beki wa kushoto na kiungo wa kati jambo linalowafanya kuhamishia nguvu kwa nyota wa kigeni.
Screenshot_20240507_145913_InstaPro%20.jpg
 
BADO HAJAMALIZA
.
03 —MO Salah ni mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kufunga mabao 10+ na kutoa asisti 10+ kwenye misimu mitatu mfululizo. Pia ni staa wa pili pekee kuwa na uwiano wa kufanya hivyo katika misimu mitano tofauti baada ya Wayne Rooney.
Screenshot_20240507_150042_InstaPro%20.jpg
 
Serikali imefanikiwa kusajili Wanafunzi 22,131 wakiwemo Wasichana 2,794 wa elimu ya Sekondari kwa njia mbadala katika vituo vya elimu ya Watu Wazima pamoja na kutoa mafunzo ya kisomo kuimarisha stadi za Kusoma, kuandika na Kuhesabu kwa Watu wazima 6,238 katika Mikoa 26.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda amesema hayo leo May 06,2024 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/2025 ambapo amesema kuwa Serikali imekamilisha moduli 11 za hatua ya I na ll kwa ajili ya vituo 151 vya elimu ya sekondari kwa njia mbadala ili kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika vituo hivyo.

Amesema Serikali imeongeza idadi ya vituo vya elimu ya sekondari kwa njia mbadala kutoka 168 hadi kufikia 190 kwa lengo la kuongeza fursa kwa wanafunzi waliokosa elimu kwa sababu mbalimbali.
Screenshot_20240507_150216_InstaPro%20.jpg
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema katika kuimarisha uthibiti ubora wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Serikali pamoja na mambo mengine itanunua magari matatu kwa ajili ya shughuli za uthibiti ubora wa Shule katika Halmashauri ya Mlele, Tunduma na Serengeti.

Akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2024/2024, Prof. Mkenda amesema “Serikali itafanya tathmini ya jumla katika asasi 6,620 (Shule za awali na Msingi 4,965, Sekondari 1,525, Vyuo vya Ualimu 66, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 14, na Vituo 50 vya elimu ya Watu wazima na mafunzo nje ya mfumo rasmi)”

“Serikali pia itafanya ufuatiliaji na tathmini kwa lengo la kubaini ubora katika uandikishaji, ufundishaji na ujifunzaji, usimamizi na ongozi na kutoa ushauri kwa Walimu wa masomo katika Taasisi 1,010 na itaendelea na ujenzi wa ofisi ya uthibiti ubora wa shule katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na ukarabati wa ofisi nne za uthibiti ubora wa shule katika Halmashauri ya Mpwapwa, Chato, Mpanda na Halmashauri ya Mji - Ifakara na itanunua samani na vitendea kazi katika ofisi 210 (Halmashauri 184 na Mikoa 26) za uthibiti ubora wa Shule”
Screenshot_20240507_150321_InstaPro%20.jpg
 
Back
Top Bottom