Makapuku Forum

Makapuku Forum

Magazeti ya leo December 8, 2024.
 
Attachments

  • IMG_6308.jpeg
    IMG_6308.jpeg
    1.5 MB · Views: 4
  • IMG_6315.jpeg
    IMG_6315.jpeg
    1.4 MB · Views: 3
Hapa ni kama koloni la Mwingereza miaka hiyo au bahari miaka hii, tumo na tumejaa hata kama hatuonekani ila tumo, siku kokoro likija kila mmoja anajitokeza kwenye upande wake. Nakusalimia tu mdau.
Hongera kwa mapumziko ya uhuru wa Tanganyika, uhuru ambao hata wenye utimamu na madaraka wanaogopa kulitaja jina Tanganyika na kusema ni uhuru wa Tanzania, Tanzania haijawahi kutawaliwa wala kuwa a protectorate wa Muingereza. Historia iwekwe kweli na ukweli huwa haupati kutu japo utauzika kwa nguvu ya kufuta maadhimisho na kumbukumbu.

Tutawakumbusha waliowazika wazee wetu, udongo walikuwa wanatupaje, mbona wanagoma kurudi na kutupatia historia kamili.!!! Udongo walichanganya na mawe!!!! sic. Au kuweka marumaru juu ya kaburi na zege ni kuwazuia wazee wasione tunavyowasema vibaya?!

Wiki la pili la Desemba hili, huu ni ukweli na kwa wenye umri kama wangu, mwezi huu wa Krismasi ni kama umekuja kwa kushtukiza, kuna wenye safari hawajajipanga, kuna wenye kununua nguo mpya, maduka ya mkononi na tiki tok yamejaa yanauza hadi mawani. Kifupi tuseme, Krismasi imekuja fast sana tofauti na miaka ile nawategemea walezi wangu wahakikishe nimevaa, nimekula, na nimekunywa. Maandalizi mema mdau.

Nisikuchoshe kwa aya nyingi kivile, unaruhusiwa kuangalia maandishi lakini kusoma inahitaji jitihada ya kuzungusha macho na akili, hulazimishwi, nchi huru hii na jukwaa hili ni huru pia.
 
🤣🤣
 
Back
Top Bottom