Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alipendekezwa mara 14 kupata tuzo za Grammy, na katika hizo alishinda tuzo 5. Huyu ni mwanamama aliyekuwa na sauti ya kukufikia masikioni na kuacha ujumbe iwe ni mapenzi au haki na usaw kwenze jamii. Hapa namuongelea mwanamama Roberta Flack., mwimbaji wa nyimbo za soul huko Marekani. Mwanamama huyu amefariki leo akiwa na miaka 88.
Kwa ambao tumebahatika kukutana na santuri za muziki (LP - vinyl) tutakumbuka mashairi ya The Closer I Get to you, yakiimbwa na kusindikizwa na kinanda. Au Tonight I celebrate my love (1983) na komesha yote japo sikuiishi miaka hiyo lakini nani asiyeujua wimbo wa Killimng Me Softly (1973) na mwaka mmoja baadaye ukashinda tuzo ya Grammy.
Wanamuziki wengi wakarudia kuuimba na hawa ndiyo ambao wengi wetu humu tumeusikia Killing Me Softly ukiimbwa na mwanamama mwingine Lauryn Hill wa kundi la Fugees (1996) mwaka ambao ndugu yenu namaliza STD, napiga mpira, kiraka najulikana hadi mitaa ya giza.
Nimeona niandike hili kwa sababu ni kitu napenda na hapa Makapuku ni sehemu nzuri kuwepo, tunasikiliza na hatujaji wewe ni nani. Tuwe na wiki njema, wiki la Ramadan.
View: https://www.youtube.com/watch?v=mrudT410TAI