Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu mfanyabiashara Hamis Said Luwongo, kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake wa ndoa, Naomi Marijani.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 26, 2025 na Jaji wa Mahakama hiyo, Hamidu Mwanga, baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi 14 na vielelezo 10 uliotolewa mahakamani hapo.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, jopo la mawakili wawili Serikali ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Yasinta Peter akisaidiana na Wakili Wa Serikali Mwandamizi, Ashura Mnzava, uliomba Mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wanaume wote wanaowafanyia ukatili wanawake wao kwa kigezo kuwa wapo kwenye ndoa.

"Kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ni cha ukatili na unatupa mashaka kwa wanawake waliopo katika ndoa na wanawake wanaingia katika ndoa, hivyo tunaomba Mahakama yako itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wanaume wanaotumia kigezo cha ndoa kufanya ukatili kwa wake zao" amedai wakili Mnzava

Katika kesi hiyo ya jinai namba 44/2023, Hamis, mkazi wa Gezaulole, wilayani Kigamboni, alikuwa anakabiliwa na shtaka la mauaji ya mkewe Naomi Orest Marijani kinyume cha kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, kama ilivyorejewa mwaka 2019.

Screenshot_20250226_151244_InstaPro2%20.jpg
 
Utajiri wa Elon Musk, ambaye ni tajiri namba moja duniani, umeendelea kushuka na safari hii zaidi dola bilioni 22.2 (Sh57 trilioni) zimepungua ndani ya siku moja.

Desemba 2024 utajiri wake ulifikia kiango cha juu cha Dola 480 bilioni, lakini sasa umepungua kwa takriban dola 116 bilioni hadi kufikia dola 364.3 bilioni Februari 2025, kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida la Wealth kupitia mtandao wake wa Instagram.

Kuporomoka huku kunahusishwa moja kwa moja na kushuka kwa thamani ya hisa za kampuni yake kuu ya Tesla, ambayo hisa zake zimepungua kwa asilimia 30 tangu Desemba 2024.

Hisa hizo zimeendelea kudorora kwa asilimia 21 tangu Januari 2025, hali ambayo imesababisha msukosuko mkubwa kwa wawekezaji na kupunguza thamani ya soko la bidhaa za kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa.

Tesla, ambayo inachangia zaidi ya nusu ya utajiri wa Musk, imekumbwa na changamoto kadhaa mwaka huu. Ripoti zinaonyesha kuwa mauzo ya Tesla yamepungua kwa kiwango kikubwa katika masoko muhimu, hasa barani Ulaya, ambako mauzo yalishuka kwa asilimia 50 Januari 2025.
Screenshot_20250226_151559_InstaPro2%20.jpg
 
Wakati wapiganaji wa M23 wakiendelea kujitanua Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Serikali ya Uingereza imeanza kutekeleza ahadi ya kuiwekea vikwazo Rwanda, huku ikiishurutisha kutowafadhili wapiganaji hao.

Rwanda imekuwa ikituhumiwa na Serikali ya Rais Felix Tshisekedi wa DRC na Umoja wa Mataifa (UN) kuwafadhili waasi hao, hata hivyo, Rais Paul Kagame kupitia mahojiano yake na CNN mwezi uliopita alikanusha kulifadhili kundi hilo.

Pia, Rais Kagame alipoulizwa juu ya uwepo wa askari wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) alidai hana taarifa ya uwepo wa askari wa Rwanda ndani ya ardhi ya DRC, huku akisema kinachofanyika ni operesheni zinazolenga kuwakamata waasi wa FDLR wanaotishia amani ya Rwanda.

Shirika la Habari la Associated Press (AP), limeripoti leo Jumatano Februari 26, 2025, kuwa Uingereza imeanza kuiadhibu Rwanda kutokana na uhusika wake katika uvamizi unaoendeshwa na M23 Mashariki mwa DRC na uhalifu dhidi ya haki za binadamu nchini humo.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kusitisha misaada ya moja kwa moja ya kifedha ambayo haihusishi misaada kwa wananchi maskini wa Rwanda.
Screenshot_20250226_151712_InstaPro2%20.jpg
 
Wanafunzi 30 pamoja na Mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari, Tumaini Jema, iliyopo Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro, wamenusurika kifo baada ya jengo moja la darasa walilokuwa wakisomea kuanguka kutokana na upepo mkali.

Wanafunzi hao pamoja na Mwalimu wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Same, ambapo hali zao zinaendelea kuimarika ambapo kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, akiambatana na Kamati ya Usalama ya wilaya, amefika katika Shule hiyo na kusimamisha shughuli zote za masomo kwa muda wa siku saba ili kupisha uchunguzi wa kina wa kubaini chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo.

Ameagiza Jeshi la Polisi, TAKUKURU, pamoja na Wataalamu wa ujenzi wa Halmashauri kufanya uchunguzi wa ajali hiyo na pia kukagua ubora wa majengo mengine Shuleni hapo “Kwa wiki hii yote, nawaombeni msitishe shughuli za masomo hapa Shuleni ili kupisha uchunguzi wa kina kuhusu ubora wa majengo haya”

Jeshi la Polisi, TAKUKURU, pamoja na Wataalamu wa ujenzi wa Halmashauri fanyeni uchunguzi ili tujiridhishe na usalama wa majengo haya, kama itabainika kuwa yapo chini ya kiwango, italazimika kubomolewa ili kulinda usalama wa Wanafunzi wetu,”

Mkuu wa Wilaya amewatembelea pia Wanafunzi na Mwalimu waliolazwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu, ambapo amewajulia hali na kuwapa pole kutokana na tukio hilo
Screenshot_20250226_151847_Instagram.jpg
 
Jeshi la Polisi nchini Uganda linamshikilia Mtanzania Naima Omary kufuatia kifo cha Mchezaji soka wa Kimataifa wa Nigeria Abubakar Lawal (29) aliyekuwa anaichezea Vipers SC ya Uganda.

Naima anashikiliwa kwa uchunguzi kwakuwa alikuwa Mtu wa mwisho kukutana na Lawal February 24,2025 kabla ya kufariki kwa utata kutokana na kuwa na taarifa mbili tofauti kuhusiana na kifo chake, taarifa ya kwanza ilisema amepata ajali ya bodaboda lakini taarifa ya Polisi imeeleza kuwa amedondoka kutoka kwenye barcony ghorofani alipokuwa amekwenda Voice Mall maeneo ya Bwebajja, barabara ya kuelekea Entebbe kuonana na Naima.

Lawal inaelezwa alifika Voice Mall akiwa na gari yake yenye namba za usajili UBQ 695G na kwenda kukutana na Naima aliyekuwa anaishi hapo toka February 20, 2025 chumba namba 416 ambapo inaelezwa Naima alimuacha Lawal chumbani akiandaa chai.

Naima yupo nchini Uganda kwa ufadhili maalum (Scholarship) kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake kucheza Basketball katika Chuo cha St Marry’s nchini Uganda.
Screenshot_20250226_151956_InstaPro2%20.jpg
 
Idadi ya vifo katika ajali ya gari la Serikali aina ya STM 6167 na basi la kampuni ya CRN T 599 DZQ vimeongezeka kufikia wanne.

Ajali hiyo ilitokea jana, February 25 katika eneo la Shamwengo Wilayani Mbeya ambapo Watu watatu walifariki papohapo wakati msafara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoani Mbeya ukitoka kumsindikiza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Rajabu.

Taarifa iliyotolewa kupitia ukurasa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala, Rodrick Mpogolo, imeeleza kufariki kwa aliyekuwa Dereva wake, Thadei Focus aliyekuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya leo February 26,2025,

Katika ajali hiyo waliofariki papohapo ni Mwandishi wa kujitegemea, Furaha Simchimba, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa CCM Wilaya ya Rungwe, Daniel Mselewa na Kondakra wa basi ambaye hajajulika jina lake kwa haraka, huku wengine saba wakijeruhiwa.

Miongoni mwa majeruhi ni Waandishi wa Habari Epimarcus Apolnali (Chanel Ten), Seleman Ndelage (Dream FM) na Denis George ambaye ni Mwandishi wa kujitegemea.
Screenshot_20250226_152057_InstaPro2%20.jpg
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu mfanyabiashara Hamis Said Luwongo, kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake wa ndoa, Naomi Marijani.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 26, 2025 na Jaji wa Mahakama hiyo, Hamidu Mwanga, baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi 14 na vielelezo 10 uliotolewa mahakamani hapo.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, jopo la mawakili wawili Serikali ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Yasinta Peter akisaidiana na Wakili Wa Serikali Mwandamizi, Ashura Mnzava, uliomba Mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wanaume wote wanaowafanyia ukatili wanawake wao kwa kigezo kuwa wapo kwenye ndoa.

"Kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ni cha ukatili na unatupa mashaka kwa wanawake waliopo katika ndoa na wanawake wanaingia katika ndoa, hivyo tunaomba Mahakama yako itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wanaume wanaotumia kigezo cha ndoa kufanya ukatili kwa wake zao" amedai wakili Mnzava

Katika kesi hiyo ya jinai namba 44/2023, Hamis, mkazi wa Gezaulole, wilayani Kigamboni, alikuwa anakabiliwa na shtaka la mauaji ya mkewe Naomi Orest Marijani kinyume cha kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, kama ilivyorejewa mwaka 2019.

View attachment 3250360
Hatimaye
 
Back
Top Bottom