PreGE2025 Makarani wa daftari la mpiga kura muwe na siri mnapayuka sana asee! Sasa miaka 18 ni kitu cha kutangazia kituo kizima?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Makarani wanaotuandikisha kwenye daftari la mpiga kura wawe na siri wanapouliza taarifa zetu binafsi kama vile mahali pa kuzaliwa, namba ya simu, mwaka wa kuzaliwa n.k

Karani anakuuliza mwaka wako wa kuzaliwa unamtajia halafu na yeye anaurudia kwa sauti kubwa ilhali watu wengine wapo kando hapo ambao hawastahili kujua hizo taarifa. Wanafanya hivyo hivyo kwenye namba za simu pia na taarifa nyingine.

Karani: Una miaka mingapi?
Mimi: 18
Karani: UMESEMA KUMI NA NANE EEEEEEH! YAANI NDIO MARA YA KWANZA KUPIGA KURA? AMA KWELI NIMEZEEKA!

Sasa hayo yote yanatoka wapi? Mpaka watu wanakosa hata ujasiri wa kujibu mana taarifa zake zinakuwa zimeanikwa kwa watu wote waliopo pale.

Wakati mwingine tume ya uchaguzi wawape muongozo na elimu kuhusu ulinzi wa Taarifa binafsi, inakeraaaa!
 
Makarani wanaotuandikisha kwenye daftari la mpiga kura wawe na siri wanapouliza taarifa zetu binafsi kama vile mahali pa kuzaliwa, namba ya simu, mwaka wa kuzaliwa n.k

Karani anakuuliza mwaka wako wa kuzaliwa unamtajia halafu na yeye anaurudia kwa sauti kubwa ilhali watu wengine wapo kando hapo ambao hawastahili kujua hizo taarifa. Wanafanya hivyo hivyo kwenye namba za simu pia na taarifa nyingine.

Watu wanakosa hata ujasiri wa kujibu mana taarifa zake zinakuwa zimeanikwa kwa watu wote waliopo pale.

Hahaha . Nenda BABINISIA HOSPITAL UKAJIONEE
DR. anakutajia ugonjwa wako akiwa Mt 10 toka ulipo tena huku anaondoka.
 
Ulifanya vyema mkuu, mana wanazianika sana taarifa zetu. mana wadau nao wapo attention kujua umezaliwa mwaka gani n.k
Wanakera sana..siku ya kwanza nimependa kupanga foleni nikawa naskia Yale mahojiano.
Umezaliwa wapi jamaa anajibu alafu karani anamuuliza tena kwa nguvu anhaa unasema umezaliwa....... Ikabidi niondoke kwanza
 
"unasema umezaliwa elfu mbili na ngapi...?" watu wengine wanaanza khee amezaliwa elfu mbili na tatu eti.

inakwaza sana asee
 
Wanakera sana..siku ya kwanza nimependa kupanga foleni nikawa naskia Yale mahojiano.
Umezaliwa wapi jamaa anajibu alafu karani anamuuliza tena kwa nguvu anhaa unasema umezaliwa....... Ikabidi niondoke kwanza
Hehehehehe
 
Makarani wanaotuandikisha kwenye daftari la mpiga kura wawe na siri wanapouliza taarifa zetu binafsi kama vile mahali pa kuzaliwa, namba ya simu, mwaka wa kuzaliwa n.k

Karani anakuuliza mwaka wako wa kuzaliwa unamtajia halafu na yeye anaurudia kwa sauti kubwa ilhali watu wengine wapo kando hapo ambao hawastahili kujua hizo taarifa. Wanafanya hivyo hivyo kwenye namba za simu pia na taarifa nyingine.

Watu wanakosa hata ujasiri wa kujibu mana taarifa zake zinakuwa zimeanikwa kwa watu wote waliopo pale.

Wakati mwingine tume ya uchaguzi wawape muongozo na elimu kuhusu ulinzi wa Taarifa binafsi, inakeraaaa!
Mi ndiomaana siendi kukataa huo upuuzi!
 
Back
Top Bottom