Makarani wa sensa ni akina nani?

Makarani wa sensa ni akina nani?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Zoezi la sensa kufikia tamati leo wakikusanya taarifa mbalimbali zinazotuhusu. Je, tunajua makarani wa sensa ni akina nani? Kama taarifa zako zikitumiwa vibaya na kuuzwa kwa watu huna pa kumshtaki zaidi ya kulalamika kwasababu mpaka sasa hivi bado hatuna sheria ya ulizi wa data.

Lakini siyo tu kwenye sensa, tunajaza taarifa zetu sehemu mbalimbali, na unakuta unaanza kutumiwa matangazo ya biashara au kupokea jumbe za ajabu, hii siyo bahati mbaya. Taarifa zako zimeuzwa!

Lakini pia kuna maeneno watu wata taarifa za watu za miaka kumi au kumi na tano nyuma, hizi taarifa ni tofauti kabisa na mtu alivyo sasa. Je, wanashikilia taarifa hizi kwa makusudi gani? Kuna utaratibu gani wa kuharibu data hizi ili zisitumike tena baada ya lengo kusudiwa kukamilika?

Je, taarifa zako ulizojaza kwenye madodoso ya sensa zikitumiwa ndivyo sivyo utasalimika mdau?
 
Makarani wa sensa walikuwa makada wa ccm
 
Back
Top Bottom