Makarani wa sensa tuwaamini bila uwepo wa sheria yoyote nchini inayolinda taarifa binafsi na faragha zetu?

Makarani wa sensa tuwaamini bila uwepo wa sheria yoyote nchini inayolinda taarifa binafsi na faragha zetu?

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Wakuu.

Awali ya yote nitoe pongezi kwa kila Raia wa nchi hii aliye bahatika kuhesabiwa. Wengine hatukupata bahati ya kufikiwa siku ya jana, natumani kwa muda muafaka, tutapata pia fursa hii ya kuingia kwenye rekodi ya takwimu muhimu za wakazi wa nchi hii.

Baada ya kutoa pongezi hili naomba sasa nielezee wasiwasi wangu.

Nimepitia maswali yote yanayoulizwa lakini nimepata wasiwasi sana. Inakuwaje zoezi la kuhesabu watu lihusishe uchukuaji wa taarifa zungine nyeti zinazohusu maisha ya mtu binafsi?

Nauliza hivi kutokana na nature ya nchi yetu. Tumepitia kwenye kadhia nyingi sana hapo nyuma hasa tunapotoa taarifa zetu nyeti kwa watu tunao waamini. Makarani hawa ni watu kama sisi, tunaishi nao mtaani. Usalama wa taarifa zetu upoje? Wakizitumia kwa mambo ya uhalifu tutawawajibisha vipi wakati nchi haina sheria inayolinda faragha na taarifa binafsi za watu?

Achilia mbali kuzitumia kwa mambo ya kihalifu, vipi kama wataamua kuziuza kwa mtu yoyote au hata kuzitumia kwa mambo ambayo serikali haikupanga?

Kwanini Serikali imeamua kufanya sensa pasipo kutunga kwanza sheria hii? Ikitokea taarifa zangu zimetumika vibaya nitamuwajibisha nani? Nitalindwa vipi?

Nipo tayari kuhesabaiwa lakini nina wasiwasi mkubwa wa nini kitaanza kutokea baada ya kukamilika kwa zoezi hili.
 
Ondoa hofu ya negativity, taarifa zako wakizitaka awahitaji mtu wa sensa awapatie.

Bodaboda tu Wana taarifa kibao za watu
 
Ondoa hofu ya negativity, taarifa zako wakizitaka awahitaji mtu wa sensa kuzipata.
Ni kweli mkuu. Mimi siilaumu serikali, ninauliza hawa watu wanaofanya zoezi hili ambao ndiyo tunawapa taarifa zetu. Tuwaamini vipi, maana ni watu wa kawaida tu kama sisi na lolote linaweza kutokea.
 
Ni kweli mkuu. Mimi siilaumu serikali, ninauliza hawa watu wanaofanya zoezi hili ambao ndiyo tunawapa taarifa zetu. Tuwaamini vipi, maana ni watu wa kawaida tu kama sisi na lolote linaweza kutokea.
Yote wamefunzwa ndiyo maana ya seminar ikiwemo na shaka hio. Juu ya usiri na utunzaji wa taarifa maadili yamezingatiwa.
 
Yote wamefunzwa ndiyo maana ya seminar ikiwemo na shaka hio. Juu ya usiri na utunzaji wa taarifa maadili yamezingatiwa.
Ni kweli boss, umeeleza vyema.

Lakini kumbuka mifano rahisi tu, mara ngapi wakurugenzi wa uchaguzi na wasimamizi wa vituo hufanya mambo ya ajabu sana vituoni na hakuna cha kuwafanya?

Nafikri huwezi kulinda maisha ya watu kwa semina na kuapa ukumbini bila uwepo wa sheria za kuwajibishana.
 
Sheria ipo Sura na 351 sheria ya takwimu pia makarani wote wamekula kiapo cha kutunza siri
 
Back
Top Bottom