Makaratasi ya uchochezi dhidi ya Serikali

Makaratasi ya uchochezi dhidi ya Serikali

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MAKARATASI YA "UCHOCHEZI" DHIDI YA SERIKALI SEHEMU YA KWANZA

Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes nilipata taarifa za kachero Amiri Kweyamba kutoka kwa kinywa cha Ally Sykes.

Ikatokea nikaja kufahamiana na mtoto wa Amiri Kweyamba.

Huyu Amiri Kweyamba alikuwa kijana wa Kihaya na alikuwa Special Branch.

Mwaka wa 1953 kuelekea kuundwa kwa TANU 1954 palizuka makaratasi ya "uchochezi," kama Waingereza walivyokuwa wakiyaita yaliyokuwa yakimwagwa katika mitaa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tabora, Kigoma hadi Mwanza yaliyokuwa yakichapwa na "cyclostyle machine," yakiwahamasisha wananchi kujiunga na TAA kwa kuwa kuna jambo kubwa linakaribia kufanyika.

Makaratasi haya yalitaabisha sana serikali kwa kuwa haikujua hilo jambo kubwa kilikuwa ni kitu gani wala haikujua wapi makaratasi yale yanakotokea.

Haya makaratasi yapo hadi leo katika Nyaraka za Sykes.

Kenya Wakikuyu chini ya Mau Mau walikuwa tayari wamenyanyua silaha dhidi ya Waingereza na wako msituni wanapigana kuikomboa nchi yao.

Serikali ilikuwa na taarifa kuwa Abdul Sykes mwaka wa 1950 alikutana na Kenyatta na kundi lake la akina Achieng Oneko, Bildad Kaggia, Kung'u Karumba, Fred Kubai, na Paul Ngei lakini haikujua nini kilizungumzwa.

Waingereza walipoanza "Operation Anvil,"Nairobi kuwasaka Mau Mau operation ile ilifika hadi Tanganyika na wakakamatwa Wakikuyu wengi Mwanza na Dar es Salaam.

Hawa Wakikuyu wengi wao walikuja Tanganyika kutarazak.

Mmoja wa hawa waliokamatwa alikuwa Dome Okochi Budohi aliyepatakuwa kiongozi katika TAA mwaka wa 1953 na akawa mwanachama wa TANU 1954 mwenye kadi no. 6.

Budohi aikamatwa pamoja na Wakenya wengine wakawekwa kwenye kambi, Handeni wakiwa wamefungwa minyororo miguuni kabla ya kusafirishwa kwenda Kenya wakiwa katika mabehewa ya ng'ombe.

Hawa wote walifungwa kisiwani Lamu.

Mkutano wa siri kati ya Abdul na Kenyatta Nairobi uliwastua Waingereza kwani Abdul alikuwa askari aliyepigana katika Burma Infantry 6th Battalion pamoja na General China aliyekuwa msituni pamoja na Dedan Kimathi.

Walitia shaka huenda Tanganyika na wao walikuwa wanajitayarisha kunyanyua silaha.

Serikali ikataka kujua haya makaratasi wapi yanatoka.

Mwandishi wa makaratasi haya na mchapaji wake alikuwa Ally Sykes, askari wa Burma na mlenga shabaha bingwa Vita Vya Pili Vya Dunia.

Special Branch wakapata fununu kuwa huyo ndiye mtu wao na mashine iko nyumbani kwake Mtaa wa Kipata.

Mtego ukawekwa wa kumkamata na hii operation akaingoza Amiri Kweyamba.

Tutie nanga hapa tutaendelea na huu mkasa ni kisa kirefu sana hawa Waafrika wawili visasi vyao havitaishia wote wakiwa wanatawaliwa.

Vitaendelea hadi Tanganyika ikiwa huru.

Ally Sykes akimtema mate Amir Kweyamba akimuona kibaraka wa Waingereza na Amiri Kweyamba akimuona Ally Sykes anamuonea bure kwani yeye alikuwa askari akifuata amri na kutimiza wajibu wake.

DSC00737~2.JPG
 
Story nzuri ila umeweka fupi sana mkuu
Paplo...
Ukirudia kusoma utakuta mahali nimesema itaendelea.

Ally Sykes huwezi kummaliza.
Ana mambo mengi sana.

Vuta subira nitakuletea hali ilikuwaje pale mlango wake ulipogongwa na yeye yuko mitamboni anachapa mikaratasi yake ya hatari na mkewe Bi. Zainab alipokwenda kuangalia nani anabisha hodi akamwambia kuwa Amiri Kweyamba yuko mlangoni na askari.
 
Paplo...
Ukirudia kusoma utakuta mahali nimesema, "tutie nanga tutaendelea na huu mkasa..."

Ally Sykes huwezi kummaliza.
Ana mambo mengi sana.

Vuta subira nitakuletea hali ilikuwaje pale mlango wake ulipogongwa na yeye yuko mitamboni anachapa mikaratasi yake ya hatari na mkewe Bi. Zainab alipokwenda kuangalia nani anabisha hodi akamwambia kuwa Amiri Kweyamba yuko mlangoni na askari.
 
Back
Top Bottom