Makato Equity bank ni wizi wa wazi

Makato Equity bank ni wizi wa wazi

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Kununua bidhaa online au Kutoa pesa Kwa Kadi ya ATM Equity utajuta kuwajua nilitoa pesa kwa visa Sydney, Australia naona makato yamekuja 110,000 TSH.

NB: Eeh ndugu usijaribu kutumia Kadi pendwa toka Equity bank
 
Hiyo benki wendawazimu wanaenda kufanya kama tulichofanyiwa na NBC.

Wanakata 15% ya transaction ukifanya muamala wa fedha ya kigeni. Mimi nilikatwa hela nililipia kwa RMB nikakatwa na rate yao ya kununua sarafu, kisha kule nilikoenda kulipa Mchina akakosea address nikafanyiwa refund. Ebwana Equity wamekata 15% ya kwenda na 15% ya kurudi. Hela ya refund yenyewe mpaka uwabembeleze ndio waweke kwenye akaunti.

Nikafanya muamala mwingine kulipia in USD, wakaniuzia $ kisha wakakata 15% yao. Hizi zote wanakata kama 30 days baada ya kukamilisha muamala. Nilishtukia natumiwa SMS nimekatwa hela mara mbili. Sijaweka hela tena naogopa wasikate makato ya zamani.

NBC walifanya huu ujinga wakalimbikiza makato unakuja kushtukia SMS kwa mkupuo unajua umekuwa hacked, wanakata zao mamilioni. Aaah kuna wadau walikatwa milioni 50 kufumba na kufumbua. Akaunti yao niliitelekeza nayo ina deni la laki kadhaa.

Suluhisho kama unafanya mara kwa mara ni kutumia akaunti ya USD ila nadhani ununue kwa USD tu, sio sarafu nyingine.

Benki za kibongo ni maajabu wanazidiwa huduma na Vodacom, yani ustadh anajua Biblia kuliko katekista.
 
Kununua bidhaa online au Kutoa pesa Kwa Kadi ya ATM Equity utajuta kuwajua nilitoa pesa kwa visa Sydney, Australia naona makato yamekuja 110,000 TSH.

NB: Eeh ndugu usijaribu kutumia Kadi pendwa toka Equity bank
Umenitisha nilitaka niamie huko maana watu wamekuwa wakiisifia.
 
Umenitisha nilitaka niamie huko maana watu wamekuwa wakiisifia.
Zingatia amesema kufanya malipo ya fedha za kigeni, sio TZS kwa TZS. Kuhusu kutoa kwa ATM au kwa wakala sijawahi zingatia kama makato ni makubwa sana kupita wengine.

Ila kwa mambo mengine Equity hawana maudhi kama benki zetu.
 
Asante kwa taarifa
 
Kwani makato benki nyingine yakoje ukiwa nje ya nchi, usikute kiwango kipo juu kama hiyo
 
Back
Top Bottom