Hiyo benki wendawazimu wanaenda kufanya kama tulichofanyiwa na NBC.
Wanakata 15% ya transaction ukifanya muamala wa fedha ya kigeni. Mimi nilikatwa hela nililipia kwa RMB nikakatwa na rate yao ya kununua sarafu, kisha kule nilikoenda kulipa Mchina akakosea address nikafanyiwa refund. Ebwana Equity wamekata 15% ya kwenda na 15% ya kurudi. Hela ya refund yenyewe mpaka uwabembeleze ndio waweke kwenye akaunti.
Nikafanya muamala mwingine kulipia in USD, wakaniuzia $ kisha wakakata 15% yao. Hizi zote wanakata kama 30 days baada ya kukamilisha muamala. Nilishtukia natumiwa SMS nimekatwa hela mara mbili. Sijaweka hela tena naogopa wasikate makato ya zamani.
NBC walifanya huu ujinga wakalimbikiza makato unakuja kushtukia SMS kwa mkupuo unajua umekuwa hacked, wanakata zao mamilioni. Aaah kuna wadau walikatwa milioni 50 kufumba na kufumbua. Akaunti yao niliitelekeza nayo ina deni la laki kadhaa.
Suluhisho kama unafanya mara kwa mara ni kutumia akaunti ya USD ila nadhani ununue kwa USD tu, sio sarafu nyingine.
Benki za kibongo ni maajabu wanazidiwa huduma na Vodacom, yani ustadh anajua Biblia kuliko katekista.