Benki ni biashara na sio huduma, wanapata faida yao kupitia makato mbali mbali wanayokata kwa watumiaji wa huduma husika.
Unapopeleka benki kutunza pesa zako lazima uelewe kwamba kuna gharama ya wao kama benki watatumia ili kutunza pesa zako vizuri.
Kuna aina nyingi za akaunti, lakini mtu hufungua akaunti inayokidhi mahitaji yake, kila akaunti ina makato yake kutokana na gharama zake za uendeshaji.
Aina za akaunti
1. Savings account au akaunti ya akiba
Hii ni akaunti maarufu na inayotumiwa na watu wengi, inamruhusu mtumiaji kutumia akaunti yake kuweka pesa muda wowote na kutoa muda wowote unaweza kutoa kwenye (ATM, wakala, mobile banking, internet banking n.k). Benki inatumia gharama kubwa kutunza akaunti za namna hii hivyo gharama zake za makato ni kubwa kwa mfano itakuwa na gharama za huduma mwezi (monthly service charges), kama umepewa kadi za Mastercard au Visa pia utakatwa service charge yake na gharama nyingine kila utumiapo kwa mfano ukitoa pesa ATM au WAKALA au MOBILE BANKING, ukiangalia salio, ukiomba bank satement.
2. Akaunti za muda maalumu (Fixed deposit account)
Hizi ni akaunti ambazo zinamuwezesha mtumiaji kuweka pesa zake kwa muda maalumu bila kuzitoa. Kwa mfano unaweka Tsh 500,000 kwa miezi 6. Au unaweza kila mwezi Tsh 100,000 kwa miezi 12 au 36. Akaunti hizi hazina makato kabisa na zinatoa faida au riba.
Kimsingi savings ni transactional account kwa sababu ni akaunti inayoruhusu kupokea pesa muda wowote na pia ni rahisi kufanya miamala ila inahitaji kuwa smart ili kukwepa gharama zisizo za lazima
Kwa hiyo binafsi huwa naona usifngue akaunti bila sababu ya msingi utawafaidisha watu wengine, angalia mahitaji yako halafu fungua akaunti yenye faida nyingi kwako kuliko gharama.
Makato ya serikali
Serikali iliamua kuanzisha kodi ya ongezeko la thamani kwenye kila charge ya benki. Lakini pia kuna tozo maalumu kama zinavyosomeka kwenye muongozo wa makato kwa kila muamala unaotoa au maarufu kama TOZO.
I stand to be corrected lakini savings account kupitia huduma mbadala za mobile banking kuna baadhi ya huduma ni bure kama kununua salio, kulipa malipo ya serikali, kulipa malipo mbalimbali lakini pia kupitia cards (visa na Mastercard) unaweza kulipa bure kwenye supermarkets na maduka mbalimbali.