Makato ya mamala yapo poa, yanawiana na Uchumi wa kati

Makato ya mamala yapo poa, yanawiana na Uchumi wa kati

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAKATO YA MIAMALA YAPO POA! YANALANDANA NA UCHUMI WETU WA KATI

Kwa Mkono wa, Robert Heriel

Nimefurahishwa na mambo yaendavyo, mwaka Jana tulipigiwa mbiu kuwa tumeingia uchumi wa Kati. Watu walifurahia hasa wenye mrengo wa kuishabikia CCM na Wanachama wa CCM pamoja na Watanzania WA kipato cha chini na wenye elimu duni.

Wengi walishangilia na kumsifia Hayatti Magufuli aliyekuwa Rais wakati huo, ambaye naye kujigamba hakukuisha mdomoni mwake kujitukuza namna alivyoupaisha uchumi kufikia uchumi wa Kati.

Mimi nilishajua hatari ya kukuambia taifa lipo uchumi wa Kati ilhali wananchi wake wapo uchumi wa mwisho kabisa huko chini.

Katika uchunguzi wangu WA kimkakati, Vijana wengi nilipowauliza kuhusu uchumi wao, nilibaki kuwaonea huruma. Wengi ni dhoofu, choka mbaya, Apeche Alolo, kuingiza 5000 Kwa siku ni kitendawili. Lakini wenyewe wanakuambia wapo uchumi wa Kati.

Sasa nikasema nisibishane nao, maana wengi wape, Ila nikasema hawa nawasubiri kwenye tuta(Bump) kwani lazima wapunguze mwendo, na Kama watakaidi basi chamoto watakiona.

Sasa tumeshalifikia tuta, waliositi za mwisho kwenye Gari chamoto wanakiona, mrusho wake wakwenda,
Na Jambo la uhakika ni kuwa barabara tunayopitia kuna Matuta mengi(bumps) za kutosha.

Waliokaa siti za mbele mpaka siti za Kati wao hawawezi ona athari za mwendo huu, Ila Wale Watanzania waliositi za nyuma chamoto watakipata.

Tupo uchumi wa Kati, makato ya kwenda,

SERIKALI ongezeni kasi, ongezeni makato kila Nyanja yanayoendana na Uchumi wa Kati.
Tunajiweza, tunamudu, tunafurukuta.

Uchumi wa Kati, makato ya Kati.

Hongera serikali,
Hongera wananchi, nimeamini tupo uchumi wa Kati.


Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dumila, Morogoro
 
Unatafuta kwa nguvu matusi asubuhi asubuhi🤣🤣🤣
... alichoeleza ndio ukweli halisi; uchumi wa kati maana yake nchi na wananchi wake wanajiweza kiuchumi; kilio cha nini tena? Ile furaha, shangwe, na nderemo za kuingia uchumi wa kati hamkuzijua? Watu walipe kodi tena walipishwe kweli kweli nchi tajiri hii.
 
Wengine kwanza wanaona tumeonewa kuambiwa kuwa eti tupo uchumi wa kati. Tangu lini tajiri, nchi tajiri ikawa uchumi wa kati? Nchi tajiri inatakiwa kuwa uchumi wa juu.

Mtu ana matenga yake matatu ya nyanya, au bando zima la nguo za mitumba za ndani za akina mama, utamwitaje wa uchumi wa kati, wakati ni tajiri?

Hao unaosema wapo nyuma ya basi wanarushwa, yawezekana hujawaangalia vizuri, hao wameweka earphones zao masikioni, wanashangilia kwa kurukaruka kwa kuwa wao ni matajiri.

Kule mbele, waliotulia kimya ni wakombozi wa hawa wanaowashangilia. Wametulia ili kusikikiza vizuri nyimbo za sifa wanazoimbiwa.

Hujamsikia huyo anayeimba, oye Mwigulu, endelea hivyo hivyo, mpaka kila mtu awe na ndege yake?
 
Wengine kwanza wanaona tumeonewa kuambiwa kuwa eti tupo uchumi wa kati. Tangu lini tajiri, nchi tajiri ikawa uchumi wa kati? Nchi tajiri inatakiwa kuwa uchumi wa juu.

Mtu ana matenga yake matatu ya nyanya, au bando zima la nguo za mitumba za ndani za akina mama, utamwitaje wa uchumi wa kati, wakati ni tajiri?

Hao unaosema wapo nyuma ya basi wanarushwa, yawezekana hujawaangalia vizuri, hao wameweka earphones zao masikioni, wanashangilia kwa kurukaruka kwa kuwa wao ni matajiri. Kule mbele, waliotulia kimya ni wakombozi wa hawa wanaowashangilia. Wametulia ili kusikikiza vizuri nyimbo za sifa wanazoimbiwa.
Hujamsikia huyo anayeimba, oye Mwigulu, endelea hivyo hivyo, mpaka kila mtu awe na ndege yake?

Mkuu amka, kumekucha, nchi imepiga hatua kubwa.
Tunasonga mbele, tupo imara.
Wananchi wanajiweza.

Uchumi jumuishi huu.
Makato yasiyoumiza
 
Nashangaa maccm yote yanalamamika wakati wamepitishwa na wabunge wao
 
Back
Top Bottom