Makazi bora ni yapi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Wengi huwa tunajenga makazi yetu ya kuishi kutokana na ukubwa wa vipato vyetu; wapo watakao jenga kwenye eneo la 10x10m, 20x 30m, 40 x 50m n.k

Pia, wapo watakaojenga kwenye eneo la ekari 5, 10, 20 n.k

Ila kwa mtazamo wangu; mimi naona makazi bora ni kujenga kwenye eneo lenye angalau ekari 10 na kuendelea, huku ukiwa unasikilimiza milio ya ndege mbalimbali.

Je, kwa mtazamo wako; makazi bora ni yapi?

 
uko sahihi ila naona ekari moja inatosha, ekari 10 hapana ni hatari kwa afya ya mkazi
 
Yes heka 10 zinatosha kwa kasri kila kitu kiwemo kwa uchache yaani hata mwezi waweza isha hujatoka nje ya himaya yako

Wasanii wakubwa America ndo mara nyingi wana hizo heka 50, 40, 30 hata makazi ya Obama niliyaona mtandaoni ni makazi haswa!
Reginald Mengi nae alikuwa makazi bora huko kwao
 
Wazee wa 250Sqm tupo kundi lipi la makazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…