Makelele ya makanisa kwenye makazi siyo sawa kidini, wala kisheria; yadhibitiwe kama makelele mengine


Si ndio ile huwa mnasomea wezi wa balbu[emoji23][emoji23]

Hiyo ni albadiri.
 
Kiukweli naomba kujua taratibu za kufata kuhusu hili, kuna kanisa limepanga kwenye kiwanja jirani hapa ni La mabati ila jamani hizi kelele ni kubwa sana akifungulia anaweka flash sauti kubwa na hilo base hadi vioo vinatikisika akiambiwa anapunguza nusu saa anaweka tena, ni mjeuri na waumini hawazidi 10. Yaani huwezi ongea na simu wala kusikilizana ndani hata tv hamuwezi washa, siku ya mkesha ijumaa balaa, hadi wazime saa 6 usiku, jumapili 12 asubuhi hadi saa 7 mchana bado weekly days. Watoto hawalali yaani huwezi kupumzika. Ni mateso kiukweli. Nilikuwa ninauguza mgonjwa ana high blood pressure ikabidi tumuhamishe. Naombeni taratibu nianzie wapi hii hali haivumiliki.
 
Vipi kuhusu misikiti na kelele za vipaza sauti na mawaidha kila siku
 
Kwahiyo Mungu wa kiarabu akapambana na Mungu wa kiyahudi?????? Allah vs Yesu????? Kilitokea nini ebu tueleze ukweli sio ushabiki wa kidini???
 
Uhuru wa kuabudu huo
 
Mkuu makelele ni makelele tu..Yawe ya mda mrefu au mfupi...Acha kuegemea upande mmoja huo ni unafiki.
 
Kwahiyo adhana haina kelele sababu ni kiarabu eeeh ila wakrsto wakisali ni kelele kisa kiswahili???
 
Mbona misikiti mda wowote wanaanzisha mawaidha yao ila ushangai hawa watu wanaenda job mda gani??? Hakuna ubaguzi mbaya kama wa kidini
 
Kelele za makanisa aloo ni kero kwanini wasitumie sauti ya kawaida lazima kila mtu asikie???ujue kuna upigaji kelele usio kera ila kelele nyingine ni kutiana majaribuni tu!
Vipi kelele za misikiti na vipaza sauti vikubwaa ???
 
Swali zuri labda watakujibu....Zanzbar kelele za vipaza sauti vya misikiti ni vipi???? Au mwananyamala kelele za misikiti ni vipi???
Wakiswali kama wanavyoswali kiada, yaani dakika hizo chache za Azana, kujitayarisha, na kusali kwa muda usiozidi dakika ishirini, hawajavunja sheria. Kiafya nako siyo tatizo sana ndiyo maana swala hizo na misikiti imeendelea kuwepo kwenye makazi sehemu nyingi duniani. Ila, inasemekana, kuna sehemu za nchi wanazidisha. Ikiwa hivyo waripotiwe Halmashauri wadhibitiwe.
 
Wewe una lako na wakristo,,,ina maana hayo mawaidha kupitia vipaza sauti sio kelele kwa dakika ishirini??????? Au wewe unajua msikitini ni adhana tu?????? Nenda mwananyamala au tandika au tandale uone kero za misikiti kwenye makazi ya watu??????? Lakini kama una chuki na dhiaka dhidi ya waafidhina wa kikrsto(Walokole) mimi nakuelewa maana Christian phobia haina tofauti na Islam phobia...
 
Kelele Ni kelele tu hakuna kelele Bora kuliko nyingine Kama Ni kukataa tukatae zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…