Makelele ya muziki katika makazi ya watu bomu linalosubiri kulipuka

Makelele ya muziki katika makazi ya watu bomu linalosubiri kulipuka

Luigi Alfred

Member
Joined
Mar 17, 2016
Posts
78
Reaction score
51
Huu ujumbe uifikie taasisi yenye dhamana ya kuhifadhi mazingira. Sio siri kwa Mtanzania wa kawaida anakerwa na baadhi ya RAIA hasa maeneo ya vijijini kufungulia hoofer za kichina sauti za juu hadi kero. Maendeleo yana gharama zake nyingine ni hasi.

Serikali imesambaza umeme vijijini ili watu waanzishe miradi midogomidogo lakini Bahati mbaya baadhi wamewekeza kwenye vilabu vya pombe za kienyeji na kupiga miziki usiku kucha.

Watu hatulali usingizi wa amani siku hizi na akili haipumzishwi wapi tunakwenda?
 
Nyie mnaojifanya kufuata protocols everywhere ndo mmeharbu nchi hii
 
Mzee uzuri sheria ya mazingira hairuhusu fika polisi mapemq tu ukatoe malalamiko yako. Wenye iko kitengo wapo ofisin tu wanakula pesa hawatoi elimu kwa Raia. Niliwahi kwenda sehemu nikakaa siku mbili kwa jke kuna hawa madogo wa kuingiza miziki anapiga mziki hadi hqiuna raha kulala nikawaulize wenyeji mwenyekiti wa mtaa anaofisi wapi nikaenda mshitaki akapigwa marufuku
 
Sheria ya mazingira tanzania haifuatwi kabisa, kuna ujinga mwingi sana. Kwa mfano kelele sehemu za ibada na vikabu vya pombe. Mimi nampenda Mungu, lakini Mungu si wa makelele ni Mungu wa utulivu sana.
 
Mzee uzuri sheria ya mazingira hairuhusu fika polisi mapemq tu ukatoe malalamiko yako. Wenye iko kitengo wapo ofisin tu wanakula pesa hawatoi elimu kwa Raia. Niliwahi kwenda sehemu nikakaa siku mbili kwa jke kuna hawa madogo wa kuingiza miziki anapiga mziki hadi hqiuna raha kulala nikawaulize wenyeji mwenyekiti wa mtaa anaofisi wapi nikaenda mshitaki akapigwa marufuku
*MUHIMU SANA KWA WANANCHI WOTE WA KATA KASHARU.

KUMEZUKA TABIA NAMIENENDO YA KUPIGA MIZIKI MCHANA KUTWA NA USIKU KUCHA KILA SIKU VIJIJINI MWETU. TUISOME HII TUIELEWE NA KUCHUKUA HATUA.

Nchini Tanzania kuna sheria inayozuia mtu au watu kusababisha kelele za usumbufu kwa wengine*.

Kisheria, jambo hili linashughulikiwa kupitia Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Sura ya 16 na pia Sheria ya Usafi wa Mazingira (Environmental Management Act, Cap 191) kulingana na aina ya kelele na mazingira husika.

1. Kanuni ya Adhabu– Kelele za Usumbufu
Kifungu kinachohusika ni Kifungu cha 176 na 186 cha Penal Code, Sura ya 16:

Kifungu cha 176(1)(b) – kinakataza kufanya kelele au kelele za kupita kiasi kwa nia ya kumsumbua au kumhatarisha mtu mwingine katika sehemu ya umma.

Kifungu cha 186 – kinahusu biashara au shughuli yoyote inayosababisha kelele kubwa au harufu mbaya katika mazingira kiasi cha kumsumbua mtu katika matumizi ya haki zake za kawaida.

Adhabu: Mtu akipatikana na hatia, anaweza kutozwa faini au kufungwa (mara nyingi kifungo kinaweza kuwa hadi miezi sita, kulingana na ukubwa wa kosa na maamuzi ya mahakama).

2. Sheria ya Usimamizi wa Mazingira
Kifungu cha 183(1) cha Environmental Management Act, Cap 191, kinapiga marufuku:

“Kutengeneza au kuruhusu kelele zinazozidi viwango vilivyowekwa na mamlaka husika.”

Adhabu: Kwa mujibu wa kifungu cha 183(2), adhabu inaweza kuwa faini isiyozidi shilingi milioni moja (TSh 1,000,000) au kifungo kisichozidi miezi 12, au vyote viwili.

✅ Kwa kifupi: Sheria hizi zipo ili kulinda haki ya kila mtu kupata utulivu, na yeyote anayefanya kelele za usumbufu anaweza kutozwa faini au kufungwa.
 
Back
Top Bottom