Makinda atoa msimamo juu ya pendekezo la serikali tatu

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuna hatari ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwa Tanzania Bara kutofanyika ikiwa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa na Tume ya Katiba yatapita kama yalivyo.
Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini (CCM) alisema ikiwa mapendekezo hayo yatatipishwa na wananchi kama yalivyo, Tanzania Bara haitaweza kuingia katika uchaguzi kwa vile haitakuwa na katiba.
Aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Jumuiya wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Njombe uliofanyika katika Kijiji cha Makumbusho.
Wakati Makinda akizungumza hayo, tayari Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeshatangaza kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya mabaraza kuanzia Julai 12 hadi Agosti 2, mwaka huu.
“Hiyo rasimu tuisome vizuri, nataka tu msome vizuri, je, serikali tatu ‘just imagine’ (fikiria) kuwe na serikali ya tatu ambayo haina ardhi, haina watu, ina watawala tu…. mkasome vizuri, mkasome vizuri,” alisema.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Spika Makinda alionesha wasiwasi wa taifa kuwa na serikali tatu. “Nchi hii itakuwa na marais watatu, maspika watatu, mabunge matatu, majeshi matatu, benki kuu tatu… sitaki kuwa biased, ndiyo maana nataka wananchi mkasome vizuri,” alisema.
“Najua Profesa Shivji ameshasema maoni yake lakini inabidi tusome hata mara 10, kwa sababu ni kitu muhimu,” alisema Spika Makinda.
Alisema watu wengi hawajaielewa hivyo kuna haja ya rasimu hiyo kupitiwa ili iweze kueleweka, vinginevyo ikipitishwa kama ilivyo uchaguzi mwaka 2015 kwa Tanzania Bara hautafanyika, kwa sababu katiba haitakuwapo.
Alisema kutokana na mapendekezo hayo, itakuwa vigumu kwa Tanzania Bara kushiriki uchaguzi kwa sababu nyingi za msingi. Alizitaja kuwa ni pamoja na ugumu wa kuwapata wabunge wa bunge la serikali ya tatu kwa vile watakuwa wanachaguliwa katika mikoa.
“Kwa jinsi mikoa ilivyo mikubwa tutaanzaje kupiga kampeni kuchagua wabunge wawili?,” alihoji.
Akijibu ombi la Wana Njombe hao kuomba Sekondari ya Njombe ifundishe kidato cha kwanza hadi cha nne kama ilivyokuwa awali badala ya kidato cha tano na sita kama ilivyo sasa, Spika Makinda alisema jambo hilo si rahisi, kwa sababu baada ya kuanzishwa kwa shule nyingi za kata taifa linakabiliwa na uhaba wa sekondari zenye vidato vya tano na sita.
“Lakini naomba muelewe mazingira ya Njombe Sekondari kuwa High School, baada ya kampeni ya serikali kuanzisha shule za kata hasa kule kwetu ambako ziko zaidi ya 27,” alisema Spika Makinda.
Alisema ikiwa shule hiyo itaongezewa vidato, itapokea wanafunzi wengi kutoka mikoani na ndiyo maana waliona ibaki kama ilivyo.
Alisema anadhani hivi sasa serikali inaangalia sera mpya ya kuzihudumia shule zinazoanzishwa kwa lengo la kufundisha masomo ya kidato cha tano na cha sita (high school), vinginevyo kutakuwa na ‘O’ level nyingi na kidato cha tano na cha sita chache, hali ambayo haitasaidia.
Awali akisoma risala ya wana umoja huo, Katibu wake, John Mwakyusa, aliahidi kwamba watashiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba mpya hadi mwisho.
Chanzo:Tanzania Daima Jumanne 16-07-2013.
 
makinda mara nyingi hawezi kuongea bila kufuata upepo unavyovuma inshort she is too dependent and she has no common stands.
 
Chadema tumbo moto.

Kwa nini mkuu! Kwani chadema inahusikaje sasa hapo. Katiba isiwe mali ya chama fulani au mtu fulani.kila mtanzania na taasisi watoe maoni na wasubiri uamuzi wa wengi.hayo ni maoni ya mtu mmoja...makinda. basi km anaona huo ni mzigo aseme kama anahitaji serikali moja.maana ndo haitakuwa mzigo.
 
Chadema tumbo moto.

How? Hayo ni maoni ya wananchi. Hivyo cdm hawana haja ya kuwa na wasiwasi maana ni maoni ya wengi wakiwemo pia wa na CCM wakongwe kama Jaji Warioba, Salim A. Salim ambao pia ni wajumbe wa tume. Tume ya Warioba imemaliza kila kitu.
 
Atulie tu huyo bibi, katiba ni ya watanzania wala si ya CCM au Makinda!
 
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuna hatari ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwa Tanzania Bara kutofanyika ikiwa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa na Tume ya Katiba yatapita kama yalivyo.
Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini (CCM) alisema ikiwa mapendekezo hayo yatatipishwa na wananchi kama yalivyo, Tanzania Bara haitaweza kuingia katika uchaguzi kwa vile haitakuwa na katiba.
Aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Jumuiya wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Njombe uliofanyika katika Kijiji cha Makumbusho.
Wakati Makinda akizungumza hayo, tayari Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeshatangaza kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya mabaraza kuanzia Julai 12 hadi Agosti 2, mwaka huu.
"Hiyo rasimu tuisome vizuri, nataka tu msome vizuri, je, serikali tatu ‘just imagine' (fikiria) kuwe na serikali ya tatu ambayo haina ardhi, haina watu, ina watawala tu…. mkasome vizuri, mkasome vizuri," alisema.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Spika Makinda alionesha wasiwasi wa taifa kuwa na serikali tatu. "Nchi hii itakuwa na marais watatu, maspika watatu, mabunge matatu, majeshi matatu, benki kuu tatu… sitaki kuwa biased, ndiyo maana nataka wananchi mkasome vizuri," alisema.
"Najua Profesa Shivji ameshasema maoni yake lakini inabidi tusome hata mara 10, kwa sababu ni kitu muhimu," alisema Spika Makinda.
Alisema watu wengi hawajaielewa hivyo kuna haja ya rasimu hiyo kupitiwa ili iweze kueleweka, vinginevyo ikipitishwa kama ilivyo uchaguzi mwaka 2015 kwa Tanzania Bara hautafanyika, kwa sababu katiba haitakuwapo.
Alisema kutokana na mapendekezo hayo, itakuwa vigumu kwa Tanzania Bara kushiriki uchaguzi kwa sababu nyingi za msingi. Alizitaja kuwa ni pamoja na ugumu wa kuwapata wabunge wa bunge la serikali ya tatu kwa vile watakuwa wanachaguliwa katika mikoa.
"Kwa jinsi mikoa ilivyo mikubwa tutaanzaje kupiga kampeni kuchagua wabunge wawili?," alihoji.
Akijibu ombi la Wana Njombe hao kuomba Sekondari ya Njombe ifundishe kidato cha kwanza hadi cha nne kama ilivyokuwa awali badala ya kidato cha tano na sita kama ilivyo sasa, Spika Makinda alisema jambo hilo si rahisi, kwa sababu baada ya kuanzishwa kwa shule nyingi za kata taifa linakabiliwa na uhaba wa sekondari zenye vidato vya tano na sita.
"Lakini naomba muelewe mazingira ya Njombe Sekondari kuwa High School, baada ya kampeni ya serikali kuanzisha shule za kata hasa kule kwetu ambako ziko zaidi ya 27," alisema Spika Makinda.
Alisema ikiwa shule hiyo itaongezewa vidato, itapokea wanafunzi wengi kutoka mikoani na ndiyo maana waliona ibaki kama ilivyo.
Alisema anadhani hivi sasa serikali inaangalia sera mpya ya kuzihudumia shule zinazoanzishwa kwa lengo la kufundisha masomo ya kidato cha tano na cha sita (high school), vinginevyo kutakuwa na ‘O' level nyingi na kidato cha tano na cha sita chache, hali ambayo haitasaidia.
Awali akisoma risala ya wana umoja huo, Katibu wake, John Mwakyusa, aliahidi kwamba watashiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba mpya hadi mwisho.
Chanzo:Tanzania Daima Jumanne 16-07-2013.
Hapo penye red serikali mbili za sasa serikali ya pili ina ardhi? mbona inaendeshwa? Kwa mfumo wa sasa tuna serikali ya Zanzibar na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa tanzania,kama hiyo serikali ya pili kwa sasa ina ardhi basi hata zikiwa tatu itaendelea kuwa na ardhi kwa sababu muungano utahusisha Zanzibar na Tanganyika ambazo ni nchi zenye ardhi.Suala la kuwa na marais watatu,maspika watatu n.k siyo issue ni nchi gani duniani yenye marais wawili, isipokuwa Tanzania naamini ulimwengu hautashangaa maana kama tuna viwili-viwili hawashangai hata tukiwa na vitatu-vitatu kwa maslahi ya taifa letu hawatashangaa pia.kila serikali ina utaratibu wake kwa maslahi ya raia wake.Huwezi kuiga wanaofuga kuku ili ufuge mbuzi.
Si busara kiridhia kupata katiba feki kwa kisingizio cha kuwahi uchaguzi,uchaguzi wa viongozi ni kila baada ya miaka mitano lakini katiba ya nchi tangu uhuru ndo tunaishuhudia ikiundwa upya,hivyo tufanye kwa umakini wote.
 
Mkuu hayo sasa ni mawazo yako yageuze na upande wa pili kwa maana ya hasala usilenge faida peke yake.
 
Kwa nini mkuu! Kwani chadema inahusikaje sasa hapo. Katiba isiwe mali ya chama fulani au mtu fulani.kila mtanzania na taasisi watoe maoni na wasubiri uamuzi wa wengi.hayo ni maoni ya mtu mmoja...makinda. basi km anaona huo ni mzigo aseme kama anahitaji serikali moja.maana ndo haitakuwa mzigo.

Katiba? mimi siongeleai katiba naongelea kutofanyika uchaguzi. Si mnajuwa maana yake nini?
 
Sasa hapa nimekuelewa,ila wenye tumbo moto wanaweweseka na serikali tatu,wanajua zikipita, kura za bure zinapotea,kwa sababu zanzibar anachukua cuf tanganyika CDM atakayeshika muungano kama hayuko bara wala visiwani ndipo msemo wa bibi wa kutokuwa na ardhi unajidhihirisha. maana fikira za... haziwezi kudumu mwezini
 
Kama haiwezekani basi si Muungano uvunjwe tu kwani tatizo liko wapi? Ni wazi kuwa serikali mbili watanganyika wengi hatuipendi na hata wazanzibari, serikali moja ndiyo usiongelee kabisa wazenji watakuua sasa kama 3 imeshindikana si kila mtu akae kivyake?
 
Katiba? mimi siongeleai katiba naongelea kutofanyika uchaguzi. Si mnajuwa maana yake nini?
Zomba. Nadhani hapo ndo kwenye mgogoro, unless tukubaliane kwa haraka kwenda kwa interim constitution na kufanya uchaguzi...otherwise hii itakuwa nouma
 
Ya nini gharama za kufanya chaguzi mara kwa mara, wasubiri tu, Jakaya Mrisho Kikwete aendelee kuwa Rais panapo uhai na majaaliwa mpaka hapo katiba mpya itapokuwa tayari, kama miaka mingine 5 au 10 poa tu. Kikwete anafanya kweli.
 
hapa kila mtu analiongelea hili suala kwa upeo na uwezo wake wa kuelewa, wengine nimeona wanaiongelea katiba inayoweza kutupeleka miaka 150 - 200 bila kuyumba lakini ni bahati mbaya kuwa wengine wanaangali 2015, yaani miaka miwili tu kutoka sasa!!! Tuna bahati mbaya sana Watanzania.
 
Back
Top Bottom