Makinda atoa msimamo juu ya pendekezo la serikali tatu

Makinda atoa msimamo juu ya pendekezo la serikali tatu

Mhh! Hapo umepotea mkuu! Kama ni lazima kuwa na mtu anayeitwa kiongozi, si lazima aliyeko sasa akaendelea kukaa kwa kisingizio cha kusubiri katiba. Tunaweza kumpatia nchi Jaji Mkuu akaendesha nchi kwa muda....make by and large tunahitaji mtu aliye-objective. Ukweli kuwa Mh Kikwete ni rais na mwenyekiti wa chama kunamwondoa kuwa objective kwa kuwa tayari anamaslahi ...mgongano wa kimasilahi na kama akiendelea kuwa kiongozi kwa kisingizio cha mpito basi itabidi awe wa Muungano (usio na bajeti), wakati rais wa Tanganyika akiwa amepatikana kiongozi wa mpito ambaye ni impartial and non-partisan.
Ya nini gharama za kufanya chaguzi mara kwa mara, wasubiri tu, Jakaya Mrisho Kikwete aendelee kuwa Rais panapo uhai na majaaliwa mpaka hapo katiba mpya itapokuwa tayari, kama miaka mingine 5 au 10 poa tu. Kikwete anafanya kweli.
 
Suluhisho ni muungano wa serikali moja ya Muungano kama Wazanzibar wako tayari kwa hiyo la hasha kama hawataki tuwe na Serikali mbili zinazotambulika kimataifa (yaani Muungano ubaki historia). Hii itasaidia kupata mapato ya wazanzibar wanaokuja kuangalia mali asili zetu huku bara
 
Serikali tatu kwa manufaa ya nchi nzima.serikali moja kwa hasara ya zanzibar.serikali mbili kwa manufaa ya ccm.wananchi tutapiga kura serikali tatu kama tu wazanzibari hawataki serikali moja.zanzibar wangekuwa tayari kwa serikali moja basi mgogoro ungekwisha kabisa.ili kila mtu anufaike basi serikali tatu ni suluhisho hata kama ni gharama potelea mbali.kama hampendi kauli hizi tatu basi muungano uvunjikeeeeeeeeeeeeeeeeeee......
 
Ni maoni yake na yanaweza yasifanyiwe kazi pia. Hata kama yeye ni Spika wa Bunge sio kila asemacho ni sawa bali kuna vingine pia ni majanga kwa mustakabali wa taifa.
 
Mhh! Hapo umepotea mkuu! Kama ni lazima kuwa na mtu anayeitwa kiongozi, si lazima aliyeko sasa akaendelea kukaa kwa kisingizio cha kusubiri katiba. Tunaweza kumpatia nchi Jaji Mkuu akaendesha nchi kwa muda....make by and large tunahitaji mtu aliye-objective. Ukweli kuwa Mh Kikwete ni rais na mwenyekiti wa chama kunamwondoa kuwa objective kwa kuwa tayari anamaslahi ...mgongano wa kimasilahi na kama akiendelea kuwa kiongozi kwa kisingizio cha mpito basi itabidi awe wa Muungano (usio na bajeti), wakati rais wa Tanganyika akiwa amepatikana kiongozi wa mpito ambaye ni impartial and non-partisan.

Safi sana, atakuwa yupo pale Othman Chande.
 
hapo kwenye red inaonesha huyu mama hana uelewa wa political science hata kidogo. kimsingi serikali haiundwi na ardhi kama anavyodhani, dola pekee ndio inaundwa na watu, ardhi yenye mipaka inayotambuliwa kimataifa, na serikali. sasa serikali na ardhi wapi na wapi


SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema kuna hatari ya uchaguzi wa mwaka 2015 kwa Tanzania Bara kutofanyika ikiwa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa na Tume ya Katiba yatapita kama yalivyo.
Makinda ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Kusini (CCM) alisema ikiwa mapendekezo hayo yatatipishwa na wananchi kama yalivyo, Tanzania Bara haitaweza kuingia katika uchaguzi kwa vile haitakuwa na katiba.
Aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Jumuiya wa Wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Njombe uliofanyika katika Kijiji cha Makumbusho.
Wakati Makinda akizungumza hayo, tayari Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeshatangaza kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya mabaraza kuanzia Julai 12 hadi Agosti 2, mwaka huu.
“Hiyo rasimu tuisome vizuri, nataka tu msome vizuri, je, serikali tatu ‘just imagine’ (fikiria) kuwe na serikali ya tatu ambayo haina ardhi, haina watu, ina watawala tu…. mkasome vizuri, mkasome vizuri,” alisema.
Kwa mujibu wa maelezo yake, Spika Makinda alionesha wasiwasi wa taifa kuwa na serikali tatu. “Nchi hii itakuwa na marais watatu, maspika watatu, mabunge matatu, majeshi matatu, benki kuu tatu… sitaki kuwa biased, ndiyo maana nataka wananchi mkasome vizuri,” alisema.
“Najua Profesa Shivji ameshasema maoni yake lakini inabidi tusome hata mara 10, kwa sababu ni kitu muhimu,” alisema Spika Makinda.
Alisema watu wengi hawajaielewa hivyo kuna haja ya rasimu hiyo kupitiwa ili iweze kueleweka, vinginevyo ikipitishwa kama ilivyo uchaguzi mwaka 2015 kwa Tanzania Bara hautafanyika, kwa sababu katiba haitakuwapo.
Alisema kutokana na mapendekezo hayo, itakuwa vigumu kwa Tanzania Bara kushiriki uchaguzi kwa sababu nyingi za msingi. Alizitaja kuwa ni pamoja na ugumu wa kuwapata wabunge wa bunge la serikali ya tatu kwa vile watakuwa wanachaguliwa katika mikoa.
“Kwa jinsi mikoa ilivyo mikubwa tutaanzaje kupiga kampeni kuchagua wabunge wawili?,” alihoji.
Akijibu ombi la Wana Njombe hao kuomba Sekondari ya Njombe ifundishe kidato cha kwanza hadi cha nne kama ilivyokuwa awali badala ya kidato cha tano na sita kama ilivyo sasa, Spika Makinda alisema jambo hilo si rahisi, kwa sababu baada ya kuanzishwa kwa shule nyingi za kata taifa linakabiliwa na uhaba wa sekondari zenye vidato vya tano na sita.
“Lakini naomba muelewe mazingira ya Njombe Sekondari kuwa High School, baada ya kampeni ya serikali kuanzisha shule za kata hasa kule kwetu ambako ziko zaidi ya 27,” alisema Spika Makinda.
Alisema ikiwa shule hiyo itaongezewa vidato, itapokea wanafunzi wengi kutoka mikoani na ndiyo maana waliona ibaki kama ilivyo.
Alisema anadhani hivi sasa serikali inaangalia sera mpya ya kuzihudumia shule zinazoanzishwa kwa lengo la kufundisha masomo ya kidato cha tano na cha sita (high school), vinginevyo kutakuwa na ‘O’ level nyingi na kidato cha tano na cha sita chache, hali ambayo haitasaidia.
Awali akisoma risala ya wana umoja huo, Katibu wake, John Mwakyusa, aliahidi kwamba watashiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba mpya hadi mwisho.
Chanzo:Tanzania Daima Jumanne 16-07-2013.
 
katiba sio lazima itengenezwe na serikali hii na wala hatuwezi kuahirisha uchaguzi kwa sababu ya katiba watekele pale walipofikia serikali inayokuja ndio ishugurikie katiba uongozi uliopo sasa hautakiwi kuachwa hata kidogo uendelee kwani ni majanga
 
Sielewi ni vipi katiba ya muungano inaweza kupatikana kabla ya katiba ya Tanganyika.
 
VOICE OF MTWARA,

..lakini inasikitisha sana, if not shocking, kwamba huo ndiyo uelewa wa Spika wetu kuhusu serikali 3.

..by the way, nimesikia Job Ndugai, naibu spika, akiunga mkono mapendekezo ya tume kuwa na serikali 3.

..mama makinda alipaswa kuulizwa kama serikali nyingine za shirikisho zina ardhi au la.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom