Makinika na mijusi wa ndani ya nyumba!

Kwel ww unamjua paka vilivyo,kuna mda anakuangalia kwa madharau , sijui anakuonaje[emoji1787][emoji1787]
Pia ana majivuno fulani ukimdekeza sana anajiona ana haki ndani ya nyumba kuliko nyinyi mlio mfuga.
 
Upo sahihi mtumishi wa Bwana, mijusi na hata wadudu, ndege, wanyama wanaweza kutumiwa kiroho...

Sikumoja nikitoka mlangoni asubuhi nikakuta ndege amekufa katikati ya ngazi za kushukia chini..

Nikaingia ndani nikachukua maji yaliyotakaswa nikamwagia na kusali, nikaingia ndani kusudi nichukue zoleo nimtoe pale, dakika chache kufika hayupo...

Vita za kiroho ni ngumu sana mtu asiye kiroho kuelewa...

NB: Wachawi huvaa sura za viumbe
 
Tangu nilipokuwa vitani katika Ulimwengu wa Roho nilipambana na mapepo katika mwonekano wa MIJUSI, na ndicho nilichokuja kukiona ndani ya net.

Mjusi yule alifanyika kitu Cha kuunganisha room na kule mashambulizi yalikotoka.

Najua nikisemacho.

Amen
Hujawahi kuwa na na safari unatakiwa kuamka alfajiri uwahi, ukalala ukoota kwamba ulishaamka na bus ulishaend kupanda, unashtuka unakuta bado hujaamka.

Umewaota mijusi kwasababu wapo akilini mwako siku zote. Kuingia ndani ya net haimanishi kwamba huyo mjusi ni mchawi.
 
Jikite kwenye mada.

Mifugo wakae bandani, hakikisha hakuna panya ndani Ili ikosekane sababu ya kufuga paka.
Iweje wewe umeshindwa kujenga nyumba ambayo haiingizi wadudu na mijusi?

Kuna nyumba wadudu hawaingii kirahisi wala haina mijusi..sasa wewe inaonekana nyumba ina nyufa au ceilling board kuna mahali imeachia.

Unashindwaje kuwadhibiti hao mijusi wasiingie.? Halafu unawashangaa walioshindwa kudhibiti panya
 
Panya na mijusi wanapita mlangoni, Si kwenye nyufa,

So dawa ya kupuliza na Sumu ya panya ni muhimu.
 
Ulokole ni ugojwa wa akili yaani mungu kamuumba paka na mbwa kwa ajili ya kuishi na binadamu alafu ww unasema watu wasifuge wanyama hao ww kama nani?

Suala la mchawi kutaka kukudhuru sidhani kama ana hitaji mzunguko mkubwa namna hiyo.
Kuna mtu na mkewe hawapendi hapendi paka . Juzijuzi w1kamuwekea paka sumu akafa. Kuna mzungu alikuwa anawapa chakula , siku anakuja anaambiwa paka mmoja kafa, yeye hakujua kama kalishwa sumu. Roho ilimuuma balaaa, ila mpaka leo hajui kama alipewa sumu. Ila yule baba naye alikufa kwa ajali wiki 2 baada ya yule paka kufa.
 
Ukiona panya Hali Sumu, au Kila mtego unaoweka anakwepa, hanasi,

Anza maombi mapema, Si panya hao.
Kwa nini uwekee panya sumu haujui ana watoto wanamtegemea kama wewe[emoji28][emoji28][emoji28]
 
No Mimi naona tofauti, hii ni platform nzuri kuhubiri.

Imagine ndani ya nusu saa wanasoma watu 2k.
 
Mungu ni MWEMA, hutushindia vita zetu.
 
Hujui unachoongea. Mimi najua nilichoandika.
 
Panya na mijusi wanapita mlangoni, Si kwenye nyufa,

So dawa ya kupuliza na Sumu ya panya ni muhimu.
Wadudu wanapitia kwenye nyufa. Nyumba yenye nyufa na ambayo ujenzi wake sio mzuri au haujakamilika lazima wadudu wawepo.
Mjusi hataweza kukaa mahali ambapo hakuna chakula.

Panya wanafata uchafu au mahali ambapo pamejaa makorokoro mengi kama stoo.

Ukiona kuna panya mahali ambapo unalala basi kuna tatizo. Hiyo room ipo kama stoo
 
Basi sawa,

MADA umeelewa barabara!!

Ubarikiwe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…