Makinika na mijusi wa ndani ya nyumba!

Sasa kama unakiri paka anaweza kutumiwa na wachawi kukushambulia,

Kwann ukae na paka ndani ya nyumba?

Narudia kusema, wengi wafuga paka, hukosi mchawi katika familia hiyo.

Eva alitumiwa na shetani, kumfitinisha mwanaume na mungu.
Delila alitumiwa na adui kumfitinisha mwanaume na Mungu..
Lkn bado hatukomi, tunaishi nao tu.
Sasa paka kakutenda nini? Au kwa rejea ya kitabu unacho kiamini wapi tunaonywa dhidi ya paka ama mbwa?
 
Unasoma BIBLIA Gani?

BIBLIA inaposema, nimewapa uwezo wa kukanyaga nyoka na nge na wasiwadhuru, ulidhani ni nyoka wapi hao?

Ni mapepo katika maumbo ya wanyama, so ukifuga mbwa, au paka, yayakuja yenye form hizo kupitia wanyama hao.

Adam na Eve ni mada ingine.
 
(Isaya 13:21)
Lakini huko watalala Hayawani wa Nyikani, na nyumba zao zitajaa bundi, mbuni watakaa huko, na MAJINI watacheza huko.

Nyumba za wasiookoka ni makazi ya wanyama hao wachafu kiroho, mapepo na majini.

Nyumba za WATAKATIFU hawakai, huja kutushambulia na tunashinda vita zaidi ya kushinda.

Amen
 
Mleta mada una kiwango gani Cha elimu. Nakushauri ujifunze tabia za viumbe walio karibu na binadamu. Halafu huoni aibu kuamini dini zilizoletwa Kwa njia ya kuwafanya mababu zetu watumwa?
 
Dini zimekuja kuwatia ujinga Waafrica badala ya kuwakombowa.

Hizi illusion zitafikia hadi huyo mkeo utamuona ni pepo.

Anyway usisahau kupeleka fungu la 10 kwa Mtumishi wa Mungu mwakani anahitaji abadiri gari, Prado itampendeza zaidi, halafu wewe utakuwekea mikono kukuombea.
 
Si kucomplicate,

Sisi tuliookoka, ni WA kiroho, macho yapo wazi, hatupaswi kuishi kama vipofu.
Walokole bhana!!,Sasa usifuge Paka wala,mbwa kisa kuogopa Mapepo?,Sasa Yesu uliyenaye si anatosha kukulinda dhidi ya maadui hao wa Kiroho?.Kuna vitu jamaa zangu mnafanya lkn sioni Theological logic ndani yake.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Kufuga paka au mbwa ni tofauti na kuishi nao ndani ya nyumba.

Wengine wanalala na vijibwa vidogo chumbani.

Mbwa lake Banda nje Afanye KAZI ya ulinzi nje.

Afu wafuga paka wengi ni wachawi, fuga kuku utamla supu!!
Kufuga kuku??? Mjini ukiona mtu kafuga kuku alafu anawafungulia kwenda kwa majirani huyo ni mchawi! Kuku ni nyumba za mashetani hasahasa mizimu!
 
Acha mara Moja kufuga paka na kuishi naye ndani ya nyumba, paka au mbwa, Pepo anaweza kuwaingia na akawatumia kukuattack.
Nimeanza kukaa na paka nikiwa na miaka6 akawa analala juu ya neti yangu. Alikufa kwa kuumwa, yule paka alikuwa hawezi kuamka mpaka anione nimeamka kwanza, wonderful enough nakumbuka napelekwa shule ananisindikiza mpaka getini halafu anarudi.

Katika viumbe ambavyo vina upendo wa ajabu ni MBWA. Anaweza kukupenda zaidi ya anavyojipenda. Mzee wangu alileta mbwa wale wa urembo aliwatoa kwa rafiki yake. Ilifika extent mpaka mtu akiwa ananifokea ana react vbaya mno.

Hizo stori sijawahi kuziona kwangu na nimeanza kukaa na hivyo viumbe nikiwa mdogo.
 
Mkuu, uko sahihi.

Mapepo yanaweza kuja kupambana na wewe kwa njia tofauti-tofauti. Pepo linaweza kuji-manifest kwako kama mjusi, chura, mende n.k. Too bad umechelewa kulijua hilo.

Hii ni lugha ni ngumu sana kwa watu wa Mataifa (wasiookoka).
 
Nimekuja mkuku nikidhani mambo ya kibaolojia kumbe takataka
 
Masuala ya wadudu yasikie tu, bora wewe mjusi mi kuna ndugu yangu alistuka usiku anahisi ubaridi pembeni yake, kumbe lahaula kufunua shuka anajikuta kadozi na nyoka pembeni japo kidume ila alipiga yowe kama anabakwa

Hivyo tuchukue tahadhari, kuwaondoa hao wadudu

Paka pia husaidia kuondoa mijusi na nyoka, na mbwa husaidia katika ulinzi

Hivyo ni muhimu kuifunika nyumba yako na damu ya Yesu uishi kwa amani hata kama una mbwa na paka

Pia nilisikia kwenye redio miaka mingi nyuma ya kuwa dawa ya miijusi ndani ya nyumba ni unyoya wa tausi (ule wenye macho), uning'inize mahali ambao unaonekana na watakimbia wote hutaona hata mmoja
 
Mnalale mmekula wanga tumbo limejaa kama mnaenda kulima mikorosho mtwara kwanini msipate ndoto za kutisha!
 
walokole mna shida sana nyie endeleen kuwapelekea watu fungu la kumi wazidi kutajirika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…