Makinika na mijusi wa ndani ya nyumba!

Upeo wako wa mambo ya kiimani uko chini sana. Umeandika upotofu kwa 99%.
Nitachambua hapa hapa.

1. Mapepo, uchawi, vimbwengo nk ni roho, hakuna namna yoyote ile vinaweza kumuathiri mtu yoyote pasipo kuhusianisha imani. Kama wewe unaamini katika Mungu (Yesu Kristo) maana yake hakuna chochote kinaweza kukudhuru wala kukugusa. Ni very automatic phenomenon.

2. Damu ya Yesu ilimwagika msalabani mara moja tu na kutukomboa na kila kitu katika ulimwengu wa kiroho. Hatuhitaji tena kufanya chochote, ni suala la sasa kutambua tu hilo lilishafanyika na kuamini na kukiri hivyo tu. Basi automatically kile kilichofanyika msalabani kinakwenda kufanya kazi kwetu kwa 100%.

3. Kitu chochote kile (kilicho hai au kisicho hai) kinaweza kutumiwa na mapepo (shetani) na kitu chochote kile (kilicho hai au kisicho hai) kinaweza kutumiwa na Mungu. Kama Ibilisi alimtumia nyoka kwenda kumlaghai Hawa kwenye bustani ya Eden, Mungu pia kupitia Musa naye akamtumia nyoka kuleta ukombozi na uponyaji kwa wana wa Israel. Tusikariri.

4. Viumbe vyote kiasili viliumbwa na Mungu, na tangu vinaumbwa mbele ya Mungu vilikuwa vizuri kwa 100%. Kuanzia Paka, mbwa, Mijusi nk.

5. Ndoto ni ndoto tu, tafsiri ya ndoto ni kitu tofauti kabisa. Ikiwa kila tunachokiota tutakitafsiri hivyo hivyo kilivyo, basi tutaishia kuchukiana, kuuana, kuchanganyikiwa nk.


Mwisho kabisa, kiumbe cha hatari zaidi na kinachotumiwa na shetani mara kwa mara kuangamiza watu ni BINADAMU, hususani wale unaowaamini na kuwa karibu nao kuanzia mkeo/mumeo, mtoto wako, rafiki yako nk. Kama unaogopa sana kusambaratishwa na shetani basi ishi mwenyewe tena huko porini kabisa!
 
Hujui kuwa wakristo pia hupambana vitani?

Kubishana na Mimi ambaye nilikuwa katika vita halisi ni makosa.

Kuthibitisha ikiwa nilosema ni Kweli au la, ingia katika maombi. Muulize Mungu ikiwa unaye Roho mtakatifu ndani, ayakuthibitishia.
 
Ulivyosema tu tuache kufuga paka na mbwa,tayari nikajua dishi limeyumba...hawa mifugo wameumbwa na Mungu ili tuwafuge domestically wewe unatukataza,kwanini Nuhu aliwapandisha kwenye safina sasa?Punguza imani za kishirikina utateseka sana.
 
Vita gani bwana....usha athirika kisaikolojia.Ukipingwa unaona kama vita
 
Unahitaji kumwona Saikologist baba ndo ushaenda hovyo wahi.. hii Dunia kilankiumbe kina haki ya kuishi Yule mjusi anakula mbu wanaoenea malaria na nzi wanaoenza Magonjwa ya Kuhara. Ninaonkwangu wengi sana Wala sifuniki neti naishi poa sana
 
Paka ni mnafki sana akiona hauna ramani ya msosi anakupotezea ila mmbwa hawezi kuacha kamwe.
 
Damu ya Yesu haichanganywi na maelekezo ya kutundika unyoya wa tausi wenye macho kufukuza mijusi,

Ukiamua njia ya Yesu kaa hiyo hiyo, na ukiamua kwingine Baki huko.

Kuchanganya Mungu na miungu ni kujitafutia matatizo.

Ubarikiwe
Mbona umeshauri wafanye fumigation damu ya yesu inachanganywa kwenye dawa za kufumigate au?
 
MAMBO YA ROHONI UNAYALETA MTANDAONI WENGI HUMU HAWASALI WAPO MBALI NA MAOMBI UNAZANI WATAKUELEWA KWELI UMEFELI PAKUBWA [emoji16]

HUMU WALETEE HABARI ZA VITA VYA ANA KWA ANA KATI YA ISRAEL NA HAMAS HIVI WATAKUELEWA LAKINI SI KWA VITA ZA ROHONI NI NGUM UMEFELI.
 
Acha mjuzi huko mbal sana
Mm hata binaadam nikiwa na wasiwas na wewe nakusanukia. Watu tumepewa jicho la tatu. Lakin hatulitumii. Tunalojicho la kuona visivyoonekana. Walpole mm nawaitaga muliofanya makosa na sasa mnajivisha ngoz ya ulokole. Mtazame mlokole yyte yule anakahistoria flan hivi ka ajab ajabu. Mods wamekuwa na tabia ya kifuta comment zangu. Futeni na hii
 
Halafu kumshtukia mjusi ni jambo gumu maana wanaonekana viumbe dhaifu tu
 
Hakuna cha mambo ya rohoni mkuu ,ili nitatzo la akili .
 
Religion is an opium, discuss 30 marks
 
Paka ni mnafki sana akiona hauna ramani ya msosi anakupotezea ila mmbwa hawezi kuacha kamwe.
Yaa paka ni mnyama ambaye hajaumbiwa shida kabisa na ndio maana hata akitaka kulala hawezi kulala chini ,atatafuta sehemu nzuri kama sio kwenye sofa basi ataenda kulala kitandani au kwenye mkeka alafu huwa hapendi uchafu.

Ukifuga paka alafu akaenda kwa jirani akakuta kuna vinono kuliko unavyo mpa ww na wasimbugudhi anakuhama siku hiyo hiyo , alafu mkionana anajifanya hakujui ili usimuharibie ulaji wake [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji3].
Yeye ni masilahi kwanza kabla ya urafiki, hata hivyo ni mnyama mzuri kuwemo ndani ya nyumba maana anaifanya nyumba kuwa salama dhidi ya wadudu hatari na waaribifu.
 
Kwahiyo na ww unakubaliana na mtoa mada kuwa watu wasifuge mbwa na paka?
 
Kwel ww unamjua paka vilivyo,kuna mda anakuangalia kwa madharau , sijui anakuonaje🤣🤣
 
Unahitaji kumwona Saikologist baba ndo ushaenda hovyo wahi.. hii Dunia kilankiumbe kina haki ya kuishi Yule mjusi anakula mbu wanaoenea malaria na nzi wanaoenza Magonjwa ya Kuhara. Ninaonkwangu wengi sana Wala sifuniki neti naishi poa sana
Mkuu kuwa nao makini nasikiaga ni sumu hatari akidondoka kwenye chakula au kinywaji bila kujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…