Makinikeni na hawa matapeli

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
BEI 420,000/=

TUNAJUA MAFUTA YAMEPANDA BEI PIGA CHINI GHARAMA HIZO TUKUPATIE BASKELI YA KISASA YA UMEME YENYE BATTERY [emoji367] YENYE NGUVU KUBWA ZAIDI , UTAWEZA KUTEMBELEA HADI KILOMETER 120-150 BILA KUSUMBUKA / UNAWEZA KUTUMIA MIFUMO YOTE KWA KUKANYAGA PEDAL AU KUENDESHA KWA UMEME TUPIGIE [emoji3513]LEO TUKUHUDUMIE AU TUMA UJUMBE KWA NJIA YA WHATSAPP NO 0755837542/ OFFER YA USAFIRI [emoji924]
BURE NA VIFAA VYAKE BADO ZIPO KARIBU / TUNASAFIRISHA POPOTE TANZANIA NA NJE YA NCHI PIA
LOCATION [emoji625]ZANZIBAR PEMBA KIUYU

========

Ofisini kwetu tuliziona hizo baiskeli na kuvutiwa nazo sana lakini tukaweka mashaka makubwa kwenye bei.. Hivyo kujiridhisha tukafanya mawasiliano na wahusika. Wakasema imebaki moja tuu na tufanye malipo haraka tutumiwe mzigo

Tulicheki na vyanzo vyetu Zanzibar na Pemba lakini tukakuta hakuna kitu kama hicho, tulitumia pia namba tofauti tatu lakini kila moja ilipewa maelezo tofauti

Huko FM/META bado jamaa wanapost na pengine wameshawapiga watu. Nimeleta hapa kama tahadhari ili vilio visije kuwa vingi baadae

 
Hawa matapeli wameshaibia sana watu kwenye vifaa vya kielectronics wanaweka bei rahisi kumvutia mteja ukijaa tu wanakupiga.

Page zao za instagram wanazipromote haswa ila mara zote wanafunga sehemu ya comments utaona likes tu ila comments hutaona.

Kuna msimu nilivutiwa na bidhaa walipost nikataka kununua ila ikabidi niwasiliane na mdau wangu yuko Z'bar ili afike akacheki hizo bidhaa kwa ukaribu maana picha zinaweza kudanganya, jamaa kufika eneo wanalosema wapo hamna duka la aina hiyo ... na akapewa ushuhuda na walioko maeneo hayo kwamba wengi wamedanganywa na hao matapeli.

Ndio ukawa mwanzo wa kujua kwamba hao jamaa ni matapeli, siku hizi nikitaka bidhaa naenda mwenyewe dukani hata kama wanafanya delivery silipii kabla ya kuona nnachokitaka.

Na wako wengi matapeli wa aina hiyo na wengi washapigwa tukio.
 
Wabongo wanaumizwa sana
 
Jamii forum ni mtandao wenye matapeli wajanja Sana utazani wamesomea wizi kuna vishoka kibao humu ukijaa tu inakula kwako
 
mtu anaona kabisa wajerumani wamesaga kengere zao masaa kadhaa hapo halafu auziwe laki nne kama infinix[emoji28][emoji28]

yapo palm village kule lisilo na betry ni kama 1m.
 
Asante kwa kutujulisha.
 
Jamii forum ni mtandao wenye matapeli wajanja Sana utazani wamesomea wizi kuna vishoka kibao humu ukijaa tu inakula kwako
Sio kama huko kwingine ambako hawadhibitiwi kama hapa JF
 
Kazi kwelii watu washapigwa na wanapigwa na watapigwa mpaka watachaakaa ukiona bei kitonga sana jiulize mara mbili. Watu wapo hapa hapa bongo unapigiwa zanzibar...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…