Makocha wa kigeni hawana jipya, wengi ni wasanii, Simba tumeshapoteana tayari

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kuajiri kocha wa kigeni katikati ya msimu ambapo mtani wetu kashatuacha kwa pointi 6 na hapo bado hatujacheza nao, hatujacheza na Azam, hatujaenda mikoani kuminyana na Ihefu, Dodoma jiji, Mtibwa ni kama tumekubali kuwa yanga bingwa tena msimu huu.

Makocha wa kigeni wa misimamo ya kijinga sana, kuna wachezaji wabovu humo Simba basi kwa mbrazil huyo watakuwa wanaanza, si ajabu mkasikia kikoc kikianza na Mkude, Akpan, Okwa, Nyoni, Mwinuke, Kibu akawa striker pacha na Kiyombo.

Nyie subirini tu, najua wapo wataotukana badala ya kujibu hoja, timu itafanywa vby halafu tutafukuza akina Matola tukidai wanahujumu timu.

Kila la heri

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Sijui mawazo yako ila naamini watoa hela wana maana yao kuna CAF na kuna mwaka kesho... mtoa mada naona unawafikilia Yanga tu pole zako
Kama wewe Simba na hujaifikiria Yanga anafanikiwa vipi wakati alikunyang'anya Mataji yote basi hauko sawasawa.

Yanga ya Sasa haikupi nafasi ya kufanya makosa na nyinyi Simba mmelazimisha kosa litokee, Sasa tusubiri tuone.
 
Kwa mwenye akili ya kucheza na Ihefu na ligi za ndani tu itamuwia vigumu sana kuwaelewa Simba. Kwa wanaoelewa moto wa mashindano ya kimataifa basi wanaelewa wazi Simba wanalenga kitu gani.
Hebu tuambie Simba wanalenga wapi ndugu?
 
Nilitegemea kusikia timu imeleta goal machine au mkata umeme zaidi ya Fraga hapo tungesema timu itafanya vema.
Mgunda afunga goal 7 hapo kocha mwingine wa nini sasa wakati huna kikosi bora?

We have the same players with same problems.
 
ila huyo kocha wa sasa ana cv kubwa sana amefanya kazi uganda si simba wamelamba dume
 
Kwa mwenye akili ya kucheza na Ihefu na ligi za ndani tu itamuwia vigumu sana kuwaelewa Simba. Kwa wanaoelewa moto wa mashindano ya kimataifa basi wanaelewa wazi Simba wanalenga kitu gani.
Simba Kimataifa kwa Mshambuliaji tegemeo John Boko.
Hapo labda Kocha aingie mwenyewe kufunga magoli.

Badala ya kusajiri washambuliaji bora mnasajiri kocha
 
Wivu na roho mbaya sana, mana wameona hawatapata pesa ya udalali na 10% zao ..ukiacha hao madalali, kuna huyu ambaye hataki mtu yoyote awe maarufu zaid yake, ushenzi tu.
Juzi nimemsikiliza Rage.....na kilichokuja kutokea... Sasa sielewi Mgunda walimchukua wa Nini na timu inafanya vizuri.
 
Shabiki mwenzako Execute anasema Mgunda ni kocha mhamasishaji tu, na asiye na mbinu za kufundisha soka! Na amefurahi kuondolewa nafasi ya kocha mkuu.

Una maoni gani juu ya hilo?
Hajui mpira, Bado sijaona shida ya mgunda mpaka sasa, kwa kikosi kile hata akija pep mwenyewe hatoboi.. tutafute wachezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…