kwa hali ya sasa bila kumumunya maneno timu ya England ipo daraja la juu ukilinganisha na miaka kadhaa ya nyuma. England ya sasahivi inaweza kuleta upinzani mkubwa au kushinda timu yoyote duniani. Kweli kocha Gareth southgate mzee wa kizibao amechangia kutengeneza timu na mbinu za ushindi. Lakini mchango mkubwa zaidi uende kwa makocha wa kigeni katika premier league . Soka la premier kwa sasa ndiyo linatamba duniani lina timu 4 champions league mpaka sasa. Pep guardiola kama kawaida kazi yake ni kutengeneza world class player sasa hivi Raheem sterling hashikiki lazima akabwe na mabeki wengi. Pochetino amewatengeneza Kane, dele Ali,tripier, dier wapo kwenye wold class form. Ole Gunnar soljier amewatengeneza rashford,lingard wamekuwa world top class. Juergen klopp anamtengeneza Alexander kuwa top player. Hivyo Safari hii premier ship imefaidika na makocha wa nje. Kipindi bundesliga imekuwa top mpaka Bayern wanacheza na Dortmund fainali ya ulaya timu ya ujerumani ikawa viwango vya juu. Halafu serie A ilipotamba ulaya timu ya Italy ikawa juu. Laliga ilipotamba ulaya spain ikawa juu. Hata hapa Tanzania makocha wa nje wamejaribu kuibua vipaji vinavyosaidia hata afcon qualifications