1. kwa maoni yangu mim nafikiri cha kwanza lugha, unajua mwalimu unachangamana na watu tofauti na mawasiliano ndio katka soccer ndio kitu cha kwanza. huezi kufundisha kwa vitendo tuu lazima uzungumze na ueleweke. tatizo nalo ona sisi watanzania hatuko comfortable na nje kiswahili confidence hivyo ni ile dhana ya uoga tu na kutokiamin
hivyo tunawaacha wakanda,warundi na makocha kutoka nchi mbali mbali kuja kwetu kuchukua kazi zetu lakin ukiangalia elimu ni ile ile wote tuko chini ya CAF hata kama ni UEFA bado atakasoma wa ulaya ndio kinafundishwa Africa hivyo ni kujiamini tu
2. Bado muamko ni mdogo hii kazi imeonekana ni ya wachezaji tu waliocheza ligi kuu na timu ya taifa tu. laikini kumbe ni ishu ambayo mtu yeyote alie interested anaeza kufanya kozi na akawa mzuri katika kufundisha kuliko huyo mchezaji. sasa namba ya makocha tz ni ndogo sana
hivyo n ngumu kua na watu nje kutokana na mfumo wetu wa elimu ya makocha hamasa ni ndogo na kutofuata sharia yaan mtu tu mwenye ameangalia mechi nyingi anafundisha huku level ya chini ambayo ndio muhim kuliko katka soccer..mim nimesoma kozi Niko nje ya tz lakin sijawahi kuulizwa kama nimewahi kucheza mpira kwa hio kubadili mtazamo na watu wapewe fursa kwa wingi hatimaye tutakua wengi ataanza kusaka ajira nje ya Tanzania.
3.pia kupitia process wabongo wengi tunataka short cut mpira hauna hivyo kama mwalim uzoefu ndio unaokupa ajira hakuna lingine hivyo uumie katika kusubiri na kuanzia chini mpaka unafika juu ukiwa competent. sio umesoma mwaka huu na huu unataka uwe ligi kuu. lazima uharibu kuna stage umezivuka hapo kwahio tunakosa Ajira nje kwasababu sisi tunarashia rashia mambo yetu kwa rushwa na usanii sasa huko kwingine lazima ufuate process...
kwahio mambo ni mengi lakin kwa haraka mimi naona hayo yanachangia pia