Makocha wazawa Uingereza wamedumaza soka la nchi yao

Makocha wazawa Uingereza wamedumaza soka la nchi yao

FATHER OF REALITY

Senior Member
Joined
Nov 3, 2014
Posts
123
Reaction score
100
Ni zaid ya miaka 20 tangu makocha wazawa wa ungereza kujaribu kuchomoza kama makocha wenye uwezo wa kufundisha vilabu vya soka nchini mwao au hata kutoka nje na kuwika, makocha hawa wameelemewa na tatizo la kuwa na ufundi wa kiwango cha chini katika ufundishaji wa soka ukilinganisha na wenzao toka ligi zinazowika ulaya kama Uhispania, Uholanzi, Italia, Ufaransa, Ujerumani na Ureno. makocha hawa wanafundisha mpira wa kibishi na kujuana, mpira wa kikakamavu na ndo mana hawana soko nje ya nchi yao katika viwango vinayofanana na makocha wenzao toka nchi nilizotaja hapo juu.

Bob Paisley, Bob Robinson walikuwa ndo moja ya makocha wa mwisho kabisa wa kiingereza kuaminiwa na timu kubwa, mfano Robinson aliwahi kuifundisha Barcelona katika uthubutu wake, kisha akarejea kwao, HAO NDO WAMEONDOKA NA UFUNDI WA SOKA LA KIINGEREZA.
Utamaduni wa soka la uingereza ni duni, uliokosa hasa ufundi wa usakataji soka kwa wachezaji wa viungo WA KATI, yaani namba 6 na 8. Pia wana beki zinazokaba kwa ubishi, usongo na kukamia ndo maana timu za uingereza zinapokutana na mipira laini ya kunyumbuluka zinapata shida sana na mara nyingi zinafungwa au kushinda kwa nguvu kubwa mno na ushindi wa wasiwasi, hili kwa wapenda soka na hakika hamjalifumbia macho mnaliona.

Jambo lingine hata mapinduzi ya soka uingereza yaliyoshuhudiwa miaka ya 1990 na 2000, yametiwa chachu na makocha wasio wazawa, Tazama ujio wa Aserne Wenger aliyeleta changamoto kwa Sir Alex ferguson aliyetaka kugeuza ligi ya Uingereza kuwa mali yake, na baadaye ujio wa ranieri, mourinho, mancini, benitez, anceloti, pellegrin na wengineo, hawa wametia chachu angalau katika ligi ya uingereza.
Chini ya ferguson na Wenger kombe lilikuwa na la waili tu, yaani Man na Arsernal, ukiondoa kocha mwingine aliyeitwa Daglish naye ni Mskotishi mnamo mwaka 1995 alipoibuka na kuchukua ubingwa ligi na Blackburn na kwenda ligi ya mabingwa kuishia round ya kwanza, tokea hapo HADI 2005 miaka tisa yote ubingwa ulikuwa ni wa Man na Asernal tu, huku klabu bingwa ikichukuliwa mara moja na Man U. ligi hii iliweka upinzani sana kalbau bingwa pale makochaa kadhaa walipokuja kumsaidia mzee Fergie aliyekuwa alikuwa na kibarua kigumu mno cha kung,arisha vilabu vya uingereza katika ligi ya mabingwa, Morinho, benitez, wenger, na wengine wa baadaye wakafanya liver kuwa bingwa Uefa ndogo na baadaye UEFA, na huku wengine wakifanya timu za uingereza kuingia nusu tatu kwa pamoja na hata fainali ya wenyewe kwa wenyewe mambo ambayo kwa hispania na italia ilikuwa kawaida, mfano mpaka sasa, ligi ya hispania iliwahi kuchezesha fainali ya mabingwa vilabu vyake mara 3, pia nusu fainali ni nyingi mno.

hivo nina amini ujio wa makocha wageni zaidi tena walio na viwango bora ligi kuu ya england kama claudio raniel, pep guardiola, mourinho, conte, clop nk itaongeza c hangamoto hasa ya kiufundi na kuwapandisha jkufanya vizuri ligi ya mabingwa hata kama si kwa msimu huu.

hii ligi iliwahi kutia aibu ya karne pale Asernal ilipomaliza ligi pasipo kupoteza mechi msimu wa 2004/2004 na kisha kuingia klabu bingwa kuanza kuzifunga timu hafifu kwaq mashaka mnba baadaye kuishia robo huku ligi ikinadia kuwa bora sana, nina hakika aibu ile haitajirudia, hil lilipelekea Sep blata rais wa fifa kipindi hicho kuwaambia waingereza wajihadhari na mfumo na viwango vya timu zao za ndani, wao walimlipa chuk lakini ukweli ulikuja kudhihilika. Katika ligi za Hipania, itali na ujerumani tumewahi kushuhudia timu zao kwa wakati tofauti zikiwa katika ubora wa hali ya juu, lakini hazijiwahi kumaliza ligi pasipo kupoteza mechi.

Kwa kifupi ligi ya uingereza ina kasoro sana za kiufundi, kuhusu hoja za kwamba eti kuna ushindani, ni kweli MAANA USHINDANI unajitokeza sana hata hapa kwetu tz, sababu ni kwamba timu zile zinafanana fanana sana viwango, kama ni chini ni chini. Kuhusu ubingwa wa hizi ligi naomba nichukuwe ligi tatu, tangu 1995 - 2016, uingereza timu zilichukua premier ni 6, italia 6, uhispania ni 5, ujerumani 5. wengi wanapenda kulinganisha spain na england, na husema wale v idume waili wanaonea sana spain, lakini wanasahau timu hizo hizo zinaonea ulaya kwa kilabu bingwa timu 2 kushukua mara 16, uku timu za uingereza zikishiriki pia, basi tukubli spain ni ligi bora kabisa maana waaongoza kuc ukua makombe yote ya ulaya. KUHUSU MAGOLI MENGI, timu za spain kutokana na staili yao zinafungana magoli mengi sana na zinaongoza kwa kutoa dozi kubwa mno klabu bingwa ulaya, yaani kila msimu lazimu timu zaidi ya 3 zipigwe 8,7 na 6 na timu toka spain. Kina asernal wapo wapi kutoa hzo dozi maana pia hupangwa na timu hafifu tena mara nyingi. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, mfumo wa spain ni mzuri sana na sumbufu kisoka.

Halafu timu ndogo za uingereza zote kila mwaka zinashiriki Europa lakini hazifanyi vizuri, ule ubora upo wapi.

Tukubali uingereza wanahitajika makocha wenye changamoto, kama wanasoka tunakumbuka, iliaminika uingereza si ligi ya timu kupigwa kalamu kubwa ya mgoli, kumbe hatukutambua makocha wao ukiondoa wenger na fergie, ingawa wenger sasa amebungua, waliobaki uwezo wao ulikuwa mdogo, kumbuka alipokuja Carlo Anceloti, hatukuona ubora wa hizo beki maana Chelsea ilifunga magoli 105, ikawa imevunja rekodi ya 1960s na kuweka mpya, afu kalamu kubwa , chelsea ilishinda bao 7 mara tau, bao 8 mara moja, 4 na tatu lukuki. Kumbe wakija wanaojua wale mnaoita mabeki wao wanaona watu wa nguvu kulukundu. nina wasiwasi na ujio wa guardola maana ana meche 4 goli 11.

Ni kwamba huyu Anceloti alikuta ukabaji wa utamaduni wa soka la kukamia kamia akafundisha jinsi mabo yanavyotakiwa yawe, lakini la mwisho, ni hili la msimu wa 2014/2015 chelsea chini ya Mourinho alipoteza mechi 3 tu, tena mbili akiwa akatangaza ubingwa, lakini wanasoka hivi ni kweli chelsea msimu huo ilikuwa na uwezo wa kupoteza mechi 3 tu katika ligi bora kabisa, twajifanya hatuoni, afu klabu bingwa akatota kwa psg, huku barca katika ubora kabisa akapata vipigo 4 na droo sita, huku madrid akipigwa mara 6, na atletiko mara 7.

Hivi huoni chalenji ndogo ya timu za uingereza ISIYO NA DIRA NDO INAMPA KIBURI WENGER KUFIKIRI KWAMBA ALIANDIKISHWA KUBAKI TOP FOUR TU, pia ufundi mdogo wa timu nyingine ndo unafanya wakishiriki klabu bingwa wapate shida sana? Hv kweli kwa kiwango cha Arsernal cha miaka ya karibuni, ni cha kutotolewa top four.
KWA UJIO WA HAWA WAALIMU MABO MMENGI YATABADILIKA.
KARIBUNI TUZUNGUMZE SOKA.
 
KAMA LIGI KUU YA UINGEREZA INGEKUWA DARASA LA SHULE YA SEKONDARI....

1.Liverpool ni mwanafunzi ane jisifia
na kuona ana akili kwa kuwa babu
yake alifaulu kwa division one japo
yeye anapata zero.

2.Manchester city ni mwanafunzi wa
kishua ambae wazazi wake
wanamnunulia vitabu vingi na vya
gharama lakini ni mvivu wa kusoma
hii inamfanya afaulu mitihani ya
ndani lakini nje ya shule ana fail.

3.Arsenal ni dogo maskini mtulivu
darasani anaesongoka sana na
huwa anabahatisha kuwa wa
kwanza kwenye mitihan ya mid term
ila mtihani wa taifa anafeli.

4.Tothenham ni dogo anaefaulu
somo moja tu mara nyingi huwa
anapishana maksi chache na arsenal.

5.Chelsea ni mwanafunzi wa kishua
ila mtemi wa darasa zima haswa
kwa wanaoongoza darasani ambae
akifeli tu anamlaumu ticha wake
mpaka afukuzwe.

6.Everton ni dogo mcharuko na
mjanja mjanja anae soma kipindi
cha mtihani tu kwa ku paniki.

7.Manchester united ni dogo
mwenye akili za kawaida ila muongo
muongo anaetegemea chabo na
kuiba mitihan tatizo anaemfanya
aibe mitihani kesha staafu ndo mana
now anapiga F kila pepa japo
kanunuliwa vitabu vipya vilivyo nje ya
silabasi.
 
Back
Top Bottom