Makocha wote wanatimuliwa, ila Matola anabaki kwanini?

Makocha wote wanatimuliwa, ila Matola anabaki kwanini?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nawauliza WanaSimba Wenzangu, kwanini ni Matola pekee anayebaki pale wanapoondolewa Makocha wenzake kwa sababu ya kiwango duni cha timu, Kwani yeye si sehemu ya benchi la Ufundi au Matola ni sehemu ya Uongozi?

Ikiwa kama Matola ni mzuri kuliko Makocha wa Nje tunaowapa mikataba ya hela Ndefu, kwanini sasa tusimpe Matola Mkataba kamili kama wa wale tuliowatimua ili ainoe Simba , tunaogopa nini ikiwa yeye si mbovu?
 
Huu ujinga ndio unaofanya ionekane Simba bado kuna mambo ya kiswahili yanaendelea, hii kauli aliwahi kuitoa Aussems wakati ule wakimfukuza kwa majungu tu, naamini Matola atakuwa analindwa na baadhi ya wajumbe wa bodi.

Matola amekaa Simba miaka mingi, wamekuja makocha wengi wamefukuzwa, lakini sioni chochote kipya kutoka kwake, anaonekana hajajifunza chochote toka kwa makocha wote waliopita Simba, sijui bado yupo Simba anafanya nini?
 
Mimi ni Utopolo kwa hiyo sina la kuchangia katika hili suala la Matola wa Makolo ila ni kocha mzuri sana sioni sababu ya kumwondoa[emoji2099][emoji2099][emoji2099]
 
Wanataka awe kama Zidane , 😀😀 , Zidane alikuwa chini ya Mourinho , Anceloti, Benitez , n.k badae akapewa timu akafanya maajabu , Simba na wao wanacheza hyo kamari ...!! Wacha tuone
 
Back
Top Bottom