Makombora ya kutoka Gaza sasa yafika Telavivi

Makombora ya kutoka Gaza sasa yafika Telavivi

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Katika wiki hii peke yake jumla ya wapalestina 24 wameshauliwa huko Gaza na ukanda wa magharibi kutokana na mashambulizi mazito kutoka ndege za Israel.Chanzo cha mashambulizi hayo si kitu cha kutafitiwa kwani mataifa ya Palestina na Israel huwa daima yako vitani.

Kwa kujua wapalestina wote wamezingirwa na majeshi ya Israel na kwamba eneo la Gaza ni kama gereza kubwa kuliko yote duniani lililozungukwa na walinzi pande zake zote,hivyo mafanikio madogo ya mashambulizi ya wapalestina yanaonekana ni mafanikio makubwa sana kwao.Hapo zamani vita vilipoanza walikuwa wakitumia manati peke yake.

Kwa sasa vijana wa Palestina wameweza kutengeneza makombora ambayo pamoja na kukosa nyenzo na ufundi lakini kila siku huwa yanaongezeka ubora na masafa yanapofika kiasi kuwa mara kadhaa yameleta madhara kwa majeshi na raia wa kiyahudi,

Moja ya mafanikio yao kwa sasa ni kuweza kurusha makombora yanayofika mpaka Tel Aviv mji mkuu wa Israel ulio zaidi ya kilomita 80.Mengi ya makombora hayo huwa yanadunguliwa na mfumo madhubuti wa ulinza wa Iron dome wa Israel.Hata hivyo makombora kadhaa hupenya Iron dome na kutua katikati ya Tel Aviv na mji wa karibu wa Sderot jambo linaloa hofu kubwa kwa wananchi wa Israel kwani ving'ora huwa vinalia mfululizo na matangazo ya watu kutakiwa kujificha kwenye mahandaki na kulazimisha mashule na masoko kufungwa.

<iframe width="400" height="500" frameborder="0" src=""></iframe>​
 
Umeandika kishabiki sana bwashe wewe ni mdini na haitawasaidia kurejesha palestina.

Mlishapoteza zamani kwa kudanganywa na arab countries so leo tafuteni namna ya kuishi na mbabe wenu Israel kwa amani ok
 
Aliyemtegemea Kisha shikishwa adabu.

Waarabu nao wanapatanishwa...tega sikio kifuatacho.
20230413_223055.jpg
 
Umeandika kishabiki sana bwashe wewe ni mdini na haitawasaidia kurejesha palestina.

Mlishapoteza zamani kwa kudanganywa na arab countries so leo tafuteni namna ya kuishi na mbabe wenu Israel kwa amani ok
Sio kishabiki.Nilichotaka kusema ni kuwa hata ukiwa na nguvu namna gani kama unaonea watu basi usitarajie kuishi kwa amani na iko siku utapigwa tu na kijana mdogo kabisa.Ukitaka udumu na heshima basi siku zote usiwe mchokozi.
 
Kabisa. Kama Russia na uchokozi wake anavyopigwa na Ukraine.
 
Back
Top Bottom