Makonda afanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Afya Kisesa usiku

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Your browser is not able to display this video.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amefanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Afya Kisesa usiku, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wananchi kuhusu huduma zinazotolewa katika kituo hicho.

Ziara hiyo imelenga kujionea hali halisi ya utoaji wa huduma na kufuatilia changamoto zinazowakabili wananchi wanapohitaji huduma za afya
 
well done waziri Makonda 🤝
 
Je kuna tija yoyote kwa Waziri wa habari kwenda kukagua vituo vya afya nchini?
Yes,
in fact ni jambo la kawaida kabisa kwa waziri wa habari kukasimishwa wajibu fulani na waziri wa miundombinu au wa afya kutokana na muingiliano wa ratiba ya waziri husika.

hivi sasa mawaziri wengi, wako ng'ambo na waziri mkuu, lakini pia na makamu wa Rais.
Haiwezekani kazi ikaachwa kufanywa na waziri mwingine ikiwa waziri husika hayupo na aliahidi kuwepo kuifanya kazi hiyo kwa siku husika.

You ladies and gentlemen you don't understand many things ee, right?

waziri mkuu yupo ng'ambo now,
unajua nani anakaimu nafasi hiyo kwa sasa? Or you are talking tu because it's free to talk?🐒
 
Sasa waziri wa afya anafanya nini ofisini
 
(Status -Seeking) kutafuta hadhi kibinafsi ili kujinufaisha.Hili eneo huyu Konda ni mahiri kweli kweli.
 
Kila nikikutana na post yako nakuonea huruma sana.

Kwanza ni lazima uchangie kila uzi hata kama huna hoja. Unabakia tu kusema ok ili uonekane pale Lumumba kuwa upo kibaruani.

Pole sana maana kibarua chako ni kizito sana.

Waziri wa habari wa nini kwani hakuna wizara ya afya yenye waziri, naibu na hata katibu mkuu.

Ni jambo la kawaida waziri wa habari kukaimishwa na waziri wa wizara nyingine kwani hakuna manaibu huko?

Waziri mkuu unasema yuko ng’ambo ndo sababu nyingine hata hueleweki.

Haya mateso yote unapewa ujira gani? 🤦🏾‍♂️
 
Sio mbunge wa eneo husika,sio waziri wa afya, sio Waziri wa TAMISEMI kaenda kama , sifa za kijinga kabisa,...sasa unampongeza kwa drama , au kuwavuta wajinga wasio jielewa ,au kwa kujifanya mjuaji ??? RUBBISH
 
Duh! Kawatelekeza wananchi wa Arusha? Kisesa si ni Jimbo la Magu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…