Ndio wajue bongo vipaji vingi sana na vinapotea mapema..
Huyu dogo alikuwa anacheza mtaani...
Ni kipaji kizuri, anafurahisha kumtazama, anaelekezeka, ana nidhamu.. nilikuwa naenjoy kucheza nae sababu ya nidhamu ya kusikiliza maelekezo uwanjani, sababu wengine kucheza bila kuelekeza hatuwezi 😂🤣, anajua hapa nacheza na mkongwe anakusawazishia makosa safi kabisa.
Lakini yeye hakuwa ndio top top talent pale, walikuwepo vijana kama wa3-5 hivi wanamzidi.. aisee wengine wakajichanganya kwenda yanga under 17, wakatoboa mpaka under 20, safari imeishia hapo, ni mmoja tu ambae yupo under 20 ya azam ndio tunahisi anaweza toboa..
Bongo wangewekeza huku chinj, na huyu dogo asidanganyike kusajili simba au yanga, atapotea mapema..
Serikali isaidie hawa watoto kupata timu huko nje... bata academies za kueleweka huko, ajax, benfica huko etc ndio watapata vizazi bora