GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Madudu anayoyaibua yanawaumbua watangulizi wake na hata "maRC"wa mikoa mingine. Kwa sasa anajulikana nchi nzima, lakini kuna watu hawayajui hata majina ya wakuu wa mikoa yao.
Mbali na kuwa anayoyafanya yana maslahi kwa umma, si wote, hasa watawala wenzake, watakaomfurahia.
Naamini naye ana account humu. Ujumbe utamfikia.
Ninayataja baadhi ya makosa aliyoyafanya ili asiyarudie.
1. Kejeli kwa wanawake
Kada mwenzake wa Chama alimtuhumu kuwa anawadhalilisha wanawake. Bila shaka tuhuma zimeibukia pale alipomwambia Eng. wa kike asiongee kama anayechumbiwa kwa sababu yeye ana mke tena mzuri. Hapo alikosea. Hakupaswa kumjibu hivyo. Ni sahihi kukemea pale inapobidi, lakini kukejeli na kuainisha iwe ni mwiko.
2. Kupigiwa magoti na Mkurugenzi wa jiji la Arusha
Nionavyo, asingepaswa kuliweka hilo wazi. Maadam huyo bwana alimfuata faragha katika jitihada za kuokoa kibarua chake, asingeueleza uma yote yaliyotendeka ofisini wakiwa wawili. Hakukuwa na umuhimu wa kueleza kuwa mkurugenzi alimpigia magoti. Kiongozi hapaswi kusema kila kitu hasa kama hakina maslahi kwa anaowaongoza.
3. Mawaziri wanaomtukana Rais
Labda kama mfumo uliamua kutumia mbinu ya "gun boot diplomacy" kuwanyamazisha wapinzani wa Rais Samia walio Serikalini kwa kumtumia Makonda.
Kinyume na hapo, alikosea. Alipaswa kuliwasilisha suala husika ama kwa bosi wake (Rais) au Chama chake au vyombo mamlaka zingine zinazohusika. Alichokifanya Monduli kilitafsiwiriwa kuwa alikuwa akitafuta umaarufu, na pengine, kujipendekeza kwa Rais Samia.
4. Kutabiriwa Urais
Inawezekana ana ndoto ya kuja kugombea Urais wa JMT, na si kosa akifanya hivyo. Lakini anapaswa kujihadhari ili wanaokitamani hicho kiti wasione anajitengenezea mazingira ya kujiimarisha katika hilo. Hawatachelewa kumtengenezea zengwe la kumkwamisha. Kitendo cha baadhi ya watu kuonesha kuwa wanatamani awe Rais wa JMT kinamwongezea maadui.
Kuna watu wamekuwa wakijiandaa kwa hiyo nafasi tokea 2010. Hawatamfurahia hata kidogo, na ikizingatiwa kuwa miongoni mwao ni watu wenye ushawishi Serikalini, wanaweza kutengeneza mkakati wa kumdhibiti. Kama ana nia ya kuja kugombea, kwa sasa anapaswa kuigiza kutokuwa na uhitaji huo. Huo ni kwa usalama wale mwenyewe na ndoto yake pia. Nafikiri anazijua fitna za wanasiasa wa Tanzania, hasa wa Tanganyika.
Pamoja na mapungufu yake kama ilivyo kwa binadamu wengine, Makonda anafanya kazi nzuri. Leo hii kungeitishwa kura ya kumchagua RC bora, Makonda angeibuka kidedea.
Kama atajitahidi kujizuai asiongee kwa mihemko, ataweza kufanya makubwa zaidi.
Bila shaka anaweza kufanya hivyo.
Ukimwangalia Makonda wa miaka ya nyuma akiwa RC wa Dar Es Salaam ni tofauti na WA sasa RC wa Arusha. Makonda wa Arusha anaonekana "amekua". Hata hivyo, bado anapaswa kukua zaidi ya hapo alipofikia.