Makonda aonya Wanasiasa wanaolenga Urais 2030, aahidi kuwashughulikia wanaomsaliti Rais Samia

Makonda aonya Wanasiasa wanaolenga Urais 2030, aahidi kuwashughulikia wanaomsaliti Rais Samia

Kauli tata..Huwenda alishaaidiwa Urais anaona kuna wanao wanacheza karata ya kumpindua au anajisogeza karibu na Urais...Viongozi punguzeni kauli za vijembe tena kwa lengo la Urais..Urais hauji kama mnavodhani.Sasa mnatuonesha nini sisi Wananchi wenu?
 
Humjui DAB wewe nenda kamuulize yule aliekua Mbunge wa Arusha mjini alikua anaitwa nani vile? Yule aliitisha Mashekhe akawapa ubwabwa anaitwa nani vile?
 
Eti naye anautaka Urais 2030 anaanza kuwapiga bit wenzake
Screenshot_20240716_193908_Google.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Christian Makonda amesema kuelekea mwaka 2030 wapo wanasiasa wengi wanaotaka kutumia shida za wananchi kupata uongozi Mkuu wa Nchi, akiahidi kushughulikia wale wote wanaopanga njama za kuharibu na kudhoofisha jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ili kufanikisha ndoto zao za Urais.

Makonda amebainisha hayo leo Jumatano Machi 25, 2026 mkoani Arusha mbele ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa mkutano wa mwaka wa wadau wa elimu kwa umma nchini, akiwaonya pia wateule wa Rais ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kupanga safu za kuwania Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, akiahidi kutomsaliti Rais Samia Suluhu.

"Mimi tukiwa kwenye vita situmi mtu, nakuja mwenyewe kukushughulikia na nina bahati pia ya kusema na Mungu, watu wote hawa wanaojipanga na Urais hawawezi hata kushika Urais mwaka 2030, mtaniona hapa na hili wekeni kwenye kumbukumbu, hawatapata kwani Watanzania si wasahaulifu na pia tutaweka rekodi ulifanya nini awali na ukweli ni kuwa huwezi kuwa malaika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi. Shetani ni shetani tu hata kama akizeeka”, amekaririwa Makonda.

Akibainisha kukerwa na kuona baadhi ya wanasiasa wakiwa kwenye mipango kuelekea 2030 pamoja na kutaja uzoefu wake katika siasa, Makonda ameeleza pia kushangazwa na maigizo ya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiigiza kusikiliza kero za wananchi, kuikosoa serikali pamoja na kutaka kujiweka kando na serikali, akimpongeza Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kusimama imara na Rais Samia Suluhu Hassan, kumtaka kutokatishwa tamaa na kuahidi kusimama na Rais Samia dhidi ya wote wanaompinga.

Baada ya kumaliza kuwashughulikia wanaSiasawa wa upinzani, sasa wamegeukiana na kuanza kuchapana wenyewe makonde ya nguvu kuhusu nani kuwa rais 2030 tena mapema sana hata ya Oct 29 hayajapoa wala kutolewa report yake.💥💥Acha wachapane maana washaanza kulalamika vifo vya ghafla vya wanasiasa wao!!
 
Attachments

  • 20260110_023125.jpg
    20260110_023125.jpg
    154.6 KB · Views: 23
Baada ya kumaliza kuwashughulikia wanaSiasawa wa upinzani, sasa wamegeukiana na kuanza kuchapana wenyewe makonde ya nguvu kuhusu nani kuwa rais 2030 tena mapema sana hata ya Oct 29 hayajapoa wala kutolewa report yake.💥💥Acha wachapane maana washaanza kulalamika vifo vya ghafla vya wanasiasa wao!!
Na hiki ndiyo anachoringia akichanganya hilo sambwanda lake.
 
Yan hata mwaka haujaisha watu washaanza kutishiana uchaguzi unaokuja dah! Alafu unambie watu hawana uchu wa madaraka?ila dalili za mama kuwa nae Hadi 2035 naziona 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hivi anavyosema hatomsaliti Rais SSH inamaanisha Mama atataka kugombea tena 2030?
 
Back
Top Bottom