Makonda ashtakiwa kwa Bashiru, hakika wameamua kumzuia Paul

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Katibu Mkuu,
Chama Cha Mapinduzi ,
S.L.P 50,
Dodoma.
15/07/2020.

Ndugu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, (Dkt) Bashiru Ally,
*
YAH: NDUGU PAUL MAKONDA KUVUNJA KANUNI NA SHERIA ZA UCHAGUZI KIGAMBONI.*

Husika na kichwa cha habari,

Kwa heshima kubwa sisi wana CCM Vijibweni-Kigamboni tunapenda kuleta taarifa hizi kwako. Ndugu Paul Makonda amekuwa akivunja sheria na kanuni za uchaguzi kabla na baada ya zoezi la kuchukua fomu za kutia nia yakugombea majimbo za ndani ya chama.

Tunaamini kila mtanzania mwenye sifa zilizoanishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ibara ya 67 (1a-c)) pamoja na katiba ya Chama cha Mapinduzi ana haki yakugombea kuwa kiongozi. Lakini ni vyema taratibu zikafuatwa na waliokiuka wakashughulikiwa ipasavyo. Ni jambo lisilopingika kuwa Chama Cha Mapinduzi ni taasisi kubwa na Kongwe si tu Tanzania bali hata Duniani kote. Tunajua kuwa chama chetu chini ya Jemedari na kiongozi wetu mkuu Dkt John Pombe Joseph Magufuli, ambae ni mwenyekiti wa chama hiki pamoja na timu yake itayachukulia kwa umakini malalamiko haya. Mwenyekiti wetu wa chama, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekuwa akisimamia kwa umakini mwenendo wa chama na ameonyesha dhahiri jinsi ambavyo chama kinatenda haki na usawa kwa wanachama wote. Ni wajibu wetu sisi wanachama kumsapoti wakati wote hasa tunapoona mambo hayaendi sawa kwa kutoa taarifa ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na mwenyekiti pamoja na jopo lake lote. Yafuatayo ni mambo machache ambayo yamekiukwa na Ndugu Paul Makonda:

*Kwanza* , ndugu Paul Makonda amechukua fomu ya kutia nia yakugombea ubunge wa jimbo la Kigamboni wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam. Hivyo alichukua fomu akiwa bado ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dar-es-salaam. Jambo ambalo limevunja “Natural principle of justice: Nemo judex in causa sua. You cannot judge your own cause” kwamba “hauwezi kuamua kesi yako mwenyewe au kesi inayokuhusu”.

Ndugu katibu mkuu, kitendo alichokifanya Paul Makonda kinaonyesha mgongano wa kimaslai kwani kiongozi hawezi kujitathmini yeye mwenyewe na hivyo, kuchukua fomu yakugombea wakati akiwa mkuu wa mkoa haikuwa sahihi. Utaratibu ilikuwa ajiuzulu kwanza halafu asubiri baada ya kupewa ruhusa. Vyombo vyote vya habari vikiwemo Mwananchi, ITV, Millard Ayo, Clouds na vingine vimetangaza kuwa mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam amechukua fomu ya kuwania ubunge jimbo la Kigamboni na si “Aliekuwa mkuu wa mkoa amechukua fomu yakuwania ubunge jimbo la Kigamboni”.

*Mbili* , Tahere 12/07/2020, siku mbili kabla hajachukua fomu za Ubunge wa Chama cha Mapinduzi, Ndugu Paul Makonda alikuwa Vijbweni Kigamboni akigawa fedha kwa wananchi wa Kigamboni. Wasamalia wema wakatoa taarifa Takukuru wilaya ya Kigamboni, Takukuru walipofika eneo la tukio ndugu Paul Makonda alitoa kauli kuwa *“….waambie hao Takukuru kuwa alie ndani ni bosi wao”.* Ndugu Katibu mkuu, CCM ni taasisi kubwa hivyo wafuatilie haya kwa umakini na watapata majibu.

*Tatu* , tarehe 14/07/2020 siku aliyochukua fomu ndugu Paul Makonda ilifanyika kampeni ambayo haikufanyika kwa mgombea yeyote aliechukua fomu. Kampeni hii ilifanyika kupitia kipindi cha “ _Masham Sham_ ” kinachotangazwa na bibi Dida na Bwana Indris kinachorushwa na Wasafi Radio na Televisheni. Kipindi kilimnadi ndugu Makonda kuwa ni kiongozi sahihi wa jimbo la Kigamboni. Jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria za uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi. Kipindi kilitaja wagombea mbalimbali waliochukua fomu ndani na nje ya Chama cha Mapinduzi. Lakini, kwa upekee kabisa kipindi kilitaja maneno ambayo yalilenga kwa makusudi kumfanyia kampeni ndugu Makonda ambayo yalikuwa katika dakika ya 17:33, 30:03 na hasa dakika ya 32:44-36:37. Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa na watangazwaji ni *“….. Jamani Makonda eeeh Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam………anakuja Kigamboni…….wakazi wa Kigamboni wanasema wamefurahi sana……….Mheshimiwa Makonda ni mwanzo mzuri………..kwahiyo kama itapendeza………..kwanini isipendeze….itapendeza tu……mwaka 2020 mwezi wa 11 hatutaongea pia kama mheshimiwa mkuu wa mkoa tutaongea na mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni……"…mheshimiwa Makonda ameonyesha nguvu yake kubwa katika miaka yote ambayo amekuwa hapa Dar-es-salaam…….kwahiyo yote kwa yote tuseme tu Makonda anatosha katika hii nafasi………”* . Ndugu Katibu mkuu, Bwana Makonda ni mlezi wa kundi la Wasafi , hivo kwa maneno haya na mahusiano aliyonayo na kundi la Wasafi ambalo ndio wamiliki wa chombo hiki ni dhahiri kwamba Makonda amekitumia kipindi hiki kufanya kampeni kitu ambacho ni kinyume na utaratibu kwani muda wa kampeni haujafika. Kipindi hiki kimetaja watu mbalimbali waliochukua fomu, lakini kwa undani na kwa upekee kabisa kimetaja na kumnadi ndugu Makonda. Linki ya kipindi ambayo inathibitisha haya ni hii hapa:

*Nne* , ndugu Makonda ametengeneza video clip ambayo inasambazwa kwa kasi kubwa mara tu baada ya kuchukua fomu. Clip hiyo yenye jina la “ *Mtoto Zainabu* ” inamuonyesha mtoto wa shule ya msingi akimnadi ndugu Makonda. Clip hii imeunganisha mambo mengi ambayo ameyafanya ndugu Makonda kipindi cha ukuu wake wa mkoa. Ndugu katibu mkuu ni dhahiri kuwa kipande hiki cha video kinachosambaa kimeandaliwa kwa ajili ya kampeni kwani kimejaa mambo mbalimbali ambayo mtoto yule hana uwezo wakukusanya hayo yote yalio ndani ya clip hiyo na kuyasambaza. Kwa hali ya kawaida na akili ya kawaida, ubunifu mkubwa uliofanyika katika kuunganisha matukio ya zamani ya ndugu Makonda hayawezi kufanywa na mtoto yule. Kwani ndani ya video hii kuna takwimu mbalimbali zimetajwa zikiambatana na picha za matukio ambayo maudhui yake ni kampeni. Ni wazi kwamba ameandikiwa na kupangiwa cha kuongea, pamoja na kuhaririwa na watu wenye ujuzi mkubwa katika utengenezaji wa video fupi za namna hii. Baadhi ya mambo yaliyotajwa na mtoto huyu katika clip ya dakika 3 na sekunde 15 ni _“Shikamoo kaka Makonda, ni mimi Zainabu. Mdogo wako wa hiyari ninaeishi juu ya pande la ardhi lenye umbo la…..liitwalo Kigamboni, kata ya Mji Mwema………….Kwanza, nikupe pole na pongezi……………..kiukweli nimeona mengi uliyoyafanya kwa dada na kaka zangu wa Dar-es-salaam……………..sijasahau pia ulivyo……..zinazohudumia akina mama wengi kwa wakati mmoja, ikiwemo lile jingo la ghorofa moja la theatre ambapo upasuaji wa wanawake 36 unaweza kufanyika kwa siku moja. Pamoja na hilo...imagine, hapa bado……kiukweli siwezi kukumbuka kwa haraka kila ulilofanya maana ni mengi mno. Ikiwemo…………pamoja na yote………..niseme nini tena!!!!! Zaidi yakusema karibu sana Kigamboni kaka yangu…..jibu tosha tulilo lililia kwa miaka mingi jambo linalo tufanya sisi wana Kigamboni tujione wenye bahati._ ” Ndugu katibu mkuu huu ni ushahidi mwingine wa Ndugu Makonda kuanza kampeni kabla ya wakati.

*Tano* , ndugu Paul Makonda amekuwa akifanya kampeni za udini akishirikina na shehe mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim. Urafiki uliopo kati ya Sheikh huyu na Makonda haufichiki na ni haki yao kuwa marafiki wa karibu. Lakini, kumekuwa na maelekezo ya Sheikh Alhad kwa waislamu wa Kigamboni kumchagua ndugu Makonda wakishirikiana na Diwani mmoja wa hapa Kigamboni. Hivyo, Sheikh huyu amekuwa akitumiwa na ndugu Makonda kuwapigia simu waumini wa kiislamu waliopo Kigamboni wampigie kura ndugu Makonda ili jina lake lipite ndani ya chaguzi za chama. CCM ni taasisi kubwa na viongozi wake chini ya Jemedari Mwenyekiti wetu Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli inauwezo wakufuatilia haya na ikapata ukweli ndani yake. Mifano michache inayoonyesha ukaribu wa ndugu Makonda na Sheikh Alhad Mussa ni: ndugu Makonda alipokuwa akishutumiwa kuhusu uhalali wa cheti chake, Sheikh Alhad alikusanya masheikh na waumini mbalimbali akawapeleka ofisi ya mkuu wa mkoa kufanya dua maalum ya Makonda. Pia, likaja suala tatanishi la Ushoga lililoletwa na ndugu Makonda, ambapo Sheikh Alhad alijitokeza na kumkinga ndugu Makonda kuwa yuko sahihi. Aidha, wakati wa vita ya madawa ya kulevya iliyoratibiwa na ndugu Makonda, Sheikh Alhad aliitisha mkutano na wanahabari “press conference” ya ghafla na kuagiza serikali impe ulinzi maalum ndugu Makonda. Kwa hayo machache, inadhihirisha kuwa Sheikh Alhad, kwa maslahi yake binafsi (sio ya dini) anatoa maelekezo kwa Waislam Kigamboni ili wampigie kura ndugu Makonda.

*Mwisho*, sisi tunaamini Ndugu Makonda amevunja kanuni na sheria za uchaguzi kwa sababu kuu tatu: (1) kuchukua fomu huku akiwa mkuu wa mkoa wa Dar –es-salaam kabla ya kutenguliwa au kujiuzulu mwenyewe, (2) Kuanza kampeni kabla ya muda kwa kutumia video clip yenye jina "mtoto Zainab" pamoja na kipindi cha “Masham Sham” kilichofanyika tarehe 14.07.2020 kilichorushwa na Wasafi Redio ambayo yeye ni mlezi wake, (3) Sheikh wa mkoa Alhad Mussa kutumia kilemba cha dini kumfanyia kampeni Ndugu Makonda.

Tuna imani kubwa na chama chetu chini ya Dr John Joseph Pombe Magufuli kuwa malalamiko yetu yatapimwa ili haki itendeke. Ni matumaini yetu kuwa haya tuliyoyataja yatafanyiwa kazi, yatachunguzwa na hivyo kufanya uchaguzi wetu wa chama uwe wa haki na usawa.

Kidumu chama cha Mapinduzi, Kidumu chama tawala.

Ni Sisi wana CCM wapenda haki.Vijibweni, Kigamboni, Dar Es Salaam -Tanzania.
 
Mwacheni tuu akajaribu viti maalumu maana huku kwingine kaangukia pua
 
Majungu hayapikwi barazani, Bali jikoni. Kila wakati Makondaa, nakumbuka miaka kadhaa nyuma kuna mchungaji mmoja alisema amelifuta jina la Makonda milele, the question is, if he did so, Why does this man still exist?? Wekeni akiba ya Maneno
Kifutio ndio kinafanya kazi saivi
 
Bashite alimchukulia poa sana Dr. Ndungulile. Pongezi nyingi kwa wanaCCM wa Kigamboni. Mmeonyesha ukomavu. Ni uzuzu kumtupa mtu aliyepigana nanyi tangu mwanzo na kuja kuokoteza wahamiaji haramu wanaoibukia kwenu dakika za majeruhi
 
Back
Top Bottom