Makonda awataka Wachezaji Yondani na Nyoni Wasistaafu Kuichezea Taifa Stars hadi wakaribie Umri alionao Mugabe sasa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Huku akijua kabisa kuwa Yeye si Mtaalam wa Soka, hajawahi hata Kucheza Chandimu wala Kusomea Ukocha sehemu yoyote ile achilia mbali Miguu yake ilivyokaa ambayo haiwezi kutoa Ushirikiano kwa Yeye kuwa Mchezaji Mpira Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Taifa Stars ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam amewatishia Wachezaji Kelvin Yondan na Erasto Nyoni kuwa hakuna Kustaafu Kuchezea Taifa Stars na kuwaambia kuwa bado wapo sana tu.

“ Hakuna cha Yondan na Nyoni Kustaafu sasa Kuchezea Taifa Stars na bado mpo sana tu halafu ole Wenu nije Kusikia hamtaki Kuchezea Taifa Stars au Mnastaafu sasa. Na kama ni kuitwa Kikosini Taifa Stars mtaitwa sana tu na Kocha ila habari ya nyie Kustaafu sitaki Kuisikia kutoka Kwenu sawa? “ alisema Makonda.

Kwa Kauli hii na Vitisho hivi vya Makonda kwa hawa Wachezaji Waandamizi wawili akina Yondan na Nyoni ambao walisikika na kukaririwa wenyewe wakisema kuwa wanataka sasa Kustaafu Kuichezea Taifa Stars kwani wamechoka na wanataka Kuwapisha Wachezaji wengine ni dhahiri shahiri kwamba sasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ndiye Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Rais wa TFF na Waziri wa Michezo na kwamba wenye Nafasi hizo akina Amunike, Karia na Mwakyembe wao wapo wapo tu.

Labda tu nimsaidie Makonda kwa kumwambia kwamba kwa Kitendo chake hiki cha Kuwatishia na Kuwalazimisha akina Yondan na Nyoni waendelee Kuichezea Taifa Stars na Wasistaafu kina Madhara makubwa mno kwa Mpira wa Tanzania na tayari kuna Sumu ya aina yake ameshaipandikiza ndani ya Kikosi hivyo leo niwe wa Kwanza kuwaambia Watanzania kwamba kama Makonda ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Hamasa ya Taifa Stars huku akiendelea kuwa na hiki Kiburi chake, Nyodo na Dharau sahauni Timu ya Taifa Stars kufanya vizuri katika Mashindano au Michezo yake yoyote ile na tutaendelea Kuchekwa na kuwa Kichwa cha Mwendawazimu mpaka tukome.
 
K
Kama hii habari ni ya kweli basi tumeingiliwa
 

Kwani yeye ndiye aliyewasajili huko? Mbana anaingilia uhuru wa watu?
 
Pamoja na gundu lote alilowasababishia bado anaendelea hajakoma tu? Balaa la misri halijamsaidia tu kujielewa kuwa anagundu na nyota ya kushindwa kila kitu .
 
Kwani hicho cheo kapewa na nani? Nipeni jibu kwanza.
 
Huyu jamaa ni moja ya kiumbe wa ajabu kuwahi kutokea Tanzania tangu tupate uhuru yaani kadri siku zinavyoenda ndio nazidi kuamini kuwa alipata ziro darasani maana mambo anayofanya hayana uhusiano na msomi hata kidogo.
 
Kwa hiyo anataka waendelee kucheza mpaka watakapopinduliwa kama Mugabe? na vipi watakapotemwa na vilabu vyao napo wataendelea kucheza team ya Taifa.
 
Ndo maana ndoto za huyo strategist juu ya nchi hii zitabakia kuwa ndoto na muda si mrefu ataamka usingizini kugundua ilikuwa ni ndoto tu. Hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kutegemea ushauri wa dab!
Ila tambua kuwa ndiye Think Tank and Chief Strategist wa anayekutawala Kikatiba kwa sasa nchini Tanzania Kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…