Makonda azikataa jezi mpya za Taifa Stars. Adai ziko chini ya kiwango na kung'aka "Tuheshimiane"

Unavofurahi utafkiri hata kama ikiwa ivo kwamba watapata hasara. Mkizikataa hizo wenzenu wanatoa bajeti mpya na ww unaecheka ndo vile, kodi yako inafanya kazi mara mbili kwa kitu kile kileπŸ˜€
Hayo mambo kwa mm naona hayameki sensi mkuu, kawaamshe vijana wenzio pale kariakoo muandamane. Jf hii sio ya kutumia kuamsha vijana kuhus matumizi ya kodi zao.

Tafuten mkakat mwengine wa kuamsha vijana. Mm kila ninacholipia kodi nina uwezo nacho nisichokiweza kulipia ujue sina uwezo nacho. Mwezi wa nne sasahiv sijanunua hata kitu kimoja kinachofika elfu 20 bei yake. Kodi yake itakuwa kias gani?
 
Kimeshaumana huko πŸ˜€πŸ˜€πŸ™ŒπŸ½
 
Waziri yupo sahihi, hii jezi ni kituko haina hadhi ya kuitwa jezi ya timu ya taifa
Acheni majungu. Hizo jezi zina shida gani hadi zionekane kituko? Au mlitaka ziwe na rangi nyekundu na nyeupe ambazo hazipo kwenye bendera ya Taifa? Nyinyi Vilaza sijui ilikuwaje mkapewa madaraka.
 
Serikali ndio inatengeneza jezi, na kumlipa kocha, hao tff hawana uwezo huo!
 
Makonda ni waziri wa kuteuliwa kwa nafasi ya ubunge au naye alishinda uchaguzi wa 29 Octoba 2025?
 
Ubora (quality) unategemeana na kiwango cha fedha kilichokubaliwa wakati wa kupewa zabuni. Yawezekana kiwango cha fedha kilichokubaliwa ni kikubwa kulinganisha na ubora wa jezi ndio maana Waziri anahoji. Vilevile, huwezi tarajia jezi zenye ubora kama umetoa fedha kidogo.
 
Nakubaliana nawe Mkuu Mawembasa1979

Ila jambo muhimu ni utaratibu uliotumika kama ulifuata miongozo, kanuni na taratibu za taasisi

Je TFF inaweza kuitwa kua ni taasisi ya uma kwa maana ipo chini ya serikali? Utendaji kazi wao wa kila siku unasimamiwa na Wizara, idara au chombo kingine cha serikali?

Taratibu na kanuni zao za utoaji zabuni kama hizo upoje? Wanalazimika kufuata sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 pamoja na marekebisho yake ya mara kwa mara kupitia wizara husika au wenyewe wana mamlaka kamili ikiwa ni pamoja na kujiamulia taratibu zake za manunuzi?

Kuhisiana na jezi kama ulivyosema pesa zimetolewa na serikali? Kama pesa ilitolewa na serikali ilitangazwa tender? Bajeti ilikua kiasi gani? Technical specifications zilikuaje? Mzabuni aliyeshinda ali bid kiasi gani?

MKuu maswali ni mengi sana. Ngoja tuone sakata linapoelekea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…