Makonda: Ferdinand atakuwepo kwa siku 3, atakwenda Bungeni, Arusha akiinjoi hali ya hewa nzuri

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Mliokuwa mnasema Paul Makonda huwa haongei kingereza hapa ni wapi?

WAziri Makonda akizungumzia ujio wa Ferdinand ambaye amewasili Mei 19, 2026 amesema atakaa nchini kwa siku 3 na atatembelea maeneo mbali mbali ikiwemo bungeni.

Your browser is not able to display this video.
 
Huyu Makonda anachokifanya sio sahihi kabisa. Ni suala lisilo na faida yoyote kwa Taifa. Rio ni mchezaji mstaafu ambaye hana impact yoyote kwenye huu ulimwengu. Ninamsihi Mama Samia ajitenge na hizi shughuli za Makonda kwa sababu hazina maana.

Makonda ajikite kutengeneza kina Samatta, Simbu na Diamond wengi ili kutangaza nchi. Siki Simbu anashinda world champion kwenye marathon nchi ilitajwa na vyombo vikubwa vyote vya habari duniani bila kulipa hata senti.
 
Huyu Makonda anachokifanya sio sahihi kabisa. Ni suala lisilo na faida yoyote kwa Taifa. Rio ni mchezaji mstaafu ambaye hana impact yoyote kwenye huu ulimwengu. Ninamsihi Mama Samia ajitenge na hizi shughuli za Makonda kwa sababu hazina maana.
Usimuonee wivu Makonda ...

Acha ale nchi, kutesa ni kwa zamu.
 
Sijui vigezo gani vilitumika kumpa huyu jamaa uwaziri, ni aibu kwa mteule wake!.
Jamaa ana mambo ya kitoto sana!
 
Kingrezza cha huyu waziri kinapaswa kuundiwa tume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…