Makonda azikataa jezi mpya za Taifa Stars. Adai ziko chini ya kiwango na kung'aka "Tuheshimiane"

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameonyesha kutoridhishwa na jezi mpya zinazodaiwa kuwa za timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda amesema jezi hizo hazikidhi kiwango anachotarajia kwa timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa kuhusu matumizi ya picha ya Naibu Waziri katika suala hilo. “Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi.

Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa. Tuheshimiane,” aliandika Makonda.

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu mchakato wa kutengeneza na kutambulisha jezi mpya za Taifa Stars, huku suala la mawasiliano na Wizara likiwa miongoni mwa mambo aliyoyasisitiza Waziri huyo

Screenshot_20260917_020445_Instagram.jpg
 
View attachment 3672170
Hivi Kumbe Mh Paul Christian Makonda wako ofisi moja na Mh Mwana F( AA)
 
Yeye kama nani anaweza kukataa jezi za Taifa?, anahusika vipi kwenye masuala ya jezi za timu ya Taifa?. Serikali anaingia kama stakeholder anayeshirikishwa na sio kutoa maamzi.. mwenye mamlaka ya jezi zipi zinafaa na hazifai ni TFF!. Kuwa na VIONGOZI kama Makonda Kuna aibiaha Taifa!.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameonyesha kutoridhishwa kwake na jezi mpya zinazosambaa zikidaiwa kuwa za timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Waziri Makonda ameweka wazi msimamo wake kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, ambapo ameeleza kuwa vazi hilo halikidhi viwango vya ubora vinavyostahili kutumiwa na timu hiyo ya taifa.

Pamoja na kukosoa muonekano wa jezi hizo, Makonda ametoa onyo kali kuhusu matumizi ya picha ya Naibu Waziri wake katika mchakato huo, akibainisha kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa yoyote.

Katika ujumbe wake huo mtandaoni, amesisitiza kuwa Taifa Stars haiwezi kuvaa jezi za kiwango cha chini na kutaka uwepo wa heshima ya kitaasisi kwa kuandika: “Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi. Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu
haina taarifa. Tuheshimiane.”

1789633845085.png
 
Mh. Waziri kaziona jezi kwa maana kapelekewa ofisini au kaziona tu kwenye mitandao?

Kama kapelekewa na yeye akaziona basi sawa anaweza kutoa maoni yake kama mdau mwingine yeyote wa michezo maana utaratibu wa mikataba ya kubuni, kutengeneza na kuuza jezi za timu ya taifa husimamiwa na shrikisjo la soka nchini

Lakini kama kaziona tu kwenye mitandao halafu akatoa remarks hizo kwa njia hiyo nadhani Waziri atakua amekosea na maswali yatakua mengi juu yake. Kwanza ubora hafifu anaozungumzia ni quality ya nguo, dizaini yake au rangi zilizotumika?

Kama ni rangi na dizaini mbona viko poa kabisa

Kwani kuna ubaya gani Naibu Waziri akivaa jezi hizo? Mkataba wa kutengeneza jezi unasimamiwa na Wizara husika? Michezo mengine nchini utaratibu wa kupata nguo zao (kit) upo kama wa TFF kwa maana lazima ukapitishwe na Waziri wa Wizara husika?

Maswali ni mengi kwakweli
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameonyesha kutoridhishwa na jezi mpya zinazodaiwa kuwa za timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda amesema jezi hizo hazikidhi kiwango anachotarajia kwa timu ya Taifa, huku akisisitiza kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa kuhusu matumizi ya picha ya Naibu Waziri katika suala hilo. “Hii sio jezi ya Taifa Stars, Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango chini hivi.

Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa. Tuheshimiane,” aliandika Makonda.

Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu mchakato wa kutengeneza na kutambulisha jezi mpya za Taifa Stars, huku suala la mawasiliano na Wizara likiwa miongoni mwa mambo aliyoyasisitiza Waziri huyo

View attachment 3672170
Waziri yupo sahihi, hii jezi ni kituko haina hadhi ya kuitwa jezi ya timu ya taifa
 
Mara paap designer tender alipewa abduli wakaidizaini mabichi boi kizimkaz pale 😂
Unavofurahi utafkiri hata kama ikiwa ivo kwamba watapata hasara. Mkizikataa hizo wenzenu wanatoa bajeti mpya na ww unaecheka ndo vile, kodi yako inafanya kazi mara mbili kwa kitu kile kile😀
 
Back
Top Bottom