Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Wakati mataifa mengine yakijikita katika tafiti mbalimbali na kuwekeza katika miradi ya kimaendeleo, Makonda siku ya leo amekusanya maelfu ya wananchi na kuanza kukemea roho chafu "zinazokwamisha" maendeleo
"Ndio mkoa pekee ukienda kusoma unafaulu, yale mapepo mgandamizo, mateso wanayoyapata watoto wetu tunayakataa, ijulikane leo ya kwamba Arusha yote ukifanya biashara unafanikiwa. Ijulikane leo ya kwamba Arusha ukifunga ndoa ya kiislamu au ya kikristo hiyo ndoa haitatenganishwa na mtu yeyote zaidi ya Mungu"
"Ijulikane leo mkoa wetu (Arusha) hautapokea tena watoto wasiokuwa na baba, kila mwenye baba atatambulika kwa baba yake... Mila zinazokatandamiza wanawake na kuwanyima haki ya kumiliki ardhi tunazifuta kwa kuwa kila mwanamke ni mfano wa Mungu."
Source: Jambo TV