Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Christian Makonda (Mb), ametangaza kutotambua matangazo ya jezi mpya za Timu za Taifa.
Hatua hii imekuja baada ya mchakato wa kubadilisha jezi hizo kufanyika bila kuishirikisha Wizara, kinyume na maelekezo yaliyotolewa hapo awali mwezi Februari 2026.
Akitangaza uamuzi huo kupitia Taarifa kwa Umma iliyotolewa leo, Tarehe 18 Septemba, 2026 jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Zaituni Mkwama, Mhe.
Makonda ameeleza kuwa uamuzi huo umezingatia kuwa Serikali inawekeza fedha nyingi katika kugharimia na kuandaa timu hizo. Aidha, kutokana na Tanzania kujiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027), kuna haja ya kuhakikisha jezi za timu za taifa zinaakisi manufaa mapana ya kiuchumi na kijamii kwa nchi.
Ili kutatua suala hili, Wizara itaunda kamati maalumu ya kuchunguza mkataba wa mzabuni wa jezi hizo. Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kubaini manufaa ya mkataba huo kwa timu za taifa na kuhakikisha fursa za mauzo ya jezi zinachangia ipasavyo katika uendeshaji wa timu, badala ya kuiachia Serikali pekee kubeba mzigo wa gharama.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa changamoto na mjadala unaoendelea kuhusu jezi rasmi za Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ hivi sasa unashughulikiwa na mamlaka za juu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Msemaji wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, wakati akijibu swali la mwandishi wa habari wa Ayo TV aliyetaka ufafanuzi kuhusu jezi sahihi wanazopaswa kununua mashabiki, kufuatia sintofahamu na mijadala iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Ndimbo amewatoa hofu mashabiki na kuwasihi kuwa wavumilivu wakati jambo hilo likifanyiwa kazi, akisisitiza kuwa timu ya taifa haijawahi kukabiliwa na uhaba wa mavazi ya michezo wakati wa mechi zake.
Pia soma: Makonda azikataa jezi mpya za Taifa Stars. Adai ziko chini ya kiwango na kung'aka "Tuheshimiane"