Makonda ni Trump wa CCM... Ole wetu!!

Ni kuota mchana kweupe kudhani makonda anaweza kuwa Rais, hata kuwa waziri mkuu au Makamu wa Rais hawezi kufika hapo
 
Ni kuota mchana kweupe kudhani makonda anaweza kuwa Rais, hata kuwa waziri mkuu au Makamu wa Rais hawezi kufika hapo
Sifa gani anakosa? Huwazi kuwa kilitokea nini mpaka akawa Mkuu wa mkoa ndani ya muda mfupi kuwa mbunge wa Arusha Kisha Naibu Waziri na Sasa waziri kamili?
 
Bashite hata huko Arusha yenyewe ndani ya chama chao ilibidi abebwe kwa mbeleko mbele ya Bashe kupewa ubunge wa mezani.
 
Hakuna ufanano wowote kati ya CCM na Republicans, Marekani CCM wako madarakani kwa kura za raia, Tanzania CCM ipo madarakani bila kura za raia.
 
Hakuna ufanano wowote kati ya CCM na Republicans, Marekani CCM wako madarakani kwa kura za raia, Tanzania CCM ipo madarakani bila kura za raia.
kura inabidi ziwe ngapi ili zijulikane ni za raia?
 
Unaelewa mambo kinyume, Kukubalika kwa Bashite ni kutokana na nguvu kutoka juu yake, Bashite ni mtu anayejua kucheza vizuri ngoma ya mtawala yeyote. Wakati JK alijua kucheza vizuri ngoma ya mkwere dhidi ya Lowassa na katiba mpya hadi kuvutana mashati na Warioba, wakati wa jiwe alijua kucheza vizuri kila mdundo wa jiwe, alipokuja Samuya alijua vizuri pia kujipachika kwenye circle yake kwa maslahi yake kiasi cha kuweza kuaminiwa kama mwanajeshi mtiifu, he is good opportunistic creature. Kwa upande mwingine Trump nguvu yake inatoka chini kwa base ya MAGA wengi wakiwa wafia dini, fanatics, racists na wajinga.
 
Subjective...
uchaguzi wa mwaka gani unaweza sema ni uchaguzi wa kweli hapa bongo toka tuingie vyama vingi --- zinatofautiana mbinu za kuiba tu, na kadri ccm inavyopoteza ushawishi ndo mbinu kali na wazi zinadhihirika
 
uchaguzi wa kweli ni very subjective, kama jiwe tu aliiba who is mama kizimkazi.
Mada ni kuhusu Bashite kufanana na Trump kwa ushawishi, kuiba uchaguzi kwa CCM ni mtu yoyote hata akiwekwa Stivu Nyerere wanaweza kumpachika kuwa rais kwa nguvu ya dola lakini haimaanishi kwamba atakuwa na ushawishi wowote.
 
Da.... unamfananisha Makonda na Trump? Trump pamoja na vituko vyake lakini ana akili. Huwezi kumweka kundi moja na Makonda. Makonda bila Samia nakuhakikishia anapotea haraka sana. Ndiyo... aliweza kumlaghai hata Magufuli lakini mpaka wakati Magufuli anafariki alishamshtukia. Na mbaya zaidi ndani ya CCM ndiyo kabisaa, ana maadui kila kona. Ndiyo... Bongo tunapata marais wa ajabu ajabu lakini hata Samia kama siyo ''ajali'' asingekaa awe rais.
 
Makonda Hana Hela tu, lakini anafanana na Trump kwa mambo mengi sana.
 
Na ndivyo alivyo Trump. Hiyo base ya MAGA kwani imetokana na nini?
Trump ni populist aliyeweza kuwatimua hadi vigogo wa Republicans kama wakin Bush, Pompeo, Mike Pence, John Bolton na wengine wengi kutoka chamani kupitia nguvu ya warugaruga wa MAGA.
MAGA wapo siku zote ndani ya Marekani.
 
Ni kuota mchana kweupe kudhani makonda anaweza kuwa Rais, hata kuwa waziri mkuu au Makamu wa Rais hawezi kufika hapo
Kwani anayemfanya mtu fulani awe rais ni nani?, kama sio wewe, pia sio mimi, sio mtu yoyote!, anayefanya fulani awe kiongozi, mbunge, waziri, waziri mkuu, makamu wa rais na rais, ni YEYE, hivyo kama amepangiwa na itakuwa, na kama hajapangiwa, hawi!.
P
 
Trump anabebwa? Inaonekana haufuatilii siasa. Trump naweza mfananisha na JPM ni "cult figures" yaani watu waliojenga ufuasi either kwa mazuri au mabaya ila wana lenga target fulani ya wapiga kura.

Mfano JPM alijijenga kama mpinga ufisadi na mcha Mungu so hata kama hakua hivyo ila wale alio watarget walimkubali.

Hii ni hata kwa Trump yeye kajibrand kama America first, so masuala ya uhamiaji, misaada, foreign policy na hata jinsia amelenga population fulani ya wazungu tena wahafidhina wanaoishi majimbo ya pembezoni na hawa kawashika akili kweli maana ni wahafidhina wasiotaka mabadiliko.

Hapo hakuna kubebwa na ndio maana alishinda kwa uwazi kabisa. Ila hapa bongo ni kundi gani linamkubali Makonda? Walokole? Ilihali ndio aliwadhalilishia Gwajima kiasi kile!! Vijana hawamkubali, kiufupi hana kundi majority ambalo kalishika akili na hata hiyo 2030 akigombea hapo Arusha mjini na uchaguzi wa huru hana uwezo wa kuishinda chadema au mgombea huru yeyote.

Kumlinganisha Makonda na Trump ni matusi mzee,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…