Makonda: Sio lazima niteuliwe, ninaweza kuwa Kiongozi wa familia

Makonda: Sio lazima niteuliwe, ninaweza kuwa Kiongozi wa familia

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paulo Makonda ameibuka upya kwa kusema kuwa sio lazima apate uteuzi bali anaweza hata kuwa Kiongozi wa Familia.

“Mimi ni mkulima, ni mfanyabiashara pia kwa hiyo ninaweza kuwa na mchango mkubwa sana hata kwenye kampuni ninazoweza kufanya kazi. Siyo lazima uwe kiongozi wa kuteuliwa au wa kupigiwa kura, unaweza kuwa kiongozi hata wa familia,” amesema.

Mheshimiwa Makonda kabla ya kuachia Ukuu wa Mkoa aligombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia CCM bila mafanikio.

MCL
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paulo Makonda ameibuka upya kwa kusema kuwa sio lazima apate uteuzi bali anaweza kuwa Kiongozi wa Familia

Mheshimiwa Makonda kabla ya kuachia Ukuu wa Mkoa aligombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni bila mafanimio
Ni bora kama ameliona hilo, nasi tunatamani asirudi kututaabisha.
 
Makonda aliona kitakachomkuta Maghufuli, kimsingi mshikaj alikuwa well prepared, na wala hakukurupuka kutamani kujibanza kwenye ubunge, kuachia kwake ofisi kulifanya defense ya Jiwe DSM ishake pakubwa.
 
Back
Top Bottom