JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Saa chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa na kuwaondoa tisa, leo Alhamisi Julai 28, 2022, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amemshukuru mkuu huyo wa nchi kwa kuendelea kuhudumu katika mkoa huo na kusisitiza kuwa amenusurika.
“Rais (Samia Suluhu Hassan) amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa kwa nia njema, lakini mimi ndugu yenu nimenusurika, kama ningeondolewa ningesikitika maana ndio kwanza nimeanza kuwazoea,” - Makongoro Nyerere.
Makongoro ameyasema hayo leo hii wakati wa zaiara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa akikagua ujenzi wa miundombinu ya Shule ya Sekondari Matui Wilayani Kiteto.