Makongoro Nyerere: Nisengekuwa hapa bila Rais Samia

Makongoro Nyerere: Nisengekuwa hapa bila Rais Samia

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere Makongoro Nyerere amewataka wananchi kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao akisisitiza umuhimu wa maandalizi bora kuelekea uchaguzi ujao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na uongozi wa Mkoa, Makongoro amewataka wakazi wa Rukwa kuhakikisha kuwa wamejiandikisha na wapo tayari kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuwa na mshikamano na kutokubali kuchochewa na watu wenye nia ya kuvuruga amani ya nchi, huku akibainisha kuwa Serikali ya Mkoa ipo tayari kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na kwa kufuata sheria.​

Chanzo:Vosfm​
 
Kwa vile yeye analishwa bure na Rais kwahiyo sisi tuendelee kusherekea mafanikio yake? huyu babu pombe na sigara zimemkataa
 
Ila Makongoro sometimes anaiaibisha sana familia ya Baba wa Taifa. Kila akipewa nafasi kuongea yeye anakomaa yale yale "nimepata nafasi si kwasababu nina uwezo, hakuna jambo la maana nililofanya la kunifanya nistahili kuwa Mkuu wa Mkoa", mara "wamenipa tu kwasababu ni mtoto wa Nyerere", halafu tena "nimepata upendeleo tu kupata hii nafasi".

Brother Makongoro, acha ujinga wa kujinyenyekeza kiasi hicho. Hiyo nafasi UNASTAHILI kabisa na wala siyo kwa ajili ya upendeleo. Unataka kusema akina Mchengerwa, Ridhiwani Kikwete, Hussein Mwinyi, Joseph Sokoine, Balozi Ali Karume wao wamepatwa nafasi hizo kwasababu wana uwezo mkubwa sana? Nakukubali bro, ila kadri siku zinavyosonga unazidi kunikera. Wao mbona hawaongei hayo unayoyaongea?

Nakuuliza, hao niliowataja hapo juu wamelifanyia nini Taifa hadi wastahili hivyo vyeo, halafu wewe usistahili?
 
Jusr
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere Makongoro Nyerere amewataka wananchi kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao akisisitiza umuhimu wa maandalizi bora kuelekea uchaguzi ujao.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na uongozi wa Mkoa, Makongoro amewataka wakazi wa Rukwa kuhakikisha kuwa wamejiandikisha na wapo tayari kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuwa na mshikamano na kutokubali kuchochewa na watu wenye nia ya kuvuruga amani ya nchi, huku akibainisha kuwa Serikali ya Mkoa ipo tayari kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na kwa kufuata sheria.​
View attachment 3371495
Chanzo:Vosfm​
Another pwaguzi
 
Back
Top Bottom